Taarifa kwa Waumini
BARAZA KUU LA WAISLAM TANZANIA {BAKWATA} – OFISI YA SHEIKH {w}
KAMATI YA MIPANGO NA FEDHA {w}
OFISI YA SHEIKH WA WILAYA YA SERENGETI-TEL:-+255 756 229 093/+255 713 417 921
E-mail:- sheikhwaser@gmail.com Website: www.envaya.org/bakwataser
13/May/2013 = 3/Rajabu/1434
Utangulizi
KAMATI YA MIPANGO NA FEDHA {w} ni kamati iliyoundwa na Sheikh wa wilaya mnamo tarehe 06/07/2012 sawa na terehe 15/Shaaban/1433h, zamani ilikuwa ikijulikana kama kamati ya maendeleo ya waislam Serengeti ili kuharakisha maendeleo ya Waislam Wilayani Serengeti.
Fikra hizi zilipatikana baada ya kikao cha Kaimu Sheikh wa wilaya SHEIKH JUMA A. SIMBA alichokifanya mnamo tarehe 8/Muharam/1433h sawa na 2/12/2011 katika Msikiti wa FORT IKOMA kwa ajili ya maadhimisho ya mwaka mpya wa Kiislam. Miongoni mwa masuala yaliyojadiliwa siku hiyo ni pamoja na uimarishaji wa Uongozi, uimarishaji wa Uislam wilaya nzima na maendeleo ya Uislam Serengeti.
Kamati hii imeanza shughuli zake rasmi tarehe 21/04/2013 sawa na 10/Jamadu Than/1434 baada ya kupata Uongozi wake rasmi, M/kiti wa kamati hii ni Ismail Nyamarege, Katibu wa kamati ni Abdallah M. Mgonja na mweka Hazina ni Muzammilu Kharid. Kamati imefanikiwa kufungua Akaunti katika Bank ya NMB tawi la Mugumu
Jina la Akaunti :- MFUKO WA MAENDELEO YA WAISLAM WILAYA YA SERENGETI
Namba ya Akaunti :- 30210001780
Kamati inawaomba waumuini wote wenye NIA njema katika kuleta Maendeleo katika jamii ya Kiislam watoe michango yao kupitia akaunti hiyo, na ikumbukwe kuwa hiyo ni akiba isiyooza ambayo wataikuta mbele za Mungu baada ya umauti wao.
Miongoni mwa mambo ambayo kamati hii itakuwa ikiyafanya
- Kupanga mikakati ya maendaleo katika wilaya na kutoa ushauri wa namna ya kupata njia/vyanzo vya mapato.
- Kufatilia utekelezaji wa mikakati ya maendeleo kwa kushirikiana na Halmashauri ya BAKWATA {w}, kamati za misikiti, na kamati zinazotambulika.
- Kutoa fedha kwa shughuli za maendeleo pale inapohitajika kwa ajili ya maendeleo na pia kufuatilia matumizi ya fedha zilizotolewa na kamati hii.
- Kubuni vyanzo vya mapato vya kudumu.
- Kupokea michango ya fedha/ maoni/ ushauri/ mapendekezo toka kwa waumini/ jumuiya yoyote ya Kiislam na Asasi/Kampuni itakayoguswa jitihada hizi za Kamati.
Mtume MUHAMMAD {S.A.W} anasema:-
“UMOJA NI REHMA NA UTENGANO NI ADHABU”
Tushikamane kwa pamoja kuleta Maendeleo Tanzania.
Ibitekerezo (7)
mungu abariki katika hili nami nauga mkono kwa dhati
asalamu
Bw, Faida Hassan,,, nimefurahi sana kupata maoni yako, kwanza tumuombe mola sote tuwe na afya, hekima na busara ktk kuimarisha dini.
pili tushikamane kwa pamoja wala tusifarakane.
Tunaomba zaidi ushauri wenu kwa ajili ya ALLAH.
bwana De Credo wa Kampala
napenda kukuhakishia kuwa hatufanyi maskhara, tupo hapa kwa ajili ya kutafuta radhi za ALLAH na si vinginevyo.
f.hassan
Jazaq llahu kheir, Inshallah Allah abariki na kujaalia kila mipango tuliojiwekea iwe kwenye mafanikio. Pia na nyie wenzetu mliojitolea kulianzisha na kulisimamia jambo hili, Allah akujazeni kheir zake. Na sisi wengine ambao tupo nyuma yenu Allah atukunjulie nafsi zetu ili tuwe wamoja na wenye mshikamano katika kuipeperusha bendera ya Laa ilaha illa llah.
Na msichoke kutukumbusha kila wakati Inshallah.
Kwa ufupi tu kila kitu kimekaa vizuri humu na kinatia moyo, suala la kuboresha zaidi na hatimae kufikai kwenye malengo, hili ni jukumu lote sote sisi ka Waislam, Inshallah.