Injira
Marafiki wa Elimu Dodoma (MED)

Marafiki wa Elimu Dodoma (MED)

Dodoma, Tanzania

Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Igiswayire. Edit translations

large.jpg

Wanafunzi kutoka shule za msingi za,Mvumi misheni,Mvumi co,ed,Nyerere,Ilolo,Ndebwe,Mvumi makulu,,Chalula na Muungano. Wakifuatilia mafunzo juu ya chaguzi za Demokrasia na uundwaji wa mabaraza mashuleni,kutoka kwa maafisa wa shirika la Marafiki wa Elimu Dodoma hawako pichani,ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa HAKI ZANGU SAUTI YANGU unaoendeshwa na shirika hili katika shule 14 za msingi na 6 za sekondari zilizopo Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma,mradi ambao unafadhiliwa na OXFA GB.

large.jpg

Shirika la Marafiki wa Elimu Mkoani Dodoma pia hutumia vyombo vya habari kutoa Elimu kwa jamii kuhusiana,Elimu,Demokrasia na Utawala bora,kama inavyoonekana kwenye picha.

large.jpg

Mratibu wa shirika la Marafiki wa Elimu Dodoma,nd.Davis Makundi akiendesha mafunzo ya chaguzi za Demokrasia na uundwaji wa mabaraza katika shule 16 za msingi na 4 ZA sekondari zilzopo Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma,ikiwa ni moja ya utekelezaji wa mradi wa HAKI ZANGU SAUTI YANGU unaoendeshwa na shirika hili kupitia ufadhili wa OXFAM GB.

 

                UJIRA WA WALIMU UZINGATIE MAZINGIRA WANAYOPANGIWA

Imekuwa ni kama kawaida kusikia ya kuwa wapo walimu wengi  wanaoshindwa kulipoti kwaenye vituo vya kazi kutokana na sababu mbalimbali ikwemo ugumu wa mazingira ya kufanyia kazi, vitendea kazi na hata uhakika wa maslai yao kuwafikia kwa wakati.

Hayo yamezungumzwa na wadau wa elimu  mkoani Dodoma wakati wakiwa kwenye shughuli za ugawaji wa msaada wa vitabu katika wilaya ya chamwino mkoani humo. Akiongea na mratibu wa shirka lisilo la kiserikali la marafiki wa elimu mkoani Dodoma Mwl Abinery Malogo wa shule ya msingi Wiliko alisema wamekuwa wakipata shida sana hasa pale wanapojikuta asilimia zaidi ya 25% ya mishahara  yao inatumika katika nauli katika kipindi kinapofika cha kwenda kuchukua mishahara yao. Aidha mwl malogo alilalamikia pia kuona walimu waliopo mijini waapewa kiwanngo sawa na wale wanaoishi vijijini.                                                                                            

                                                                                                                                                  (Moja kati ya ofisi ya walimu kama inavyoonekana katika shule ya msingi Mzula iliyopo wilayani Chamwino)

 kitu ambacho amedai  kuwa  hali hiyo imekuwa ni tatizo kubwa na linaloonekana kama ni uonevu kwani kwa wao kukubali kutumikia maeneo ya vijijini.

Hakika kama walimu waliopo vijijini wangekwa wanapatiwa kiwango kikubwa tofauti na wanachopewa sasa hakika walimu wengi wengi ambao wamekuwa wakipangiwa katika maeneo ya vijijini wangekuwa wanaripoti kwa wakati na kufanya kazi kwa moyo mmoja na kuwa na uhakika wa kuwa na maisha bora na ya mfano kwa wote wanaopenda kuwa walimu.

Mbali na ugumu wa mazingira pia baadhi ya vitu vilivyoonyesha kuhatarisha maisha ya wlimu hao ni pamoja na uchakavu wa majengo, kama vile ofisi za walimu,vyoo kutokuwa na madarasa ya kutosha kitu kinachowalazimu baadhi ya wanafunzi kufundishiwa sehemu zisizo kidhi matakwa yao, pia ukosefu wa madawati ya kukalia wanafunzi imeonekana ni kikwazo katika maeneo mengi wilayani humo. Mbali na ukosefu wa madawati lakini pia wapo wanafunzi wanaosomea chini ya miti kitu ambacho kinaonekana kama ni hadithi za kale, lakini ukweli ndivyo ulivyo kwenye maeneo mengi ya vijijini mkoani Dodoma.

