Envaya

KATIBU  wa BAKWATA Wilaya Gairo mwenye Sweta akiwa na Eng. Nasoro Kindamba wakiwa katika harakati za kupima jengo la Shule katika mradi wa ujenzi wa Shule Kimashale Wilayani hapo. Aidha Katibu wa Wilaya anatoa wito kwa Wadau na Waislam wote kushiriki katika kuchangia ujenzi wa Shule Hiyo ya umma wa Kiislam. Ujenzi wa Shule ni ghari sana unahitaji mabilioni ya hele hivyo inahitaji mshikamano haswa wa Kiimani ili kufanikisha hivyo tunatoa wito sote tushiriki ili kuujenga uislam wetu. Mnaweza changia vifaa vya ujenzi au fedha kupitia Akaunt zetu NMB 24010003220 au M-Pesa 5081600

KAWASASA TUPO KATIKA HATUA ZA MSINGI

 

UCHAGUZI MKUU BAKWATA , MRUMA ATEMA CHECHE

...
🔅 “Tukibaini mgombea anayefaa na anayetakiwa na waislamu amekatwa tunafuta uchaguzi”
🔅Asema: wagombea wajiandae kuwa “Watumishi” wa watu na siyo “Wafalme”
🔅Awataka viongozi kupitisha wagombea wanaofaa na siyo wagomea waliowaandaa kwa maslahi binafsi ili kujijengea kinga na kudumisha “Ufalme wao”
🔅Aonya kuchagua kwa misingi ya ukabila, majimbo na ujamaa
🔅 Asema BAKWATA ni moja anayefaa anaweza kuchaguliwa popote
🔅viongozi wa kuteuliwa“chekeche litafanya kazi”

Na : Harith Nkusa
Mwandishi maalumu wa Mufti

🔸HABARI KAMILI

Kufuatia kutolewa kwa waraka maalum unaelekeza kufanyika uchaguzi mkuu wa BAKWATA kuanzia mwezi ujao katibu mkuu wa BAKWATA Alhaj Nuhu Jabir Mrumaamefunguka na kusema bayana kwamba hataruhusu mchezo mchafu kwenye uchaguzi huo

Katibu mkuu amemwambia mwandishi maalum wa mufti kwamba wenye nafasi kwenye uchaguzi huu ni wagombea wanaoweza kwenda na kasi ya samaha mufti Zubeir mwenye dhamira na lengo la kujenga "BAKWATA mpya" na wakati wote watazingatia haja kubwa ya maendeleo iliyoko sasa.

Kwa mujibu wa waraka huo uliotolewa na katibu huyoTarehe 8/1/2020 na kuelekezwa kwa makatibu wa mikoa na wilaya zote nchini, uchaguzi kwenye ngazi ya misikti na kata utafanyika kuanzia tarehe 15/2/2020 mpaka 28/2/2020 wakati uchaguzi ngazi ya mikoa na wilaya utafanyika kati ya tarehe 15 mpaka 31/3/31/2020 na uchaguzi ngazi ya taifa utafanyika kati ya tarehe 14 na 30/4/2020. Kwa mujibu wa waraka huo chaguazi hizo za ngazi zote zitahusisha kuchaguliwa viongozi wa Jumuia za Vijana na wanawake.

Alha Mruma ameonya vikali kupitisha majina ya wagombea au kuwachagua kwa misingi ya ukabila, mkoa na ujamaa. Akasema viongozi wanaohusika kupitisha majina ya wagombea wachuje majina kwa kuzingatia sifa kwa mujibu wa katiba ikiwa ni pamoja na uchamungu, kujituma, kujitolea, ubunifu na uaminifu.

