Log in
Umoja wa Wawezeshaji Kioo

Umoja wa Wawezeshaji Kioo

Ilagala, Tanzania

Parts of this page are in Swahili. Edit translations

Kioo ni nini!

Mbura Chiragwile (Kigoma Town)
July 28, 2011 at 9:03 AM EAT

Naleta hoja kioo ni nini

Edward (Ilagala)
July 28, 2011 at 10:50 PM EAT (edited March 26, 2012 at 8:06 AM EAT)

@Mbura Chiragwile (Kigoma Town): 

Abdallah Mohamed Ramadhani (USAGARA,MISUNGWI, MWANZA,TANZANIA)
August 29, 2011 at 10:21 PM EAT (edited March 26, 2012 at 8:06 AM EAT)

Nani anaombwa ridhaa ya katiba mpya?nani amekataa katiba mpya? nani anapaswa akubali ili katiba mpya iwepo?haya maswali na maswali mengine mengi ni baadhi ya maswali ambayo watanzania nikiwemo mimi binafsi tunajiuliza.kwani madai ya katiba yasiwe kivuli, lazima tusimame imara kuhakikisha kwamba haki na uhuru wetu na maslahi ya watanzania hayaathiriwi na matumizi mabaya ya uhuru na haki zetu,si viongozi wqa kisiasa kwa maana ya mheshimiwa Kikwete,slaa,mheshimiwa mbowe,lipumba, asasi za kiraia za nje na ndani wanauwezo wa kuwaamulia watanzania eti kisa tu wanalojukwaa la kusemeya.si sahihi wanasiasa wawaamulie wananchi kwani tumeshuhudia wanasiasa wengi wanatawaliwa na maslahi binafsi hivyo wana chembechembe za kifisadi,sasa hapo inakuwaje? hivyo si haki kuwaamulia watanzania namna katiba inavyopaswa kuwa,mtu anaweza akatoa rasimu ya katiba mpya kwa mtizamo wake ,na anavyodhani katiba iwe sio kila anayetoa madai ya katiba mpya ana nia njema na maslahi ya watanzania,na sikweli kwamba mawazo ya watu juu ya mbadala wa vifungu vya katiba yote yana tija,hebu tafadhali tuondoe mbwembwe za kisiasa na usanii katika suala hili nyeti lenye athari kwa vizazi vilivyopo sasa na vijavyo je tuko pamoja kwa dhati  na ukweli wa mungu kuwa tunatafuta katiba ya kitanzania? maana naona bado tuna pata suluba zakifikra pamoja na usomi tunaodai tunao,na wataalamu tunaodai tunao,kwani takribani miaka 50 sasa imepita hata kwa kupima kwa vigezo ambavyo wakati ule kutokana nahila zao za kitapeli,kinyonyaji,kibeberu  kikoloni na udanganyifu hatukuvijua lakini sasawananchi  wanavijua,wasomi wanavijua na serikali pia inavijuatoka kabla ya uhuru,basi ni vyema  fursa ya kuandaa katiba mpya izingatie maslahi ya watanzania wa aina zote yaani walionacho na wasionacho na sio Magod father wa wanasiasa,na sio kinachalabi watanzania.Maana mtanzania wa leo tena msomi mwenye uzalendo na kiu ya mabadiliko yenye tija ya nchi yake sio ili mradi mabadiliko hatawaliwi kifikra,sio lazima akopi na kupaste kutoka ughaibuni kwani hata mazingira hayafanani,tusilazimishe mambo ya watu tuaproach katiba kitanzania na sio kimarekani walakiingereza , na tuwe wabunifu kulingana na utanzania wetu na sio visasi,na kuingiza milija mipya ya wanyonyaji,bali katiba itakayotumika kuondoa  milija hiyo ya sas naya zamani sambamba na kulinda raslimali za taifa letu.

Mwalimu Nyerere aliwahi kusema jumamosi  ya mei 30, 1969 katika ukumbi wa diamondjubilie hotuba ambayo aliitoa kwa walimu waliohudhuria sherehe za vijana nakumbuka alisema  hivi namnukuu.

