HIFADHI YA MAZINGIRA
Tumepanda miti katika msitu wa umuishanga na kutoa elimu juu ya kuhifadhi msitu kwa jamii ya watu wasiopungua 150000,mradi ulianza mwezi Agosti mwaka2011.
ELIMU YA UKIMWI:
Tumeelimisha wanafunzi wote wa shule za sekondari zilizopo katika kata ya KANYIGO juu ya elimu ya UKIMWI namna ya kujilinda na maambukizi ya mapya,mradi huu umesaidia sana kupunguza maambukizi mapya ya VVU
KILIMO CHA UMWAGILIAJI
Tumeanzisha mashamba darasa kwa vikudi vya vijana wanaojishughulisha na kilimo cha mbogamboga, vijana wengi wameshiriki katika shughuli hii na imesaidia kubadili uchumi wa vijana katika maeneo ya mradi.
MAANDALIZI YA VITALU VYA MITI
Asasi kwa sasa inajiandaa kuotesha miti 50000 aina ya misonobali(emiyojwe) tayari kwa ajili ya kuigawa kwa wanakijiji ili kusaidia kurudisha uoto katika maeneo ambayo miti imekatwa kwa wingi,pia miti hii itasaidia kuongeza kipato kwa jamii ya wana kanyigo