Shirika la MUWWE Women/ Youth Povery Reduction Organisation, imeanzishwa mwaka 2003 na kusajiliwa Wizara ya mambo ya ndani Usajili No. SO14024 mwaka 2005, pia likasajiliwa usajili wa Asasi (NGO) Office ya Makamu wa Rais mwaka 2006 na kupata cheti cha compliance certificate.
KAZI ZA ASAS YA MUWOYOPORO - NGO NI:
(1) Kutoa elimu ya kuzuia maambukizi ya UKIMWI na VVU pia kuwahudumia walioathirika na UKIMWI.
(2)Kutoa elimu ya kujiajiri ikiwa ni wajasiliamali kupita vita uamsikini na kujenga nyumba kwa gharama nafuu
(3) Kutoa elimu kwa jamii, kutunza mazingira pamoja na kupanda miti na kutunza uoto wa asili na vyanzo vya maji.
(4) Kuelimisha jamii kuwa na maendeleo kwa kuanzisha miradi endelevu kwa kuunda vikundi na kuwa na viwanda vidogo vya uzalishaji pamoja na kusaidia wakulima wadogo wadogo ili kupunguza umasikini.
(5)Kusaidia yatima na watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi pamoja na kusaidia wazee.
Kutetea haki za binadamu katika jamii na pamoja na kutatua migogoro kati ya wakulima na wafugaji.
Lengo ni kuhakikisha jamii inapata huduma bora tena endelevu. Kwa kupunguza umasikini na magonjwa kwa vijana na akina mama Tanzania. Mtazamo kuwa na miradi endelevu kwa vijana na akina mama kupita vita umasikini na kuondoa maradhi. Miradi: Shirika la MUWWE Women / Youth Poverty Reduction Organisation. Mwaka 2005 - 2006 tulihamasisha jamii kusafisha Ziwa Victoria mwambao kwa kutoa magugu maji pamoja na kuwa na vitalu vya kuotesha miti na kuwagawia jamii na mashule pia kuwapatia elimu ya upandaji na utunzaji miti kuwa endelevu. Hatukuwa na ufadhili, tuliendesha mradi kwa nguvu kazi za viongozi na wanachama wa asasi.
Mwaka 2007 - 2010 Shirika la Muwoyoporo kwa ufadhili wa wanachama wake tulioa elimu kwa wavuvi wadogo kwa kuwapatia nyenzo za kuwasaidi kuvua kwa utaalamu ili kujiongezea kipato kupiga vita uamsikini.
Mwaka 2011 tumekuwa wasuluhisi wa migogoro kati ya wakulima na wafugaji eneo la vijijini. Pia viongozi wa asasi wamepatiwa mafunzo ya kubuni mradi na jinsi ya kuwa na kumbukumbu za utumaji fedha. Mafunzo haya yamefadhiliwa na The Foundation for Civil Society toka Dar es Salaam Tanzania
Team ya Viongozi wa asasi:
(1)Mkutano Mkuu- wote
Bodi ya asasi watu- 7
Kamati tendaji watu 5
Kamati ya mipango - watu 3
Kamati ya fedha - watu - 4
Kamati ya elimu watu- 3
A. Mwenyekiti mtendaji Katibu Mkuu Mhazini.
B. Mkurugenzi wa Asasi Mratibu mipango Mhasibu Mkuu Afisa elimu Makaguzi wa nadani.
Shirika la Muwwe Women / Youth Poverty Reduction Organisation ina majukumu makubwa yanayogusa kila hitaji la jamii ni ombi letu kushirikiana na kila asasi yeneye moyo wa kusaidia jamii tushirikiane na tunaomba kupewa umuhimu wa kupatiwa ruzuku ili tuzidi kuboresha ufanisi makini katika kutoa huduma kawa jamii
Ahsante
PENINA B. MACHUMU
PROGRAM OFFICER MUWOYOPORO - WGO
MUSOMA - MARA
TANZANIA EAST AFRICA