Envaya
Parts of this page are in Swahili. Edit translations

 Centre for Children and young people Development  linaungana na dunia pamoja na     watanzania  wote kusheherekea siku ya wanawake duniani March 2012. Siku hii pekee inatupa nafasi ya kutambua mchango wa wanawake  katika harakati ya kumkomboa mwanamke. Centre for Children a Young people and Adult Development  linapenda kuadhimisha siku hii kwa  kuikumbusha jamii ushiriki wa pamoja kwa kupinga unyanyasaji na ukatili kwa wanawake na watoto ambayo huadhimishwa kila mwaka mwezi December. Asasi inatambua mchango wa akina baba , vijana , watoto katika nguvu za pamoja katika kuleta mabadiliko na maendeleo ya kisasa.

Asasi   inaungana  na  mashirika mengine  kutambua mchango wao katika kutetea  na kupigania haki ya mwanamke. Mwanamke wa leo ni shupavu , jarisi na ameonesha anao uwezo  wa kufanya mambo mengi bila kuwa tegemezi . Wanawake wa Tanzania ni mhimili wa Taifa letu ambalo ndilo linajenga maendeleo ya nchi yetu. Daima tusonge mbele.

March 8, 2012
« Previous Next »

Add a comment

Your name:
Your location:
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.