TANZANIA COMMUNITY MEDIA ORGANIZATION (TACOMO) ni Shirika lisilokuwa la kiserikali, lililoanzishwa na wanataaluma mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari, wauguzi, Maafisa ugani na walimu mwaka 2010, Kwa ajili ya kufanya kazi mahali pote Tazania Bara.
Shirika hilli linasaidia jitihada za serikali katika kuwezesha jamii hasa Vijana, wazee, Kilimo, Afya, kuandaa Mafunzo/warsha, uwezeshaji, kushiriki na kushirikishwa katika shughuli za maendeleo ya nchi na kuibua mijadala ya hoja.
Madhumuni makubwa ni kuiunganisha jamii ili kujaliana na kutokomeza umasikini katika nyanja za Kilimo, Afya na kuibua hoja mbalimbali na kuifikishia Serikali kupitia vyombo mbalimbali vya habari hususani Magazeti, Redio, Televisheni, Mitandao (Blog), vipeperushi nk.
.KAZI ZA SHIRIKA;
. Kuandaa Warsha na semina za mafunzo kwa waandishi wa habari juu ya jinsi ya kuandaa habari za uchunguzi na kuwapa ruzuku ili waweze kufika Vijijini na kuibua mambo mbalimbali ya maendeleo yanayohusu matakwa ya jamii Vijijini na mijini na hatimaye kuwezesha sauti za wasiosikika kusikika.
. Kuwajengea uwezo waandishi wa habari wanaochipukia ili waweze kuandika habari za uchunguzi kwa kufuata vigezo vya kutambua habari (News Significance), kutambua na kutendea haki vyanzo halisi vya habari(Balance Sourcing), kujiridhisha na uhalisia (Indepth Reporting), mbinu za kutumia(Methods used) na Style ya kuanza kuandika habari husika.
• Kuelimisha vijana wa kike na kiume na wazee kwa ujumla wao juu ya ujasiliamali na jinsi ya kujiunga na vikundi na kuwaelekeza katika mashirika yanayotoa mikopo kwa makundi hayo.
• Kuibua vyanzo vinavyochangia kutokuwa na huduma bora za Afya ikiwemo matatizo ya wanawake, unyanyasaji wa kijinsia, Kilimo, Maji, Miundombinu na kusuluhisha migogoro katika jamii na kupatanisha.






Reba ibigo mwegeranye