Injira
Temeke Youth Development Network

Temeke Youth Development Network

Temeke/Chang'ombe, Tanzania

Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Igiswayire. Edit translations
TAARIFA YA MTANDAO WA VIJANA MANISPAA YA TEMEKE KWA KIPINDI CHA UTEKELEZAJI CHA JAN-APRILI 2010
KUTOKA: MTANDAO WA MAENDELEO YA VIJANA MANISPAA YA TEMEKE (TEYODEN)
KWENDA KWA: MKURUGENZI WA HALMASHAURI MANISPAA YA TEMEKE
1.0 UTANGULIZI
TEYODEN katika kipindi cha utekelezaji cha taarifa hii imefanikiwa kutekeleza shughuli mablimbali.Taarifa hii inalengo la kueleza shughuli zilizofanyika,mafanikio changamoto na mapendekeozo ya vijana katika kipindi cha uutekelezaji wa taaifa hii.
2.0 SHUGHULI ZILIZOFANYIKA
1.1 Mjadala wa vijana centre 1.
Kama ilivyo kawaida kwa vijana wa TEYODEN kufanya midahalo kila jumamosi mbili katika mwezi.Katika kipindi cha taarifa vijana walifanya midahalo 8 na wastani wa vijana 247 walishiriki katika midahalo hiyo.
MADA IDADI YAVIJANA MASUALA YALIYOIBULIWA MAPENDEKEZO YA VIJANA
Kilimo kwanza 42 > Uelewa mdogo wa vijana kuhusu dhana nzima ya kilimo ya kwanza.
> Suala la upatikanaji wa rasilimali ardhi lilionekana kuwa ni changamoto miongoni mwa vijana.
> Upatikanaji wa mitaji kwa ajili uanzilishi wa kilimo /ununuzi wa pembejeo. > Kuinua uelewa juu ya Kilimo Kwanza ili kuwawezesha vijana kushiriki kwa kiwango kikubwa na kuondoa umasikini .
> Kutia mkazo wa utekelezaji wa Kilimo Kwanza kwa vijana.
> Kuwawezesha vijana katika upatikanaji wa rasilimali ardhi ili waweze kushiriki katika nyanja ya Kilimo kwa ujumla.
Uanzishaji na Uendeleaji wa SACCOS 49 > Kiwango cha fedha cha kuanzisha SACCOSS kimeonekana kuwa ni kikubwa na hivyo kuwakwamisha vijana wengi kushindwa kuanzisha kuendesha SACCOS hizo. >Vijana wajitolee kwa hali na mali ili kuanzisha SACCOS itasaidia sana kwa kuwafanya kupata mitaji katika shughuli za ujasiriamali.
> Uhamasishaji na elimu zaidi ya ujasiriamali kwa vijana inahitajika ili kuwavuta vijana wasio na taarifa na elimu ya ujasiriamali.
Usawa wa kijinsia 38 > Uelewa mdogo kwa vijana juu ya usawa wa kijinsia ilionekna kuwa ni changamoto kwa vijana walio wengi. > Ili kuendana na kutekeleza yaliyokubaliwa ktika mkutano wa Beijing, elimu zaid inahitajika kwa vijana katika suala la Usawa wa Jinsia.
VVU/UKIMWI katika maendeleo ya vijana. 50 > Katika sual hili, vijana waliibua changmoto ya upanukaji na kutandaa kwa elimu sahihi ya VVU/UKIMWI hivyo kuonekana kuwa bado ni changamoto kwa vijana > Elimu, uhamasishaji na usimmizi wa uwajibikaji unahitajika zaidi ili kuleta msisitizo kwa vijana.
> Vijna wajitolee na kuunda vikundi vya uhasishaji na utoaji elimu ili kuleta msukumo wa kuondokana na tatizo na kubakiza nguvukazi ya taifa.
vijana na Uchaguzi 31 > Vijana walio wengi wameonekana kuwa nyuma katika suala zima la uchaguzi kwa uchaguzi na kuona kuwa suala hilo ni la wazee na si vijna. > Elimu na uhasishaji pamoja na fursa za vijana katika uchaguzi inahitajika zaidi ili kuleta mvuto kwa vijana na kuibua ushiriki mzuri wa vijana.
ushiriki na ushirikishawaji wa vijana kijamii na kimaendeleo 37 > Katika kujadili mada hii, suala la imani limeonekana kuwa ni changamoto kwa vijana kwa kuwa vijana wengi wameonekana hawaaminiki katika kuleta mabdiliko ya kimaendeleo katika jamii. > Vijana wapewe fursa ya kushirikishwa katika mambo ya kimaendeleo ili waoneshe imani na uwezo wao.

Katika kipindi cha utekelezajitaarifa hii viongozi wanachama na walengwa wa TEYODEN walipata nafasi ya kushiriki shughuli mbalimbali kaaifutavyo:-
1.) Mafunzo ya Stadi za amaisha kwa Vijana 72 kwa kta 24 za manispaa ya Temeke na vijana 3 kutoka kila kata kwa muda wa siku 14.
2.) Mafunzo ya sera ya vijana yaliyofanyika katika kituo cha vijana cha Makangarawe yaliyoshirikisha vijna 40, aidha mafunzo hayo yalikuwa ya siku 3.
3.) Mafunzo ya kujenga uwezo kupitia taasisi ya vijana ya Sokoine katika kata ya Somangila, mafunzo hayo yalishirikisha vijana 22 kwa siku 5.
4.) Ziara ya vituo vya vijna vya kata ili kukagua uhai wa vituo.

5.) Kupokeas ugeni kutoka wizarani.

Aidha katika shughuli zote, vijana / walengwa walipata fursa ya kuwezeshwa na kushiriki katika mambo mbalimbali ya vijana.
`
4.0 HITIMISHO
TEYODEN inaamini kuwa mabadiliko kwa vijana yatakayochangia maendeleo ya vijana yanawezekana kama vijana wanapewa uzito na fursa zinaostahili katika kupanga, kutekeleza, kufuatilia na kutathmini shughuli za maendeleo. Viongozi wa TEYODEN na vijana siku hadi siku wamekuwa wakiongezewa uwezo katika kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ipasavyo. Hivyo tunawashauri wadau kutumia fursa hii adimu kwa kuwatumia ili kutatua matatizo ya vijana.vijana tukijiwezesha na kuwezeshwa tunaweza.
8 Kamena, 2010
« Inyuma Ahakurikira »

Tanga igitekerezo

Izina ryawe:
Aho uherereye
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.