Log in
VITONGOJI ENVIRONMENTAL CONSERVATION ASSOCIATION

VITONGOJI ENVIRONMENTAL CONSERVATION ASSOCIATION

chake-chake, Tanzania

Parts of this page are in Swahili. Edit translations

Asasi hivi sasa inatekeleza mradi wa ushawishi na utetezi wa haki za wanawake na umiliki wa ardhi. Hii imetokana na tafiti nyepesi iliyofanywa na shirika letu pamoja na jamii ilituzunguka na kubaini kwamba wanawake wanafanyiwa udhalilishwaji mkubwa kutokana na mila na desturi potofu zilizojengeka katika jamii. Wanaume wanamiliki haki zote katika jamii pale jamii hizo zinafiliwa na wazazi wao, ama wanapoondoka kwa kwa kuolewa na kwenda kuishi eneo la mume. Rasilimali ardhi na nyenginezo nyingi zinakuwa chini ya mamlaka ya wanaume.

Kwa msingi huo jamii ya Vitongoji kwa kushirikia na VECA zilibuni mradi huu ili kuwasaidia wanawake na wanaume kupata elimu ya umiliki wa ardhi kisheria kwa mujibu wa haki inavyostahiki katika jamii.

Mradi huu umewezeshwa na Shirika Foundation for Civil Society la DSM ambao utatekelezwa kwa muda wa miaka mitatu, na hivi sasa tumeshatekeleza mwaka mmoja kwa shughuli mbalimbali mikutano ya hadhara, maigizo, semina kwa ngazi mbali mbali katika jamii na taasisi za Serikali na viongozi wa kidini, midahalo na shughuli nyengine.