UTAMBULISHO
Chama cha Wazazi wa Watoto wenye Ulemavu wa Mtindio wa Ubongo, Akili na Viungo Tanzania (CHAWAUMAVITA) ni chama kilichoanzishwa mwezi Aprili 2012,Tumefanikiwa kupata usajili mwezi april 2013 namba S.A 18732.
Tunaamini-“Umoja daima ndio suluhisho kwa changamoto”
Dira ya CHAWAUMAVITA ni kuwa CHAMA cha mfano kitachochangia upatikanaji wa huduma bora na endelevu kwa watoto wenye Ulemavu wa Mtindio wa Ubongo, akili na Viungo Tanzania ili kuhakikisha watoto wenye Ulemavu wa Mtindio wa Ubongo, akili na Viungo wanasaidiwa kukabiliana na changamoto zilizopo na kuandaa mazingira bora ya makuzi na maisha yao kwa ujumla
Malengo ya CHAWAUMAVITA ni
- Kuwaleta pamoja watu/familia zinazolea watoto wenye ulemavu wa mtindio wa Ubongo,akili na viungo ili kubadilishana uzoefu, kupata elimu ya namna ya kuwatunza watoto wenye ulemavu wa Mtindio wa Ubongo akili na viungo.
- Kutoa elimu ya ulemavu wa Mtindio wa Ubongo na Viungo ili Kupunguza athari na maumivu yatokanayo na Mtindio wa Ubongo ,akili na viungo.
- Kukusanya, kuchapisha na kusambaza taarifa zinazohusu matatizo yatokanayo na ulemavu wa Mtindio wa Ubongo,akili na viungo.
- Kuwasaidia wanachama/wazazi katika kuwatunza na kutetea na kupata haki zao kwa mujibu wa sheria.
Tunatanguliza shukrani zetu za dhati kwako.Pamoja na salaam, zetu za
“Kwa pamoja tukishikamana tutashinda”