     '' jitihada tunayojaribu kufanya sasa ni jitihada kubwa;na tunajaribu  kuona kama viongozi wetu wataelewa nini hasa tunachojaribu kufanya si kuelewa juu juu tu,lakini kuelewa kwa kwelikweli ,kwa dhati,nini tunajaribu kufanya.na namna ya kueleza upya.''sasa kwa maneno ya Mwalimu nyerere na kwa hali ya kimbunga cha mabadiliko ,na madai ya katiba mpya ni lazima wadau wote,yaani wananchi waelewe wazi jitihada ambayo wanasiasa,wanazuoni,mawakala watanzania na wasio watanzania wanachojaribu kukifanya sasa,lakini kubwa zaidi na la msingi ni kujaribu kuona kama viongozi wetu wanaelewa wanachojaribu kufanya sasa katika mabadiliko ya katiba au katiba mpya.si kuelewa juu juu tu,kuhusiana na udhaifu,mapungufu na athari za vifungu ambavyo vinatumika kama viashiria vya ubovu wa katiba tuliyonayo sasa , lakini ni kuelewa kwa kwelikweli,kwa dhati nini kinapaswa kufanyika na kwa maslahi ya watanzania na sio mabwanyenye na na mawakala wao. pia waweze kueleza matarajio ya mapendekezo ya vifungu vipya na mahitaji ya katiba inyotosheleza mahitaji ya watanzania wote na sio kuongozwa na fikra tegemezi mfu za watanzania waliokufa kiakili,wakitegemea remote control kutoka uingereza na marekani.katiba mpya itadhihirisha uhuru wetu hasa wa kifikra na kujiamulia mabo yetu wenyewe..

lakini mwl nyerere hakuishia hapo alikazia hotuba yake na kusema'tunasema tunataka  kufanya mapinduzi .' na alitahadhalisha kwa kusema kuwa "sikuhizi neno mapinduzi linapendelewa sana  mengine sio mapinduzi;mengine ni maasitu,nayo yanaitwa mapinduzi! lakini nasema tunataka kufanya mapinduzi; na ni kweli tunataka kufanya mapinduzi.lakini kwanini tunataka kufanya mapinduzi? inafaa kurudi nyuma kidogo,kutazama kwa nini lazima tufanye mapinduzi."

