Furaha ya Wanawake Wajasiriamali kwa Viziwi Tanzania (FUWAVITA) ni Asasi iliyosajiriwa na kutambulika Kisheria kwa Namba 17120 na inawajumbe 17. Asasi hii ilianzishwa kutokanana na Utafiti uliofanywa na Bi Aneth Gerana ambapo aliwezeshwa na Shirika la Maendeleo ya Walemavu (ADD) Kutafiti katika Asasi mbalimbali zinazowahusu Viziwi , na kugundua kuwa Asilimia 49‰ ya Wanawake Viziwi wamepatwa na Matukio ya Uzalilishwaji na Unyanyasaji wa kijinsia ikiwa ni pamoja nakukabiliwa na hali Ngumu ya Maisha kwani wengi wao wanafamilia ambazo zinawategemea hivyo ndio hukawa Mwanzo wa kuzaliwa kwa Chombo hiki cha kuwakomboa Wanawake Viziwi ili kutetea haki zao kupitia Ujasiriamali.
Asasi ilianza shughuli zake mwaka 2008 lakini rasmi mwaka 2010 ilipopata usajili kamili Waanzilishi ni Kiziwi aliyehitimu Chuo Kikuu cha Dar es slaama ambaye ni wa kwanza kuweza kufika chuo kikuu Tanzania kwa kushirikiana na Wanzake waliomaliza katika Vyuo binafsi vya Ualimu ambao hawakufanikiwa kupata Ajira kutokana na Ukiziwi wao. Tanzania Bara kuna asasi nyingi za kiraia ambazo zimekuwa zinatetea wanawake Nchini lakini hakuna hata moja iliyosimama imara kusimamia na kutetea mwanamke Kiziwi