Injira
Masasi Non-governmental Organization Network

Masasi Non-governmental Organization Network

Masasi, Tanzania

Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Igiswayire. Edit translations

         Kupitia mradi wa Utetezi, jinsia na UKIMWI unaofadhiliwa na GIZ, MANGONET imeendesha mafunzo mbalimbali katika Wilaya ya Masasi. Tarehe 20/4/2012 MANGONET iliendesha mafunzo ya Afya ya uzazi, jinsia na UKIMWI katika ukumbi wa mikutano uliopo katika ofisi ya MANGONET, mafunzo hayo yalishirikisha washiriki mbalimbali kutoka kila Kata za Wilaya ya Masasi.

      Mwezeshaji wa mafunzo hayo alikuwa ni Bi. Tryphonia Malibiche mkunga wa Hospitali ya Wilaya Mkomaindo, idadi ya washiriki alikuwa 54 (KE 28 na ME 28).

TAARIFA FUPI YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA UTETEZI, JINSIA NA UKIMWI.

Mtandao wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali Wilayani Masasi (MANGONET) umetekeleza mradi wa kupambana na maambukizi ya UKIMWI kupitia shughuli za utetezi jinsia na UKIMWI chini ya ufadhili wa shirika la Ujerumani GIZ.

Kwa mkoa wa Mtwara mradi huu umetekelezwa katika Wilaya mbili za Masasi (MANGONET) na Manispaa ya Mtwara (MTWANGONET) baada ya utafiti mbalimbali kuonyesha kuwa maeneo haya yameathiriwa sana na maambukizi ya UKIMWI. Mradi huu umefanywa kwa muda wa miaka miwili, yaani kuanzia Octoba 2010 hadi Septemba 2012.

Kwa MANGONET mradi umefanyika kwa Asasi 6 ikiwemo MANGONET yenyewe asasi hizo ni kama ilivyoonyeshwa kwenye kiambatanisho.