MAFUNZO YA UJASIRIAMALI YANAYOENDESHWA NA MTANDAO WA VIJANA (TEYODEN) YAENDELEA KATIKA WIKI YA TATU.
Sasa imeshafikia wiki ya tatu toka mafunzo ya anzisha na kuza wazo lako la biashara yanayoendeshwa na TEYODEN hapa,Temeke kwa kushirikiana na mwezeshaji kutoka I.L.O yanayosimamiwa na asasi ya Restless Tanzania.
Mafunzo haya yanachukua wastani wa wiki moja kwa kila kundi la vijana 30.Mpaka sasa tumefikia vijana 60 kutoka katika kata 3 ambazo ni Chang’ombe,Keko na kata ya Kijichi.Shabaha yetu hasa ni kufikia vijana 300 kutoka katika kata zote 30 za manispaa ya Temeke,wafikirie vyema mawazo yao ya biashara,wayakuze na yawezeshe ajira kwao na kwa vijana wengine.
Tathmini ndogo tuliyofanya kwa walengwa waliopatiwa mafunzo haya,wanasema kuwa, hakujawahi kufanyika kwa mafunzo mazuri ya ujasiriamali kama haya ya wakati huu.Hivyo wanawashauri vijana wengine wa Manispaa ya Temeke kujitokeza na kutumia fulsa hii.
Utaratibu wa kuomba nafasi hii ya kuwa mmoja wa vijana 300 watakaowezeshwa kupata nafasi ya kuelimishwa ni pamoja na kuchukua fomu,kuijaza na kuirudisha katika ofisi za TEYODEN zilizopo Mtaa wa Bora,karibu na TRA,Katika jengo la Afisa Mtendaji wa kata ya Chang’ombe tunawakaribisha sana vijana wote.
Note that: Maendeleo ya mtu huletwa na mtu mwenyewe na si vinginevyo.