Amesema viongozi wasipitishe majina ya watu wao waliowandaa kwa maslahi yao binafsi ili waendelee kuwa mabwana wakubwa na wafalme wasioshaurika na wasiokosolewa kwenye maeneo yao

“Najua kuna viongozi tayari wana majina yao mifukoni. Lakini sisi tunasema Hata kama ni mpinzani wako maadamu ana sifa apitishwe kama mgombea. Acheni waislamu waamue. Acheni kusema huyu ni wangu na huyu si wa kwangu. Akiwa mdadisi na mwenye kuhoji anafaa. Lazima tukubali changamoto. Vinginevyo maendeleo yataendelea kuwa ndotoni”

Amesema na kuendelea “Uchaguzi uwe huru, kila mwenye sifa awe huru kugombea, jambo muhimu wagomea hao wajue majukumu na mipaka yao kikatiba. Tukibaini mahala palipo na aina yoyote ya upendeleo tunavunja uchaguzi na hatua kali zitafuata kwa kiongozi aliyehusika”

Akisisitiza onyo hilo alhaj Mruma alionyesha kukerwa na watu ambao bado wanafikiria na kuweka mbele maslahi yao binafsi

"Uchaguzi unalenga kuwapatia waislamu wa Tanzania viongozi sahihi. Viongozi watakaoleta maendeleo kwenye Uchumi, elimu, afya na huduma nyingine za kiibada na kijamii. Waislamu wanataka mengi ambayo yamekuwa yanakwama na watu wenye dhamira na uwezo wa kuwakwamua wapo. Kwa nini wasipewe nafasi? Ameuliza kwa masikitiko makubwa.

Amesema uhuru anaoutaja hatarajii utakuwa mlango wa kuwapenyeza mamluki na watu wasioitakia mema BAKWATA, waislamu na Tanzania kwa ujumla.

" Wagombea wawe na nia na dhamira ya kweli na ya wazi kutetea na kulinda BAKWATA, maslahi ya waislamu, amani na maendeleo endelevu ya taifa letu. Asichaguliwe mtu atakayetuvuruga. Umoja tunaoutaja usiwe mlango wa kuwaingiza watu wenye mawazo na fikra potofu" amesisitiza

Akasema viongozi watakaochaguliwa waweke mbali Ubwana na ufalme. Wawe watumishi wema wa waislamu na washaurike.

"Ile desturi ya kujipa nguvu ya maamuzi na mamlaka ya kusema na kufanya lolote haitusaidii. Kuna watu wanaifanya ndiyo njia ya kujiimarisha. Wanatisha watu. Ukiwa mtumishi mwema watu watakutii. Kwa nini uwatishe na kuwakandamiza? Jitathmini kwanza" ametoa rai.

Akawaomba waislamu watoe taarifa ya ukiukwaji wa haki (kwa dhamira njema) pasina kuongeza fitina na majungu.

"Nitapokea taarifa na kuzifanyia kazi. Majungu, fitina na chuki binafsi havitakuwa na nafasi. Lakini tutazifanyia kazi taarifa hizo kwa uadilifu mkubwa" amesema.

VIONGOZI WA KUTEULIWA

Kwa upande wa viongozi wa kuteuliwa katibu huyo mkuu amesema chekeche litafanya kazi. Amesema upembuzi yakinifu unaendelea na viongozi wasiofaa watawekwa pembeni

Alhaj mruma akasema bayana kwamba haridhishwi na utendaji wa baadhi ya makatibu wa mikoa na wilaya, akasema Mabadiliko yaliyofanywa hivi karibuni huko Katavi, Mwanza, Dodoma, Kaliua na Maswa yataendelea mikoa na wilaya zingine.

"Hatuwezi kuvumilia watu wanaotuchelewesha, wasiofanya kazi, wasioleta taarifa na ambao wanaficha taarifa za mapato na matumizi kwa makusudi"

Amesema na kuendea kufafanua "Kuna viongozi waliojimilikisha mikoa na hata wilaya. Hawafanyii kazi maelekezo ya ngazi za juu na maamuzi halali ya vikao. Ni wafalme na watawala wanaoendeleza ubinafsi. Hatutawavumilia"
........

Katibu mkuu wa BAKWATA ndiye mkurugenzi mkuu wa uchaguzi huo. Atakasimu madaraka kwa viongozi wa mikoa na wilaya ili wawe wasimamizi wa uchaguzi kwenye maeneo yao.

