Log in
MWANAKWEREKWE ENVIRONMENTAL ETHICS AND CULTURAL ORGANIZATION (MEECO)

MWANAKWEREKWE ENVIRONMENTAL ETHICS AND CULTURAL ORGANIZATION (MEECO)

Zanzibar, Tanzania

Parts of this page are in Swahili. Edit translations

large.jpg

Vijana wa MEECO talent group nao hawakombali kushiriki katika uhamasishaji wa utunzaji wa Mazingira katika mikoko katika kijiji cha Unguja ukuu

large.jpg

Wanachama wa MEECO wakiwa katika safari yao ya kwenda kuhamasisha utunzaji na uhifadhi wa mazingira katika kijiji cha Unguja Ukuu

large.jpg

Wanachama wa MEECO wakiwa na sheha wa Shehia ya Pangawe katika dhiara ya kuhamasisha utunzaji wa mazingira katika kijij cha Unguja ukuu Mkoa wa Kusini Unguja

large.jpg

Uwongozi wa jumuiya ya MEECO ukishirikiana na Kamati ya ulinzi na usalama wa Shehia ya Mwanakwerekwe wakiwa Ofisini skuli ya Sekondari Mbarali katika jitihada za kutatua tatizo la uvutaji wa bangi kwa baadhi ya wanafunzi wakorofi wa skuli hiyo!!

large.jpg

Mwenyekiti wa kitengo cha Mazingira ambaye pia ni diwani wa viti maalum akihutubia moja ya vikao tendaji vya jumuiya hiyo

large.jpg

Moja ya vijana walioathirika kutokana na ukosefu wa elimu ya maadili ndani ya Mji wa Mwanakwerekwe. Vijana hawahawa huwa ndio waharibifu wakubwa wa mazingira hususan kwa uchimbaji wa mchanga katika mji huo na maranyigi ni vigumu sana kuwakabili kwani huwa na silaha kama mapanga,visu nk. MEECO inawakati mgumu na kazi nzito kuhakikisha suala hilo linaondika kabisa katika jamii ya Zanzibar

large.jpg

Moja ya Vikao vya MEECO katika kujadili mas-ala ya utendaji wa jumuiya hiyo kikihutubiwa na Mshauri wa kigeni wa MEECO Bi. Katrina

large.jpg

Katibu wa MEECO Nd. Suleiman J. Pandu akiwa na Mshauri wa kigeni wa jumuiya hiyo Bi. Katrina moja katika dhiara zao za kuangalia hali ya mazingira katika kijiji cha Makunduchi kilioko mkoa wa kusini Unguja

large.jpg

Shimo kubwa linalochimbwa Mchanga na vijana waharibifu wa mazingira liliopo mtaani katika mji wa Mwanakwerekwe-Taveta ni miongoni mwa athari za uharibifu wa mazingira katika mji huo

large.jpg

Mchanga uliochimbwa katika maeneo yasioruhusika ukiwa umekwisha uzwa. Hali ambayo inachangia wa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira katika Mji wa Mwanakwerekwe