Timu ya Dira Theatre Group na wasamaria wema wakisaidiana kuinasua gari walilokuwa wakisafiria lililokwama kwenye tope. Hii ni katika kijiji cha Ibindo, wilayani Kilosa.
Timu ya Dira Theatre Group katika harakati za kuifikia jamii vijijini. Hapa wakilazimika kutembea kwa miguu baada ya gari lao kukwama kutokana na ubovu wa barabara. Hii ni kuelekea kijiji cha Inyunywe, wilaya ya Kilosa.
Viongozi wa Dira Theatre Group, kutoka kushoto, Asha waziri, Erasmo Tullo, Deogratius swai na Saada Juma, katika pilika za uelimishaji wa jamii vijijini.
Viongozi wa Dira Theatre na washiriki wa mafunzo wakiwa katika picha ya pamoja, kata ya Rudewa, wilaya ya Kilosa, mkoani Morogoro.
Picha ya pamoja ya viongozi wa Dira Theatre na washiriki wa mafunzo ya sera na sheria za ardhi kutoka vijiji vya kata ya Kimamba,wilayani Kilosa mkoani Morogoro.
Picha ya pamoja ya viongozi wa Dira Theatre na washiriki wa mafunzo ya sera na sheria za ardhi kutoka vijiji vya kata ya Mamboya, wilayani Kilosa.
Picha ya pamoja ya washiriki wa mafunzo ya sera na sheria za ardhi kutoka vijiji vya kata ya Maguha.
Diwani wa kata ya Maguha Ndg. Dickson Magoma akieleza jambo kwa washiriki wa mafunzo ya sera na sheria za ardhi (hawapo pichani) yaliyoendeshwa na Dira Theatre kwa ufadhili wa The foundation for Civil Society (FCS).
Meneja wa Dira Theatre Ndg. Erasmo Tullo (aliyesimama) akitoa maelezo kwa wajumbe wa mabaraza ya ardhi ya vijiji juu ya utekelezaji wa sera na sheria za ardhi.