Kulia ni Mtunza hazina wa TACOMO Ezekiel Kamanga akiwa na Mkurugenzi wa TACOMO wakitafakari jambo.
Je uvunaji huu wa kisasa unaoendelea katika shamba la shirika la kilimo Uyole Jijini Mbeya, wakulima wadogohasa vijijini watafikia hapo?
Wakina Mama wajasiliamali katika Kata ya Mshangano Manispaa ya Songea wakiuza mazao ya mbogamboga chini katika Soko la Mshangano ambapo wamekuwa wakitozwa ushuru wa kati ya Shilingi 200 na 500 kwa siku kutokana na biashara hiyo,licha ya kuwa ni hatari kwa afya za watumiaji,imekuwa ikishangaza kuona Manispaa inachukua ushuru bila kujali kutengeneza miundombinu stahiki katika soko hilo jambo ambalo linatafsirika kama ni kuwadhulumu wakina mama hao miaka 50 ya uhuru.
Daraja la udongo hilo je ni salama ama ni kushindwa kuwajibika kwa viongozi tunaowachagua?!!!
Watoto kama hawa wanastahili kuendelezwa vipaji vyao kama wanavyoonekana, hawana viatu lakini duh! mambo safi
TUKOMESHE ajira kwa watoto. Hawa ni watoto wa kike wakazi wa eneo la Iziwa Jijini Mbeya wakiwa wamebeba kuni kwa ajili ya kuuza ili kujipatia kipato.
Wanafunzi wa shule ya Msingi Yala wilayani Mbarali mkoani Mbeya wanaosoma darasa la sita na la saba wapata0 93 wakiwa katika darasa moja!!!
Wananchi wa kijiji cha Yala wilayani Mbarali mkoani Mbeya wanaosubiri kuhamishwa na Serikali kupisha hifadhi ya wanyama