Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Igiswayire. Edit translations
Kupitia mradi wake wa 'TEGEMEZA' inaendesha kampeni juu ya kujikinga na maambukizi ya VVU/UKIMWI, katika programu hii COLD imedhamiria kueneza ufahamu wa jinsi ya kujikinga ili kupunguza maambukizi mapya nchini Tanzania. Mpango huu unalenga kuondoa imani potofu kuhusu VVU/UKIMWI na kuhakikisha kuwa jamii ina habari sahihi zitakazowasaidia kufanya maamuzi sahihi. Mpango huu umekusudia:- 1. Kuhamasisha jamii kufikiri kuhusu mapenzi na kuwaruhusu kutathmini madhara yatokanayo na aina yoyote ya mapenzi. 2. Kuwafundisha watu jinsi ya kupunguza madhara ya maambukizi kwa kuwahamasisha kuacha ngono, kuchelewa kujiingiza katika vitendo vya ngono, kutumia kondomu na kupunguza idadi ya wenzi wao. 3. Kuwapa watu ujasiri na silaha ili waweze kujadiliana na wenzi wao kuhusu suala la mapenzi. 4. Kuwasaidia watu kuelewa madhara ya kuwa muathirika na kuhamasisha kutunza afya zao kwa kadri iwezekanavyo ili kupunguza uwezekano wa kuambukizwa. 5. Kuwapa ufahamu walezi namna ya kuwahudumia waathirika wa VVU/UKIMWI walio majumbani.
2 Nyakanga, 2011