Waraka nambari moja ulioelekezwa kwa makatibu wa mikoa na wilaya utafuatiwa na waraka wa pili utakaoelekeza mengi ikiwa ni pamoja tarehe halisi na siku ya uchaguzi wa kila ngazi.

Nakala ya waraka nambari moja pia imefikishwa (kwa taarifa) kwa samaha Mufti, Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini, Mwenyekiti wa Halmashauri kuu, Masheikh wa mikoa na Wenyeviti wa mikoa
...........

Taswira inaweza kujumuisha: Mtu 1, matini yanayosema 'Nuhu Jabir Mruma Katibu Mkuu BAKWATA'

61

ISLAMIC FUNDATION WAKABIDHI MSIKITI BAKWATA

Mwenyekiti wa tasisi ya The Islamic Foundation amekabidhi msikiti wa vibandani Morogoro Mjini. Makabidhiano hayo yalifanyika baada ya kukamilika kwa ujenzi huo na kufanyika ufunguzi rasmi wa msikiti huo uliopewa jina la Masjid Madina. akiongea mara baada ya ufunguzi huo Mwenyekiti wa Islamic Fondation aliwahusia Waislam kutumia vizuri msikiti huo ili iwe sababu ya wao kuingia peponi badala ya kuanza kugombania uongozi mpaka kufikia kuvunja mipaka ya Allah S.W
Akionggea Sheikh wa Mkoa wa Morogoro ambae pia ni Sheikh wa Wilaya ya Gairo alisema. waislam tuache kubaguana kwa kuwa sisi sote tupo katika njia moja ya Laila ha Ilallah hivyo tunapaswa kuungana kwa pamoja na kufanya yetu kama Waislam Chuki za Kitaasisi magovi baina ya Mtu na Mtu hayana maana badala yake tutumie misikiti yetu kama vituo vya kuendesha mambo yetu ya kidini. Tuache majungu. Mwisho Sheikh alitoa Shukran kwa Islamic Foundation kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa msikiti wa Kisasa.

MAADHIMISHO YA MAULID YA MTUME S.A.W 1349/2017 MKOA WA MOROGORO

Baraza kuu la Waislam Tanzania BAKWATA Wilaya ya Gairo tunawakaribisha katika maadhimisho ya mazazi ya Mtume Muhamad S.A.W yatakayo fanyika kimkoa katika Wilaya ya Gairo Kata ya Chakwale. Akiongea na waumini wa msikiti mkuu wa wilaya Katibu Wa BAKWATA wilaya Gairo Sadi M.Msita alisema, Maulidi kimkoa yatafanyika tarehe 15/12/2017 katika kata ya chakwale. Aidha tunachukua fursa hii kuwakaribisha waislam wote kujumuika nasa katika kusherekea mazazi ya Mtume Muhamad S.A.W. kwani kuja kwake mtume ni Rahma kwa viumbe wote. Wakati Sheikh wa Wilaya ya Gairo ambae pia ni kaimu Sheikh wa Mkoa wa Morogoro ameelekea mkoani Lindi akiwa na jopo lake la Viongozi wa Mkoa kudhulia maadhimisho hayo yatakayo fanyika katika Wilaya ya RuangwaKaimu Sheikh wa Mkoa wa Morogoro (aliye vaa kanzu) na viongozi wengine wa Mkoa wa Morogoro wakiwa njiani kuelekea Ruangwa kwenye Maulid ya Kitaifa.

 

TAARIFA KWA WAISLAM WOTE

BAKWATA GAIRO, Tunapenda kwataarifu waislam wote ndani na nje ya nchi kuwa tumeanzisha ujenzi wa shule ya kiislam katika eneo la Chakwale, ujenzi unategemea nguvu za waislam mbalimbali, wafadhiri, kutoka ndani na nje ya nchi ili kufanikisha ujenzi huo. wewe kama Muislam unajua mtu au kampuni au taasisi yoyote yenye kuweza kutusaidia kufanikisha ujenzi huu tafadhali tupe taarifa tuwasiliane nao kwa maendeleo ya Uislam (wasiliana nasi kupitia +255713694952)Pichani ni baadhi ya Waislam waliokuja kujitolea nguvu zao kwa kusafisha eneo la ujenzi wa Shule ya Kiislam na Kituo cha kuhifadhisha Quraan. (Aliesimama ni Katibu wa Bakwata Gairo. Ust. Sadi Msita)

