Envaya
Parts of this page are in Swahili. Edit translations
TAARIFA YA MTANDAO WA VIJANA MANISPAA YA TEMEKE KWA KIPINDI CHA UTEKELEZAJI CHA MEI JUNI 2009.

KUTOKA: MTANDAO WA MAENDELEO YA VIJANA MANISPAA YA TEMEKE (TEYODEN)
KWENDA KWA: MKURUGENZI WA HALMASHAURI MANISPAA YA TEMEKE

1.0 UTANGULIZI
Temeke Youth Development Network (TEYODEN) ni Mtandao wa Maendeleo ya Vijana unaoendeshwa na vijana wenyewe miongoni mwa mitandao 19 iliyotokana na programu ya vijana nje ya shule iliyotekelezwa na Halmashauri 19 nchini Tanzania kwa ufadhili wa UNICEF. Mtandao umesajiriwa chini ya ofisi ya Makamu wa Raisi, namba ya usajiri ni OONGO/0170.TEYODEN inasimamia na kuratibu shughuli zake katika vituo 24 vya vijana vilivyopo katika kata 24 za Manispaa ya Temeke.

1.1 Dira ya TEYODEN
Kuwa Mtandao bora wa Maendeleo ya vijana Tanzania unaowezesha vijana kuwajibika vya kutosha katika kubadili tabia hatarishi na kujiletea
katika vituo vya vijana vya kata na asasi wanachama wa TEYODEN.

1.3 Lengo kuu la TEYODEN
Kuchangia juhudi za kuleta maendeleo endelevu na thabiti ya tabia na mienendo ya vijana katika mahusiano yao hususani katika masuala ya ngono ili kupunguza kasi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi na kutekeleza mkakati wa kupunguza umasikini ili kufikia malengoya milenia (MDG`s)

2.0 SHUGHULI ZILIZOFANYIKA
• Katika miezi 3-(Julay -sept)ya utekelezaji, shughuli zifuatazo zilitekelezwa:

2.1 Ufuatiliaji wa shughuli za vijana baada ya mafunzo ya kujenga uwezo
Baada ya mchakato wa mafunzo ya kujenga uwezo vijana wawakilishi walirudi katika kata zao na kufanya utekelezaji katika kata zao.
Katika ziara ya ufuatiliaji wa matokeo makuu ya mradi (project impact) mambo yafuatayo yalijitokeza
Vijana wanaendeleza matunda ya mradi kwa kuendeleza dhana ya kujitegemea mfano kata ya Vituka, Charambe, Azimio na miburani wapo katika michakato ya kufungua akaunti japo kuwa benki zinamasharti magumu kwa vikundi vidogo vya kijamii.

2.2 Uibuaji wa mradi wa kuamsha ari ya uwajibikaji na ushiriki wa vijana katika masuala ya kijamii na kimaendeleo.
Katika kipindi cha utekelezaji wa taarifa idara ya tafiti na takwimu iliendesha vikao 4 vya vijana vya kuibua mradi wa kiwango cha kati na kuuwasilisha The Foundation for civil society kwaajili ya maamuzi ya kupatiwa fedha.mradi huu unajulikana kama kuongeza ari ya uwajibikaji kwa vijana katika shughuli za kijamii na maendeleo manispaa ya Temeke.

2.3 Mjadala wa vijana centre 1
Kama ilivyo kawaida kwa vijana wa TEYODEN kufanya midahalo kila jumamosi mbili katika mwezi.katika kipindi cha taarifa vijana walifanya midahalo 6 na wastani wa vijana 120 walishiriki katika midahalo hiyo.

2.4 Mafunzo ya kujenga uwezo wa watendaji wa TEYODEN.

Katika kipindi cha taarifa viongozi na wanachama wa TEYODEN walipata nafasi ya kuhudhuria mafunzo ndani na nje ya mkoa wa Daresalaam kama ifutavyo:-

Ushiriki wa vijana 30 katika mafunzo ya ujasiriamali ukumbi wa vijana centre ilala
Lengo la mafunzo -
Lengo la mafunzo haya ni kuinua uelewa wa vijana katika stadi za ujasiriamali ili kukuza biashara zao na kujiepusha na makundi rika na kuondoa uamsikini miongoni mwao.

