Nakumbuka siku moja aliyekuwa Raisi wa Msumbiji wakati akiaga Watanzania...kipindi cha Mzee Mkapa alipokuwa akijibu hotuba ya Mkapa(ya Kiingereza) yeye alijibu kwa Kiswahili sanifu alisema huku akicheka."Maendeleo tunayoyafanya Msumbiji tumeiga sera na mipango yote ya Tanzania wakati tukiwa Nachingwea. Sisi Msumbiji ndio tunapaswa kujifunza zaidi kutoka Tanzania". Kwangu mimi nilijisikia aibu sana kama Mtanzania.
Sisi Watanzania kinachotumaliza ni ubinafsi wetu hasa Viongozi.Kila mtu anataka kuwa Bill Gate.....kwa pesa ya KODI. Hakuna miradi mipya ya uzalishaji, tekinolojia mpya kila mmoja anataka kutembelea (Hummer, Vog)