 

Asema hata akifaulu shule ya Kata hasomi:

Mwanafunzi wa shule ya msingi Mvumi Makulu Elia Mkwila (13) amesema hayuko tayari kusoma katika shule za serikali za kata kutokana na elimu inayotolewa katika shule hizo kuto kukidhi mamhitaji ya elimu bora nchini. Kijana Mkwila ayasema hayo alipofanya mahojiano mafupi na Mrartibu wa shirika la Marafiki wa Elimu Dodoma (MED) Bw. Davis Makundi wakati wa kukabidhi vitabu kwenye shule hiyo iliyoko katika Tarafa ya Mvumi.

 Hali inaonyesha wazi kuwa kwa sasa hata wanafunzi wenyewe wanaona kuwa hawata kuwa tayari kuona juhudi zao zikiishia katika shule zinazokosa vigezo vya kutoa msaada wa kuwafanya waendelee kuwa bora katika elimu yao. Kutokuwa kuwa kwao tayari kusoma katika shule za kata ni sawa na mtu anaye amua kujitoa mhanga maisha yake kama njia mojawapo ya kuonyesha kutorizika na jambo fulani.

Mwanafunzi huyo mlieleza kuwa katika masomo yake ya darasa la saba amekuwa akifanya vizuri kwenye masomo mengi ila kazi kubwa iko kwenye masomo mawili ya Hisabati na Kiingereza ambayo hufanya vibaya kila mwaka.

 Katika hatua nyinhgine mmoja wa walimu wa shule ya msingi Mvumi Makulu anakosoma kijana nElia ambaye hakutaka jina lake litajwe alieleza kuwa licha ya juhudi kubwa za walimu katika kufundisha, bado ana mashaka makubwa na hai itakavyokuwa kwa wanafunzi wa darasa la saba wakati wa mtihani. “watoto hawa wanahitaji kazi ya ziada katika kuwasaidia katika mtihani wao wa darasa la saba kutokana na masharti ya kutumia karatasi za (OMR)”.

 

MED YATOA SAADA WA VITABU.

Shirika la Marafiki wa Elimu Dodoma MED limetoa msaada wa vitabu vya kiada na kiongozi cha mwalimu vyenye thamani ya zaidi ya Sh. 397,363,300 kwa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino kwa lengo la kuboresha Elimu katika Wilaya hiyo. Mdsaada huo wa vitabu vya masomo ya kiingereza, Hisabati na Jiografia utawanufaisha walimu na wanafunzi wa shule 82 za Halmashauri ya Chamwino iliyoko Mkoani Dodoma.

Akitoa shukrani kwa niaba ya wanafunzi wa shule ya msingi ya Handali ambayo ni moja kati ya shule zilizonufaika na msaada huo wa vitatu mwalimu Grace Mtani alisema msaada huo umekuja atika wakati muafaka hasa ukizingatia kuwa utakuwa ni msaada mkubwa hasa kwa wanafunzi wa darasa la saba ambao wapo kwenye maandalizi ya mtihani wa taifa. Akionyesha kuwa nia yao ni kutaka kusaidia jamii inayowazunguka kwa wakati mratibu wa shirika hilo la marafiki wa elimu mkoani Dodoma Bw. Davis Makundi amesema msaada huu ni mwanzo tu katika halmashauri hiyo ya Chamwino,kwani wamejipanga vizuri kwa kushirikiana na wadau wengine katika kuboresha elimu ya wanaChamwino.

Mbali na msaada huo wa vitabu katika wilaya hiyo, MED imeweza pia kushuhudia matatizo mengi yanayowakabiri wanafunzi wengi katika wilaya hiyo hasa likiwemo tatizo la ukosefu wa madawati kitu ambacho kimeonekana kama kuwa  ni tatizo lililoanza kuzoeleka katika maeneo mengi katika wilaya hiyo, pia limejtokeza tatizo kubwa linalohatarisha afya za wanafunzi wengi katika shule nyingi katika wiaya ya chamwino ni ukosefu wa vyoo, vyumba vya madarasa, madawati, zana balimbali za lujifunzia na kufundishia pamoja na mafunzo ya walimu kazini.             

MED KUGHARAMIA MITIHANI YA MAZOEZI IV KIKUYU SEKONDARI.

Shirika la Marafiki wa Elimu Dodoma MED litagharamia uchapishaji wa mitihani ya Mazoezi kwa wanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Kikuyu ili kuongeza maarifa kwa wanafunzi wa shule hiyo wanaotarajiwa kufanya mtihani wa kuhitimu kidato cha nne mwezi Novemba, 2013.

