VOLUNTEERS OPPORTUNITIES
There are many ways you can contribute to us because of supporting the various needs we serve in our Serengeti community. Our institution is a non-profit organization that is available for the benefit of support, for that reason we do not have enough money for the success of a certain number of people at this time who can access financial capacity, so anyone who can use the hand can use our Bank Account which is MAENDELEO YA WAISLAM SERENGETI and our account number is 30210001780. NATIONAL MICROFINANCE BANK - MUGUMU SERENGETI
Volunteer now!
It doesn't matter how old you are, what you mean or who you are, but just remember that your support can make a big difference in the world.
SPONSOR
If you have a voice commanding others then we ask you to use the lessons and look at all the people and we hope you can do better in that. If you are committed to looking after money then realize that your role is very important in doing work that you can use and change the lives of our beneficiaries. With a new mindset, you will lead by evaluating your events and activities that affect life around the world.
WORK EXPERIENCE
We ask you to be our Great Volunteer Assistant!
You will be part of a brilliant team that makes development projects better, more powerful than ever. Please feel free to volunteer in our Office !.
This is a great opportunity for the less talented minds in everyday matters to affect the right society such as people with disabilities, widows, orphans, and people living with HIV with great dedication and passion to make a difference in the world. Here, use the hard work of spending money, doing a life-changing campaign, and your favorite comments with a team of enthusiastic people.
We ask for help from different volunteers who will be happy to work with us with different skills or expertise. We are happy to have anyone from any country in the world as we know people have different opinions so we are ready to order every day.
Contact us by email: -
jmagohe@gmail.com
May ALLAH bless you for accepting our request
FURSA ZA KUJITOLEA
Kuna njia nyingi ambazo unaweza kutuchangia kwa sababu ya kusaidia wahitaji mbalimbali tunaowahudumia katika jamii yetu ya Serengeti. Taasisi yetu ni taasisi isiyo ya faida bali ipo kwa ajili ya kusaidia, kwa sababu hiyo sisi hatuna fedha za kutosha kuendelea kuhudumia watu wenye mahitaji maalum na kwa wakati huu bado hatujapata uwezo wa kifedha, kwa hivyo mtu yeyote ambaye atahisi kutuunga mkono anaweza kujaribu kutumia Akaunti yetu ya Benki ambayo ni MAENDELEO YA WAISLAM SERENGETI na nambari ya akaunti yetu ni 30210001780. NATIONAL MICROFINANCE BANK – MUGUMU SERENGETI
Jitolee sasa!
Haijalishi una miaka mingapi, una uzoefu gani au wewe ni nani,bali wewe kumbuka tu kuwa msaada wako unaweza kuleta mabadiliko makubwa katika ulimwengu.
MFADHILI
Kama utakuwa na sauti ya kualika wengine basi tunaomba uitumie kikamilifu na tutawakaribisha wote na tunatumai kuwa unaweza kufanya vizuri zaidi kwenye hilo. Kama utajitolea kutafuta pesa basi tambua kuwa hilo jukumu lako ni muhimu sana katika kufanya miradi yetu iweze kuendelea na kubadilisha maisha ya walengwa wetu. Ukiwa na akili mpya, utaongoza kwa kuandaa hafla zako na shughuli ambazo zitaathiri maisha kote ulimwenguni.
UZOEFU WA KAZI
Tunaomba uwe msaidizi wetu Mkuu wa kujitolea!
Utakuwa sehemu ya kikosi chenye kipaji kinachofanya kazi za miradi ya maendeleo kuwa bora zaidi, yenye nguvu na kubwa kuliko wakati wowote. Tafadhali naomba uwe kujitolea Ofisini kwetu!.
Hii ni fursa nzuri kwa akili zenye talanta kushiriki katika mambo ya kila siku ya kuhudumia jamii zanye uhitaji kama watu wenye ulemavu, wajane, mayatima, na watu wanaoishi na virusi ya ukimwi kwa kujitolea sana na shauku ya kufanya mabadiliko makubwa ulimwenguni. Hapa, utasaidia kupanga shughuli kubwa za kukusanya fedha, kufanya kampeni za kubadilisha maisha, na kushiriki maoni yako ya kupendeza pamoja na timu ya watu yenye shauku.
Tunaomba msaada kutoka kwa wajitolea tofauti ambao watafurahi kufanya kazi na sisi kwa ustadi wowote au utaalam. Tunafurahi kuwa na mtu yeyote kutoka nchi yoyote ulimwenguni kwani tunajua watu wana maoni tofauti kwa hivyo tupo tayari ili kujifunza kila siku.
Wasiliana nasi kwa email:-
jmagohe@gmail.com
Mwenyezi Mungu akubariki kwa kukubali ombi letu.