Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Igiswayire. Edit translations
Vitongoji Environmental Conservation Association ni jumuia isio ya kiserikali inayojihusisha na uhifadhi wa mazingira. Ilianzishwa mwaka 1996 kufuatia tokeo ambalo lilisababisha watu 35 kupoteza maisha yao kwa ajili ya kula nyama ya kasa aliyesadikiwa kuwa na sumu Tokeo hilo baya ndio chanzo kikubwa cha kuanzishwa kwa Jumuia hii.
Jumuiya hii imepata usajili wake mwaka 1997 na ina hati ya usajili no.33 chini ya sheria no.6 ya Zanzibar ya mwaka.Miongoni mwa mafanikio yake ni pamoja na :
- Uhifadhi wa mazingira ya ukanda wa pwani mashariki ya Kisiwa cha Pemba
- uhifadhi wa mikoko na mazalio ya viumbe vya baharini.
- kuweza kuwapatia taaluma ya uhifaadhi wa mazingira wananchi katika jimbo la wawi na Wilaya ya Chake kwa ujumla u oteshaji wa vitalu vya miti na upandaji wa miti
- kutambulika na jamii,serikali kuu na baadhi ya mashirika
- imeweza kufanya kazi na mitandao ya mazingira (mfano ) MTAMAZA
- tumeweza kufanya kazi katika jimbo na wilaya wakati mwanzoni ilikuwa ni viitongoji tu
- tumeweza kupata watendaji katika asasi na mafunzo mbali mbali ya uandaani wa miradi na usimamizi wa fedha.