Uamuzi huo wa MED umetolewa katika kikao cha pamoja kati ya wazazi, wanafunzi na walimu wa kidato cha nne wa shule hiyo kilichoitishwa kwa lengo la kutathimini matokeo ya kidato cha Nne 2012 na kujipanga kwa ajili ya matokeo ya mtihani wa mwaka huu.

Akichangia katika kikao hicho Mratibu wa MED Bw.Davis Makundi Amesema kuwa ili kuhakikisha kuwa wahitimu wa mwaka huu wanafanya vizuri  hapana budi jamii,walimu,wazazi,wanafunzi na wadau mbalimbali kuungana pamoja kuwawezesha wanafunzi kupata mazoezi ya mara kwa mara ya majaribio ya mitihani ya kujipima

Akiwasilisha taarifa ya maandalizi ya mtihani wa kidato cha nne 2013 kwa wazazi mwalimu wa taaluma shuleni hapo Francis Tumaini  Wambura amesema kidato cha nne kwa mwaka huu kina wanafunzi 168 ambao wanatarajiwa kufanya mtihani wa kuhitimu kidato cha nne.

Kwa mujibu wa taarifa za idara ya taaluma shuleni hapo kati ya  wanafunzi 168 wanaotarajiwa kufanya mtihani wa kidato cha nne mwaka huu wanafunzi 21 mpaka sasa hawaja sajiliwa kutokana na utoro.

Aidha taarifa zimeongeza kuwa  zoezi la kulipia ada ya mtihani wa taifa linalotarajia kukamilika tarehe 28 mwezi huu wa pili inaonekana kusuasua ambapo wanafunzi 40 pekee ndio waliolipia ada hiyo hadi sasa.

large.jpg

Wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Kambarage Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma wakiwafurahia wafanyakazi wa shirika lisilo la kiserikali la Marafiki wa Elimu Dodoma hawako pichani walipokwenda kutembelea shule hiyo ikiwa ni mojAwapo ya ufuatiliaji wa mradi wa HAKI ZANGU SAUTI YANGU.

large.jpg

Afisa mipango wa MED Luhaga Makunja,kulia akimsikiliza mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Kambarage iliyopo katika Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma mwalimu Emmanuel Ndepeka wakati wa ufuatiliaji wa utekelezaji wa mradi wa HAKI ZANGU SAUTI YANGU katika shule hiyo.

NDEBWE YALETA MABADILIKO KATIKA DEMOKRASIA.

Na. MED Information Unit

Shule ya Msingi Ndebwe iliyoko katika Halmashauri ya Wilaya ya Dodoma imeonesha matokeo mazuri katika uchaguzi wa kidemokrasia kwa kumchagua msichana kuwa Kiranja Mkuu wa shule hiyo na kuwashinda wavulana waliokuwa wapinzani wake wa karibu.

Rosemary Masaka (pichani) mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya Msingi Ndebwe alipata ushindi huo baada ya kuamua kugombea nafasi ya kiranja Mkuu kufuatia mafunzo ya elimu ya kidemokrasia katika kuwapata viongozi wa shule yaliyotolewa na shirika la Marafiki wa Elimu Dodoma (MED) kupitia mradi wake wa Haki zangu Sauti Yangu unaofadhiliwa na shirika la Oxfam GB.

Akiongea na maafisa wa MED mtoa habari hizi ambaye hakutaka jina lake litajwe alieleza kuwa hii ni mara ya kwanza shule yao kupata kiranja Mkuu mwanamke. “zamani tulikuwa tuna chagua viongozi sisiwenyewe walimu na kuwatangazia wanafunzi” alisema mtoa habari huyo.

Aliongeza kuwa awali shule ilikuwa zikichagua viongozi kwa cheo cha kaka Mkuu na Dada Mkuu ambapo sasa utaratibu umebadilika na kuwapata viongozi hao kwa cheo kipya cha kiranja Mkuu bila kujali jinsia.

Mradi wa My Rights My Voice ni mradi wa miaka mitatu (2012 – 2014) unaotekelezwa katika shule 16 za msingi na 4 za sekondari katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino kwa lengo la kuimarisha ari ya watoto kujifunza na kuanzisha mabaraza ya wanafunzi kwa kuendesha chaguzi za kidemokrasia katika kuwapata viongozi wake.