Ushiriki wa vijana 30 katika mafunzo ya ujasiriamali yaliyoandaliwa na Safer Cities kupitia Sustainability Cities.yalioyofanyika katika ukumbi wa karimjee.
Lengo la mafunzo -
Lengo la mafunzo haya ni kuinua uelewa wa vijana katika stadi za ujasiriamali ili kukuza biashara zao na kujiepusha na makundi rika na kuondoa uamsikini miongoni mwao.

Ushiriki wa mweka hazina wa TEYODEN katika mafunzo ya uhasibu MTCDC chini ya ufadhili wa The Foundation for Civil Society.
Lengo la mafunzo:-
Lengo la mafunzo haya ni kuwezesha washiriki kuwa na uwezo wa washriki kuendesha shughuli za mahesabu katika Asasi zao kwa uwazi na uwajibikaji.

Ushriki wa mwakilishi mmoja kutoka TEYODEN katika mafunzo ya ushiriki na ushirikishwaji wa vijana katika shughuli za kijamii mafunzo yaliyofanyikia morogoro.
Lengo la mafunzo:-
Lengo la mafunzo haya ni kuwezesha washiriki kujua haki na wajibu wa jamii kushiriki katika shughuli za kijamii na kuwa wawezeshaji kwa vijana wengine

Ushiriki wa mwakilishi mmoja wa TEYODEN katika mafunzo ya mbinu za kutunisha mfuko wa asasi yaliyofanyika mbezi garden jijini Daresalaam kwa ufadhili wa The Foundation For Civil Society.

2.5 Ushiriki wa mwakilishi mmoja wa TEYODEN katika safari ya upandaji mlima iliyoandaliwa na Kilimanjaro initiative kupitia Safer Cities.

2.6 Uandishi na uwakilishi wa Andiko la miradi kwa wafadhili
TEYODEN katika kipindi cha utekelezaji wa taarifa hii imeibua kutayarisha na kuwasilisha maombi yafutayo ya fedha:-

-Mradi wa uchimbaji wa kisima cha umwagiliaji katika kambi ya vijana ya Somangira. Mradi huu umewasilisha katika ubalozi wa ujerumani.

- Mradi wa kudarizi na ushonaji kwa vijana wa kike walio nje ya shule 80 kutoka kata 5 za Azimio, Makangarawe, Sandali, Vituka na Tandika.Mradi huu umewasilishwa katika ofisi za ubalozi wa Ujerumani.

3.0 KAZI ZILIZOPANGWA KUFANYIKA
3.1 TEYODEN imepanga kufanya mambo yafuatayo:-

-Kufanya uhamasishaji kwa vijana kuhusu uibuaji wa vijana na watoto wanaofanyiwa ukatili.

-Uhamasishaji kwa vijana katika ushiriki wa nane nane ngazi ya wilaya na ngazi kanda.

-Uhamasishaji wa vijana katika ushiriki wa mkutano wa kambi ya dunia utakaofanyika kuanzia tarehe 21/7/2009 hadi 27/8/2009 katika ukumbi wa sabasaba karume hall.

-Ushiriki wa vijana katika shughuli za uvuvi katika pwani ya bahari ya hindi maeneo ya vijibweni.

4.0 :HITIMISHO
TEYODEN inaamini kuwa mabadiliko kwa vijana yatakayochangia maendeleo ya vijana yanawezekana kama vijana wanapewa uzito unaostahili katika kupanga, kutekeleza, kufuatilia na kutathmini shughuli zinazowahusu. Viongozi wa TEYODEN na vijana siku hadi siku wamekuwa wakiongezewa uwezo katika kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ipasavyo.Hivyo tunawashauri wadau kutumia fursa hii adimu kwa kuwatumia ili kutatua matatizo ya vijana yanayowakabili .
June 8, 2010
« Previous Next »

Add a comment

Your name:
Your location:
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.