Maeneo ya ukurasa huu ni kwa Kiingereza. Hariri tafsiri
Maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika
Community Organization for Life and Development "COLD" imeshiriki kikamilifu katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika ambayo yameadhimishwa kimkoa katika kata ya Bugarama wilaya ya Kahama, ambapo mgeni rasmi amekuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Brigedia Jenerali mstaafu, Dk. Yohana Balele. COLD imetoa msaada wa sare za shule na madaftari hamsini na tano kwa watoto yatima wanaoishi katika mazingira magumu kumi na mmoja, wavulana watano na wasichana sita wanaosoma katika shule ya msingi Bugarama ambazo wamekabidhiwa na mgeni rasmi. Mgeni rasmi amelipongeza sana shirika hili kwa juhudi zake na kuahidi kuwa yuko tayari kulisaidia kistadi na kiushauri. Pia mgeni rasmi amekabidhi hundi ya shilingi mia tano elfu kwa mkurugenzi mtendaji wa COLD Bw. Kisumva Mathew Maziku ukiwa ni msaada wa kuunga mkono jitihada za shirika kutoka halmashauri ya wilaya ya Kahama.16 Juni, 2011