- USULI
Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) ni chama kilichoanzishwa na Viziwi wenyewe mwaka 1983 na kusajiliwa rasmi na Wizara ya Mambo ya Ndani tarehe 04/09/1984 na kupewa no so. 6466 na baaada ya kupitishwa kwa sheria ya Uanzishwaji wa vyama vya kiraia ya mwaka 2002, CHAVITA ilipata hati namba NGO 1878 tarehe 21/04/2006.
Kwa sasa CHAVITA ina Matawi 17 kwenye Mikoa 17 ya Tanzania bara ambayo ni Mwanza Shinyanga, Mara, Kagera, Dodoma, Tabora, Kigoma, Arusha, Tanga, Mbeya, Iringa, Ruvuma, Morogoro, Pwani, Mtwara, Kilimanjaro na Dar Es Salaam.
CHAVITA Tawi la Dodoma lilianzishwa February 1992, toka kuanzishwa kwake limekuwa likiunua maisha ya Viziwi wa Mkoa wa dodoma katika kupiga vita Umaskini na Unyanyampaa pamoja na kupigani a haki zote za kibinadamu kwenye nyanya zote za maisha ya Viziwi zikiwapo shughuli za mapambano dhidi ya kuenea kwa Maambukizi ya VVU/UKIMWI na kutoa ushauri nasaha kwa waathirika Ili kufanikisha shughuli za utetetezi na ushawishi na kuhakikisha kwamba Viziwi wana Maisha bora CHAVITA-Mkoa wa Dodoma inasisititiza utekelezaji wa utume na Dira za CHAVITA zinazoongoza Matawi yote nchini. Na kwa sasa CHAVITA-Dodoma imejidhatiti katika kutoa huduma katika Wilaya zote sita (6) za Mkoa wa Dodoma ambazo ni Mpwapwa,Kongwa,Chamwino,Dodoma mjini,Bahi na kondoa