Envaya
Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Icyongereza. Edit translations
2.0 SHUGHULI ZILIZOFANYIKA
• Katika miezi 3-(Julay -sept)ya utekelezaji, shughuli zifuatazo zilitekelezwa:

2.1 Utafiti kwa vijana juu ya uwajibikaji na ushiriki wa vijana katika shughuli za jamii na maendeleo.
TEYODEN imefanya utafiti shirikishi kuhusu uwajibikaji na ushiriki wa vijana katika vikao vya maendeleo na shughuli za kijamii na maendeleo.Utafiti huu umetokana maoni ya The Foundation For Civil kuwa ni vyema kufanya tafiti ili kujua hali ya uwajibikaji na ushiriki wa vijana kabla ya kuwasilisha tena mradi.Matokeo ya utafiti uliofanywa kwa Mukhtasari ni kama ifuatavyo:-
• 61.7% ya walengwa wa utafiti walionyesha uelewa kuhusu maana ya uwajibikaji na 38.3 % walionyesha kutoelewa maana ya uwajibikaji na dhana nzima ya uwajibikaji kwa vijana.
• 50% ya walengwa walionyesha kuwa kuna uwajibikaji hafifu kwa vijana katika mitaa na kata wanakoishi na 47% ya vijana wahojiwa walisema kuwa kuna uwajibikaji wa wastani miongoni mwa vijana katika mitaa wanayoishi.
• 85.3% ya vijana walisema hawashiriki katika vikao na shughuli za maendeleo ngazi ya kata na 14.7% tu ya vijana wanashiriki katika vikao na shughuli za kijamii na kimaendeleo ngazi ya kata.
• 73.5% vijana waliohojiwa walisema hawashiriki vikao na shughuli za kimaendeleo ngazi ya mtaa na 26.5% walisema wanashiriki katika vikao na shughuli za kimaendeleo na jamii ngazi ya mitaa.
• 67.6% ya vijana walisema hawashiriki katika shughuli za kujitolea na 32.4% za vijana walisema wanashiriki katika shughuli za kujitolea ngazi ya manispaa na kata.
• 76.5% ya vijana walisema wanashiriki katika vikao vya vijana katika vituo vya kata na 23.5% wanashiriki ipasavyo katika vikao vya vituo vya vijana vya kata.
• 76.5% ya vijana walihojiwa walisema vijana wanapaswa na ni muhimu sana kushiriki na kushirikishwa katika kufanya maamuzi ya kujamii na kimaendeleo,20.6% ni muhimu na 2.9% si muhimu sana kwa kuwa haina matokeo yoyote.
Maazimio ya vijana kutokana na utafiti huu ni kuanzisha kwa mradi au mpango maalum utakaowezesha vijana kujua umuhimu wa uwajibikaji na ushiriki wao katika shughuli za kijamii na maendeleo.Andiko la mradi limeandikwa upya na kuwasilishwa katika ofisi za Foundation.

2.2 Mradi wa uenezaji wa sera ya vijana wa Kituo cha vijana cha makangarawe.
Kituo cha vijana cha kata ya makangarawe kimeibua mradi wa kueneza sera ya vijana kwa vijana katika kata hiyo.Mradi huu umepata bahati ya kufadhiliwa na taasisi ya The Foundation For Civil Society.Mradi huu unategemewa kutekelezwa katika kipindi cha miezi 3 kuanzia mwishoni mwa Oktoba na kumalizika mwishoni mwa Disemba.

2.3 Mjadala wa vijana centre 1.
Kama ilivyo kawaida kwa vijana wa TEYODEN kufanya midahalo kila jumamosi mbili katika mwezi.katika kipindi cha taarifa vijana walifanya midahalo 6 na wastani wa vijana 107 walishiriki katika midahalo hiyo.
8 Kamena, 2010
« Inyuma Ahakurikira »

Ibitekerezo (1)

Ayoub K Bombwe (Temeke) bavuzeko
safi sana vijana wa Temeke kwa jinsi mnavyoonesha mupo active keep it up! change will come soon we need to see Temeke be like a Geneva
16 Mutarama, 2013

Tanga igitekerezo

Izina ryawe:
Aho uherereye
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.