MALENGO YA CHAVITA
Kama wanajamii, viziwi wanayo haki ya kuchangamana na watu wengine na kushirikishwa kikamilifu katika shughuli za jamii. Hii ni haki ya msingi ya binadamu. CHAVITA itahakikisha hili kwa:
- Kuhamasisha matawi ya CHAVITA na jamii ya Viziwi popote walipo hapaTanzania, jamii ya watanzania, taasisi na serikali kuhusu haki za Viziwi.
- Kupigania usawa katika fursa za elimu, huduma za jamii na nyanja zote za maisha ya binadamu.
- Kupigania kutambulika kisheria kwa Lugha ya Alama yaTanzania.
- Kujenga mwamko na kukuza matumizi ya Lugha ya Alama kwa matawi ya CHAVITA, jamii ya Viziwi nchini, na kwa jamii ya watanzania kwa ujumla.
- Kuhakikisha shughuli za maendeleo ya jamii na ki-uchumi kwa matawi ya CHAVITA na jamii ya Viziwi nchini zinaboreshwa.
- Kuhakikisha matawi ya CHAVITA na jamii ya Viziwi nchini wanapata uwakilishi katika ngazi zote za uongozi.
- Kufanya na kuendeleza utafiti kuhusu masuala yanayowahusu Viziwi
- Kupambana na Virusi vya Ukimwi (VVU) na UKIMWI pamoja na majanga mengine yanayowakabili Viziwi.
Mabadiliko Mapya

CHAMA CHA VIZIWI TANZANIA CHAVITA-TAWI LA MKOA WA DODOMA imeongeza Habari.
chavita dom haikuwa nyuma katika shughuli zake katika kusaidia watoto wenye ulemavu viziwi kama pichani ni watoto viziwi wa shule ya msingi kigwe wakifurahia jambo.
15 Desemba, 2012

CHAMA CHA VIZIWI TANZANIA CHAVITA-TAWI LA MKOA WA DODOMA imeongeza Habari 2.
pichani washiriki wa mafunzo yaliyoendeshwa na chavita dodoma kwa ufadhili wa fcs. ni wanachuo na wazazi wa viziwi na viziwi wenyewe yalifanyika ukumbi wa cct dodoma mjin.
14 Julai, 2012

CHAMA CHA VIZIWI TANZANIA CHAVITA-TAWI LA MKOA WA DODOMA imeongeza Habari 2.
pichani ni kwaya ya wanafunzi viziwi wa shule ya viziwi kigwe wakiwa katika kanisa la viziwi kigwe wilayan bahi mkoa wa dodoma.
31 Mei, 2012
CHAMA CHA VIZIWI TANZANIA CHAVITA-TAWI LA MKOA WA DODOMA imeumba ukurasa wa Miradi.
Chavita inajiandaa kuweka ripoti ya miradi hivi karibu..
9 Februari, 2012
CHAMA CHA VIZIWI TANZANIA CHAVITA-TAWI LA MKOA WA DODOMA imeumba ukurasa wa Timu.
CHAVITA Makao makuu na CHAVITA wilaya ya Dodoma mjini
9 Februari, 2012
CHAMA CHA VIZIWI TANZANIA CHAVITA-TAWI LA MKOA WA DODOMA imeongeza FCS kwenye orodha yake ya Mashirika ya Ubia.
9 Februari, 2012
Sekta
Sehemu
DODOMA, Dodoma, Tanzania
Tazama mashirika ambayo yapo karibu
Tazama mashirika ambayo yapo karibu