Habari wadau wa Maendeleo.
Napenda kuchukua fursa hii kuwasalimia na kuwatakia maandalizi ya sikukuu zijazo mbeleni,lakini pia kuhakikisha mnaipitia upya mipango kazi tayari kwa maboresho kwa mwaka mpya ujao.
Changamoto kubwa iliyoko mbele yetu ni upashanaji wa habari ambayo bado inasumbua sana na hatupashani habari kwa wakati lakini pia mwaka mpya unaokuja tujenge tabia ya kutembeleana na kubadilishana uzoefu
Naomba niishie hapo
Ramadhan Omary
Mkiurugenzi
Kijogoo Group for Community Development
Tell 0754 948 767 & 0715 948 797
Habari zenu wadau,
Kijogoo Group for Community Development Imebahatika kuwasilisha maombi ya ruzuku ubalozi wa Ufaranza,hivyo na hamasisha wadau wote tutumie fursa hii kutuma maombi ya Ruzuku ili tuweze kuisaidia Nchi katika kupambana na mabadiliko ya Tabia Nchi na kusaidia Jamii inayoishi katika mazingira magumu ili sote tusonge mbele na kupiga hatua za kimaendeleo.
Asanteni sana
Ramadhan said
Mkurugenzi
Kijogoo Group for Community Development
Timu ya ufuatiliaji wa maendeleo na matokeo ya mradi kutoka Kijogoo Group ikiongozwa na Mkurugenzi wake Bwana Ramadhan Omary,Bwana Rajabu Msumi,mwandishi wa habari Bwana Thadei Hafigwa,Bwana Mohamed Nguku na Bi Ignita pamoja Bi Christina Mdaku wakifanya mahojiano na mtu mmojammoja na vikundi
Katika utekelezaji wa shughuli zetu tuliweza kutembelea Ofisi za Serikali kujitambulisha na Mkurugenzi wa Kijogoo Group akisaini kitabu cha wageni kwenye Ofisi ya Afisa Mtendaji kata ya Nawenge
Katika Jambo lolote lile changamoto hazikosekani,hapa usafiri tuliokuwa tukiutumia umenasa kwenye tope zito baada ya miundo mbinu ya barabara kuharibika vibaya kutokana na mvua zilizokuwa zikinyesha wakati huo
Bwana Thadei Hafigwa mwandishi wa habari za makala tunayemtumia katika utekelezaji wa shughuli zetu akiwa darasani kufuatilia kwa umakini ili apate ya kuandika ni mwandishi wa Gazeti la Jambo Leo
Hii picha ya Pamoja kati ya Mkurugenzi wa Kijogoo Group for Community Development Bwana Ramadhan Omary aliye chuchumaa mbele Akiwa na timu ya UUJ/SAM iliyotokana na mafunzo yaliyotolewa na shirika hilo Wilayani Ulanga .Wajumbe hao Wametoka Kata za Nawenge na Msogezi
Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Ulanga akifungua mafunzo ya siku 4 kwa Wananchi,Viongozi wa serikali za Mitaa,Wajumbe wa Kamati za Afya za Kata na wadau wa Afya ambayo yameandaliwa na Shirika la Kijogoo Group Kwa Ufadhili wa The Foundation For Civil Society ya Dar Es Salaam
Pichani aliye simama ni Mkurugenzi wa Kijogoo Group For Community Bwana Ramadhan Omary Akitoa maelezo kuhusu mradi wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji wa Jamii Sekta ya Afya kwa washiriki wa mafunzo hayo 40 kutoka Kata ya Nawenge