Log in
dhulusportsclub

dhulusportsclub

mwanzacity, Tanzania

Parts of this page are in Swahili. Edit translations

HISTORIA YA DHULU SPORTS CLUB:

       Dhulu Sports Club ni club inayojishughulisha na kutafuta, kuendeleza vipaji pamoja na kutoa semina za afya na dawa za kulevya kwa vijana wa Tanzania.

Michezo tunayojiusisha nayo ni mpira wa miguu,kikapu,pete,wavu, riadha pamoja na muziki.

       Dhulu Sports Club imetokana na timu ya mpira wa miguu iliyojulikana kama GOLA FC ambayo ilikuwa ikishiriki katika mashindano mbali mbali ya ngazi za chini katika jiji la Mwanza. Dhulu ni neno la kibantu lenye maana ya mabadiliko. Hivyo miongoni mwa wachezaji katika GOLA FC ndiyo waliohusika katika kuanzisha Dhulu Youth Club. Kutokana na club kuwa na vijana wengi wa kujituma na wenye kutaka mabadiliko jina la Dhulu Youth Club lilipendekezwa kuienzi GOLA FC.

    Mwaka 2009 baadhi ya waliokuwa wachezaji wa GOLA FC waliokuwa wameenda mikoani (Nje ya mwanza) kimasomo na kishughuli walipata kukutana na wenzao wakati wa rikizo mkoani Mwanza akiwemo mwenyekiti wao wa sasa Bw. Habibu Hassan na wakafanya majadiliano yakubadilisha jina la Dhulu Youth Club kuwa Dhulu Sports Club.Wazo hili lilikuja kutokana na kwamba waanzilishi hawa walikuwa wakipenda michezo tofauti tofauti hivyo ilibidi michezo kama mpira wa miguu, mpira wa pete, mpira wa kikapu, mpira wa wavu, riadha na muziki viwemo katika club hii. Kwa wakati huo Club ilikuwa na wanachama wasiozidi 40.

Hivyo mwanzoni mwa mwaka 2010 utaratibu wa kuisajiri club ulifanyika na mwezi wa    kumi na moja mwaka 2010 Dhulu Sports Club ilisajiriwa chini ya “National sports council of Tanzania act,1967” na kupewa cheti cha usajiri chenye usajiri namba nsc964 na kutambulika kitaifa kuwa ni miongoni wa clubs za michezo Tanzania.

Kwasasa Club ina ofisi zake katika Mkoa wa Mwanza Wilaya ya Nyamagana mtaa wa Uhuru ikiwa na wanachama zaidi ya 150.

   Karibuni Dhulu Sports Club tuwasaidie vijana na tuisaidie Tanzania katika Michezo na Mapambano ya dawa za Kulevya na Ukimwi

AHSANTENI

PAMOJA TUNAWEZA