Log in
dhulusportsclub

dhulusportsclub

mwanzacity, Tanzania

PROJECTS ZA DHULU SPORTS CLUB:

 

Projects kuu tunazojiusisha nazo ni

  • Utafutaji na Uendelezaji vipaji kwa vijana wa kitanzania.

Kamati husika katika Club itashirikiana na meneja wa michezo katika kutimiza lengo kuu la kuvipata na kuviendeleza vipaji. Kwa kupitia mafunzo na Mabonanza mbalimbali yatakayo andaliwa na club, vijana wenye vipaji kutoka shule mbali mbali katika mkoa husika watapatikana na kutengeneza timu bora za Dhulu Sports Club (mfano timu bora ya mpira wa miguu itapatikana kwa kuchukua wachezaji wenye vipaji kutoka katika shule mbalimbali na mitaani).Hivyo club itachukua jukumu la kuviendeleza vipaji hivyo ili kuvifanya kuwa chanzo cha ajira.

 

  • Utoaji wa elimu ya afya kwa vijana.

Dhulu Sports Club kwa kupitia kamati yake ya afya na nidhamu inatoa elimu ya afya kwenye shule zilizoitikia wito wa club na kwa vijana wa mitaani.

Elimu italenga juu ya kujikinga na utimiaji wa dawa za kulevya na maambukizi ya ukimwi kwa vijana.