Parts of this page are in Swahili. Edit translations
Habari zenu wadau,
Kijogoo Group for Community Development Imebahatika kuwasilisha maombi ya ruzuku ubalozi wa Ufaranza,hivyo na hamasisha wadau wote tutumie fursa hii kutuma maombi ya Ruzuku ili tuweze kuisaidia Nchi katika kupambana na mabadiliko ya Tabia Nchi na kusaidia Jamii inayoishi katika mazingira magumu ili sote tusonge mbele na kupiga hatua za kimaendeleo.
Asanteni sana
Ramadhan said
Mkurugenzi
Kijogoo Group for Community Development
June 1, 2016
Comments (2)
Asante
Tangazo hili limetolewa na
Mkurugenzi
Bwana Ramadhan Omary
Utafiti uliofanywa na shirika letu kwa kushirikiana na Viongozi na Watendaji wa Serikali ngazi ya Vijiji na Kata wakazi waishio kwenye kata hizo bado wamekuwa wakiendeleza mila zilizopitwa na wakati na tohara hasa kwa wanawake na wamebadili tabia sasa wana wakeketa wakiwa wadogo wanaosoma darasa la kwanza na la pili.
Hali imekuwa ikidhalilisha utu wa mtoto na kumkosea haki zake za msingi hivyo tunawaomba wadau mtakaoguswa na ujumbe huu mtusapoti kifedha ili twende tukaweke kambi ya kutokomeza hali hiyo kwa kuendesha elimu kwa njia ya makongamano na sanaa shirikishi jamii.
Ni mategemeo yetu wadau,mashirika ya ndani na nje,wafadhili wa ndani na nje na serikali pia mtatuunga mkono kwa hili lililopo kwenye jamii ya watu wa Wilaya ya Gairo inayoongozwa na kabila la Wakagulu
Maombi haya yametolewa na
Ramadhan Omary
Mkurugenzi
Kijogoo Group For Community Development
Simu namba 0754 948 767 & 0715 947 897
Email - kijogoogcd@yahoo.com au ramadhankgcd@yahoo.com