Namimi naamini naamini hata leo na wakati huu mjadala wa katiba  mpya umepamba moto baada ya wakoloni wetu waliotuachia msingi wa katiba tuliyonayonayo,ambayo imewalipa sana kuliko walivyotarajia,bila shaka mpango wa kazi ulikuwa unaanzia  kwa wenzetu wa Kenya na wamemaliza kwa mafanikio sas ni zamu yetu tutakwepaje? hivyo juu ya hili tuwe makini katiba yetu tuitengeneze kwa kuzingatia maslahi ya watanzania tuwaepuke vijibwa vinavyotumika na kuwezeshwa ili kuleta matokeo ya katiba dhaifu inayokumbatia wanyonyaji, wakoloni mamboleo. maana mtu mmoja aliniumiza kichwa alivyosema kuwa hakuna haja ya mchakato wa kura za maoni ya wanachi wote , kukusanya maoni ya wananchi eti ni kupoteza mda wakati eti katiba imeshaletwa  mpya imechapwa na kuandaliwa na hao Magodfather wa watu na sasa kinachofanyika ni semina elekezi na kutawanya fedha ya kuendeshea ushawishi na utetezi wa vifungu muhimu vilivyolengwa na  hao mabwana mkubwa!  na ushawishi huo utendeshwa na asasi na taaasisi mbalimbali zilizopo nchini za ndani na nje  kwa kisingizio cha elimu juu ya katiba  kwa wananchi hivyo asasi zipo katika mchakato wa mafunzo ya jitihada za kuendesha ushawishi na utetezi wa mabvwana mkubwa hao sasa sijui tulijikomboa kwa lipi? mbona hatuamui mambo yetu wenyewe? Nadhani sasa tunapaswa kupigania zaidi uhuru wa kifikra,na tukomboe fikra zetu,na wasiwasi tatizo hili ni kubwa zaidi.maana kama hazitutoshi vileeti kuna watu wanaamini fikra zao kuongozwa na mtandao wa wikileaks,na bado mtu anaupa hadhi wa kuongoza fikra zake na anashawishi habari za mtandao huo wa kijasusi zitumike kama vigezo vya maamuzi ya muhimu ya nchi! na mtanzania hajiulizi maslahi ya anayetoa siri hiyo ni yapi? na atanufaikaje na kuvuja kwa siri hiyo wakati yey sio mtanzania .kurukia habari za kijasusi ambazo hutolewa  kwa malengo ya kibeberu lazima watanzania wawe macho kwani hat  Saddamu naye aliponzwa na habari za aina hii, habari zilisema ana silaha za maangamizi walimwengu wakarukia na kumuuadhibu watoto wasio nahatia walikufa kwa gharama ya habari hiyo ya uongo na hadi leo bado mambo si shwari ,lakini sio mimi wala wamarekaqni wenyewe wameshuhudia silaha za maangamizi.hakuna mtu duniani anayeweza kutoa siri bila kuwa na maslahi na kuvuja kwa siri hiyo sasa mimi na wewe tanzania tujiulize kuna maslahi gani kwa marekani katika hili? naona hii kama scramble of natura resource iliyopo tanzania  na hekaya ya abunuwasi wa kileo,sababu za mamlaka makubwa ya raisi,kushindwa kumshitaki rais mkapa naviongozi wengine wastaafu, mgombea binafsi sijui kwa maslahi ya nani? mabinafsi wote? matajiri wote? maskini wote? kama mtu hawezi kuungana hata na cham kimoja cha siasa atawezaje kuungana na watanzania wengi kuleta maendeleo ,eti hiyo nayo inapewa baraka za demokrasia,mi nadhani maana ya demokrasia inapanuliwa isivyo uhalisia kwa maslahi ya wabinafsi. kudhibitiwa kwa bunge na  serikali,raisi kuvunja bunge kutoridhishwa watu na uteuzi wa rais,sio dira ya katiba mpya, mi naona dira yetu ni katiba mpya inayokidhi maslahi ya watanzania wote na sio kundi la watu,katiba itakayolinda haki ya kila mtanzania bila kuathiri haki ya mtanzania mwingine,katiba itakayoleta usawa na haki ,umoja wa kitaifa,itakayojenga uzalendo,itakayochochea ukombozi wa kifikra,katiba itakayoundwa bila kutumia mitizamo ya visasi katika kuiandaa na katiba isiyo kwa maslahi ya ukoloni mamboleo,itakayolinda raslimali za watanzania,katiba itakayoondoa utumwa wa kifkra na matamanio ya maslahi binafsi,maana uzoefu unaonyesha  viongozi wengi wa kisiasa wananyanyasa utanzania wao na hawaruhusu fikra mpya kupenya, fikra zao kama maroboti. basi madhari tumeyaona haya basi mapinduzi yetu ya kifikra hayana budi yawe makini hatuna budi tujenge watanzania wapya,ambao hawatakuwa na utumwa wa kifkra,na unyonge wowote ule,na kazi ya kuunda mtanzania mpya itarahisishwa na kutengeneza katiba mpya ya kitanzania maana tulitaka uhuru ili tuwe watanzania na sio uhuru wa kuwa waingereza ama wamarekani.uhuru wa kitumwa hauna nafasi wala tija,unatumwa na unahusudu kutumika na hili linajitokeza katika jitihada za kutaka kutambulika na bado kuna jitihada nyingi za wanasiasa wa kitanzania,viongozi,wanazuoni kujipendekeza kupitia vyama vyao,asasi zao, taasisizao jumuia zao dini zao na vikundi vyao. wachina wanawaita watu kama hao running dogs yaani vijibwa.hivyo ni vyema kuwa running dogs wa watu GODFATHER.Kazi ya kwanza ni kukataa kuwa running dogs katika uundaji wa katiba mpya ni vyema watanzania wakafanya urafiki na marafiki na watu wa nje lakini si kuwa running dogs ,sivyema kuwa running dogs wa nchi za ughaibuni..namalizia kwa maneno ya mwalimu nyerere aliyosema november24,1970 huko bagamoyo akifungua semina ya maofisa wa jeshi alisema"Hatutazamii kijana wetu,awe katika jeshi,awe katika youthleague,au mahali popote,kwamba kijana wa TANU au AFRO-SHIRAZI PART awe running dogs wa mtu mwingine.na akasema lazima nchi zote duniani zijue kuwa msingi wa kushirikiana  na watanzania ndio huo,kila siku tunataka uhuru wa kudumisha mila zetu,tunataka uhuru wa mambo ya kisiasa,na tunataka uhuru wa kuendeleza imani zetu.lakini hatuwezi hatuwezi kuwa running dogs"

kwa maana hiyohiyo katika suala la katiba mpya ninawaomba watanzania,vijana,wazee,awe katika jeshi,awe katika vyama vya siasa yaani CCM,CHADEMA,CUF,TLP,NCCR-MAGEUZI,NGOS,CBOS,Taasisi za kidini,vyombo vya habari na wabunge kamwe wasikubali kuwa marunning dogs[vijibwa] katika mchakato wa katiba mpya ya tanzania na watanzania na vbiongozi makini hawatazamii kuona wanakuwa vijibwa vya watu wengine,hata kidogo.tena itawaudhoi watanzania na wataona wamefanya kazi bure,jambo jema la muhimu ni kuhakikisha watanzania wanaachiwa jeuri ya uhuru wao na amani yao .. running dogs hapana.

   haya nia maoni yangu na  mtizamo wangu huru

Abdullah Mohammed Ramadhani

 

Godlisten Msaki (Nyengedi)
September 24, 2011 at 4:20 PM EAT (edited March 26, 2012 at 8:07 AM EAT)

ahsante kwa maono yako, lakini kubwa watanzania hatuijui katiba ya zamani mpya tutaiiteteaje au tunajua ina mapungufu gani. wakati hata cover yake mimi nimeiona mwaka jana. Tufundishwe katiba ya zamani tuone mapungufu yake halafu tutoe maoni


Add New Message

Invite people to participate