Log in
MWANZA TRANSPORTERS ASSOCIATION

MWANZA TRANSPORTERS ASSOCIATION

JIJINI MWANZA, Tanzania

Parts of this page are in Swahili. Edit translations

Hapa Tanzania, miaka ya nyuma, kabla ya mwaka 2003 huduma ya Usafirishaji ilikuwa inasimamiwa na Mamlaka ya Leseni Tanzania. Mamlaka hii, kwa kipindi chote ofisi zake zilikuwa ndani ya majengo ya serikali, kwa wakuu wa Mikoa. Hivyo, kila mkoa ulipewa himaya ilio sawa na eneo la utawala wanao miliki kiutawala wakati huo na kujulikana hivyo. Kwa hapa Mwanza, kulijulikana kisheria kama MWANZA REGION TRANSPORTATION LICENCING AUTHOURITY - MRTLA. Mamlaka ya mkoa ilikuwa na majukumua ya kutoa leseni za usafiri za ndani ya mkoa wake tu. Safari za kwenda kuishia nje ya mkoa ziliratibiwa makao makuu ya Mamlaka - Dar es Salaam.

Mabadiliko kwenye Sera ya Taifa ya Usafirishaji, Siasa ya nchi, mabadiliko ya kiuchumi na sababu nyingine nyingi kimataifa, zilihalisi serikali ilipeleka rasimu za sheria kadhaa kuunda MAMLAKA ZA UDHIBITI - ( REGULATORY AUTHORITIES ) na kujafuta zilizokuwepo zamani. Mamlaka hizo za Udhibiti ziko nyingi, na zimesambaa kwenye wizara mbali mbali zikiwemo EUWRA, TFDA, FCC, SUMATRA n.k. Kuingia kwa SUMATRA, kwanza kulifuta TLA, na ndio iliochukua jukumu la Kutoa Leseni kwa vyombo vyote vya Usafirishaji Tanzania kwa mujibu wa SURA ya 413 ya Sheria za Jamhuri ya Tanzania. Sheria tajwa juu, pia iliingiza usimamizi wa Reli na Vyombo vitumikavyo kusafiri kwenye Maji chini ya Mwemvuli mmoja.

Sheria hizo mpya ndio zilio tambua uwepo wa Wadau na kuwahamasisha kuwa nao karibu kwa lengo la kubadilisha uzoefu na kutatua changamoto zinazo kabili tasnia hiyo ya usafiri Tanzania kwa kuegemea TARATIBU SHIRIKISHI. Kuendana na mahitaji ya kuweza kufikisha mawazo yetu kwa pamoja, wamiliki wa vyombo vya usafirishaji Mwanza tuliitana hapo mwanzoni mwa 2008 kwa kikao cha kwanza na baadae vikao vingine vilifata hadi tulipofanikiwa kuitisha Mkutano wa kutengeneza Katiba. Katiba yetu ilipita kamati na usanifu sehemu kadhaa hadi tulipo fanikiwa kwenda isajiri Dar es Saalam mwaka huo huo na kupewa HATI.

Toka kipindi hicho,tumekuwa tukishirikiana na Wadau wenzetu mbali mbali kuhakikisha huduma za usafiri Jijini zinakuwa :-

                                a) Bora na zinatolewa na vyombo vyenye viwango

                                b) Zinapatikana kwa makundi yote

                                c) Huduma inayo zingati Hadhi na Heshima kwa binadamu wenzetu