TARIFA KWA WAISLAM WILAYANI GAIRO
BAKWATA wilaya ya gairo tunawatangazia waislam wote wilayani Gairo na maeneo ya jirani kuwa sherehe za Maulid ya Mtume (s.a.w) zita fanyika kiwilya Gairo mjini kwenye msikiti wa wilaya (Masjid Rahmaan) uliyopo Unguu Road. Akitoa taarifa hiyo Sheikh wa wilaya amesema, maadhimisho hayo yatafnyika siku ya ijumaa mwezi 29 mf 6 sawa na tarehe 31/01/2014. Maulid hayo yatatanguliwa na maulid ya kinamama baada ya swala ya ijumaa. Mgeni rasmi katika shuguli hiyo anatarajiwa kuwa Sheikh Mohamed Iddy Mohamed (Abuu Iddy). Waislam wa Gairo wana wakaribisha waislam wote wa maeneo ya jirani kuja kushirikiana kwa pamoja kusherehekea sikukuu hiyo ya kuzaliwa Mtume wetu Muhammad (s.a.w) alisema.
16 Januari, 2014