Sheikh wa Wilaya Gairo akiwa na Mh Muft wa Tanzania alipo tembelea Wilayani Gairo nakuwaombea duwa wakazi wa Gairo Mh. Muft aliwaasa viongozi wa wilaya Gairo kuendana na kasi ya maendeleo iliyopo sasa na kuwaeleza kuwa wajitahidi kutafuta maeneo popote na kufanya uwekezaji hasa katika maeneo ya elimu na uchumi kwa ujimla wake

BARAZA KUU LA WAISLAM TANZANIA Wilaya ya Gairo linawata kheri na baraka katika kusherehekea Idd l'fitri. Ibada ya ya Suna ya Idd kiwilaya itafanyika katika msikiti mkuu wa wilaya Masjid Rahmaan uliopo Gairo Unguu road kuanzia saa 1.30 asubuhi. Akizungumza na waumini wa masjid Rahmaan jana mwezi 29 ramadhan Sheikh wa Wilaya alisema BARAZA la idd litafanyika siku ya jumanne katika kijiji cha Ng'olongo kiliopo kata ya Idibo kuanzia saa saba baada ya swala ya adhuhuri na kuwaasa kuwa waislam wote kuungana kwa pamoja katika Baraza la idd  hata hivyo amsema usafiri wa kuelekea huko utapatikana masjid Rahmaan kuanzia saa 5 asubuhi. (BAKWATA Wilaya)

Mwenyekiti wa Halmashauri Wilaya BAKWATA Gairo amefariki leo majira ya saa 4 asubuhi. Kwa taarifa ya kifo chake mwenyekiti huyo bwana Sheikh Ramadhan Makame amepatwa na umauti baada ya kusumbuliwa muda mrefu na tatizo la upungufu wa damu, mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho saa 7 baada ya swala ya Adhuhuri. INNA LILLAH WA INNA ILAIH RAAJIUN
VIGODORO/ RUSHAROHO Nimarufuku kwenye sherehe za kiislam GAIRO. Hayo yalisemwa na sheikh wa kata ya Gairo Sheikh Nassoro Bakari baada ya kumalizika kikao cha baraza la masheikh kata ya Gairo. Akitoa taarifa hiyo makamu wa Imam wa msikiti wa Wilaya ust. Yusuf alisema, Hairuhusiwi kwa Mislam kuhusisha sherehe za kidini na miziki. Hata hivyo amesama atakaekiuka masheikh hawata fika kwenye shughuli yake na atatengwa katika maswala ya kidini ikiwa ni pamoja na kutofika kwenye msiba unaoihusu familia yake. Msumeno huo utamkumba pia Sheikh atakae shiriki kwenye mkumbo huo, ni msimamo mkali ambao sheikh wa Wilaya pia ameunga mkono na kupendwa na waislam wanaozingatia dini.

TARIFA KWA WAISLAM WILAYANI GAIRO

BAKWATA wilaya ya gairo tunawatangazia waislam wote wilayani Gairo na maeneo ya jirani kuwa sherehe za Maulid ya Mtume (s.a.w) zita fanyika kiwilya Gairo mjini kwenye msikiti wa wilaya (Masjid Rahmaan) uliyopo Unguu Road. Akitoa taarifa hiyo Sheikh wa wilaya amesema, maadhimisho hayo yatafnyika siku ya ijumaa mwezi 29 mf 6 sawa na tarehe 31/01/2014. Maulid  hayo yatatanguliwa na maulid ya kinamama baada ya swala ya ijumaa. Mgeni rasmi katika shuguli hiyo anatarajiwa kuwa Sheikh Mohamed Iddy Mohamed (Abuu Iddy). Waislam wa Gairo  wana wakaribisha waislam wote wa maeneo ya jirani kuja kushirikiana kwa pamoja kusherehekea sikukuu hiyo ya kuzaliwa Mtume wetu Muhammad (s.a.w) alisema.