Envaya

DAKAWA PERFOMING ARTS ORG Ilianzishwa mwaka 2007 kikiwa ni kikundi kidogo cha wasanii kilicholenga awali kutoa elimukwa jamii kwa kutumia mbinu ya sanaa hasa sanaa shirikishi kwa maendeleo ya jamii.

Kikundi kilianza kikiwa na wasanii sita waanzilishi na wasanii waalikwa sita.

Kilifanya kazi zake za awli kwa ushirikiano na mashirika mabalimbali ambayo ni wadau wa maendeleo ya jamii,kwa kiwango cha ufanisi wa hali yajuu huku kikiwa na mfumo wa  " utendaji na kujifunza"

Hadi kufikia mwaka 2009 kikundi kikiwa na usajili wa kudumu kikawa na mpango mkakati wa kuenea na kutanua uwanda wa kiiutendaji hivyo kuamua kuunda shirika mama la kiamaendeleona kiuchumi llinalotambulika kama DAKAWA ECONOMIC DEVELOPMENT ORGANIZATION .{DAKEDEO} Huku kikundi kikibaki na jukumu lake kuu la kuona kuwa utamaduni wa mtanzania haupopolewi na mabadiliko ya utandawazi unaotokea duniani.

-kwa sasa DAPEA ni shirika mwanachama wa DAKEDEO na mshirika mkuu wa SHIRIKA MAMA HILO,

Ifahamike kimuundo DAPEA pamoja na kuwa mwanachama wa shirika mama la DAKEDEO  lina chombo kamili cha uongozi,Uongozi pamoja na Katiba kanunu na taratibu za kiiuendeshaji zinazojitegemea,