Log in
Mpotola Secondary School

Mpotola Secondary School

NEWALA, Tanzania

Parts of this page are in Swahili. Edit translations

Shule ya sekondari Mpotola ilianzishwa kwa nguvu za wananchi mnamo Mwaka 2006 tarehe 16 Januari, Baadaya ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Ndg Ishidor Shirima akiongozana na Afisa elimu wa Mkoa wa Mtwara Ndg Wahab Essay kuridhishwa na kufurahishwa na juhudi za wanakijiji wa Mandala kujenga shule yao ya Msingi iliyosababisha kuhama katika eneo la sekondari hii na kuhamia eneo lenye majengo mapya.

Ili kutopoteza historia ndipo Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa akatoa zawadi kwa wanakijiji wa kata ya Kitangari wajenge Shule ya Sekondari katika eneo la majengo yaliyoachwa na ambayo yalikuwa machakavu.

Hapa shule ilianza kujengwa kwa michango mbalimbali ya wananchi kwa kiasi kikubwa ikichangiwa nan mavuno ya Korosho hivyo kukatwa Tshs 10/= kwa kila kilo ya Korosho ambayo imeiwezesha shule kufikia kuwa na madarasa 8 ya nguvu za wananchi na 2 ya serikali kuu. Pia shule ina Nyumba 2 za walimu na matundu ya vyoo 12. Shule inakosa majengo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Maabara kwa masomo yote ya sayansi, Jengo la utawala, bwalo, mabweni, Ofisi za Idara, Maktaba na Ofisi za ushauri shule haina Jiko wala ukumbi wa mikutano

Kwa sasa Shule ina wanafunzi 604 kati yao wasichana ni 297 na wavulana 307 ina walimu 6 na wafanyakazi wa muda ambao hulipwa kwa michango ya wananchi 3

Kupitia tovuti hii shule inakusudia kuendelea kupanua wigo wa mradi wake wa ujenzi wa madarasa, Maabara, jengo la utawala na Mabweni.

Shule inaomba kwa mashirika hisani kusaidia katika hili ili shule iweze kufikia malengo yake ya kufikia kipeo cha maendeleo na kufuta umaskini kwa wananchi wa kitangari na Tanzania kwa ujumla