Envaya

ANGALIZO KWA VYOMBO VYA HABARI

Waandishi wote hususani nchini Tanzania wenye tabia ya kutoa habari bila utafiti wowote au wa kina, mnatahadharishwa kutoendelea kutumia wanasiasa watumiao siasa vibaya katika kuharibu taaluma zenu na umaana wa uwepo wenu kwa jamii kwa kutoa habari pasipo kufanya utafiti au utafiti wa kina. ''NO RESEARCH NO RIGHT TO TALK''

TAHADHARI KWA WANANCHI WOTE

Shirika la APAPO linawatahadharisha wananchi wote hususani  mkoani Rukwa nchini Tanzania kuwa makini na watu wanaotumia vivuli vya Serikali kupoteza uhuru, wajibu na haki zao kikatiba na kuwa na hofu ya kutotumia fursa wanazopewa na serikali zao zenye lengo la kuwaboreshea maisha yao na taifa lao kwa ujumla.

APAPO tunaomba wawakilishi na watendaji wa serikali hususani wa ngazi za wilaya wasiotii sheria, wasiokuwa waadilifu na waaminifu kwa serikali kuu na raia wake, wanaposhindwa kutoa ushirikiano kwa shirika baada ya  kushirikishwa kama lilivyo lengo la Shirika, wasitumie fursa hiyo kuliharibia Shirika lengo na ahadi yake kwa serikali na raia wake. Sisi hatujaribu, Tunafanya.

Mkoani Kigoma maombi ya nafasi za kazi yamesitishwa mpaka hapo yatakapotangazwa tena iwapo italazimu.