Zantel na TEYODEN wafanya programu ya ushirikiano ili kuwezesha vijana kuongeza kipato chao na kuwa na uwezo kukabiliana na changamoto za kimaisha.
Vijana wa kata ya kilakala wamefanya kikao cha pamoja na katibu mtendaji wa TEYODEN na mhamasishaji jamii wa kampuni ya ZANTEL.Lengo la kikao ni kufanya majadiliano ya pamoja na kukubaliana juu ya ushirikiano wa pamoja kati ya pende hizo mbili.mhamasishaji wa ZANTEL alieleza kuwa vijana wanaweza kujiunga na kampuni hiyo ya simu na kupata faida ya asilimia zaidi 10 kwa uuzaji wa bidhaa za kampuni hiyo wakati pia wakiongeza pato lao kama kikundi.Akiongeza maelezo ya mhamasishaji bwana Katibu mtendaji wa TEYODEN bwana Yusuph Kutegwa aliwataka vijana wa Kilakala kuwa mfano kwa kulichukulia maanani suala hili la kijasiriamali ili kuleta tija kwa vituo kuliko kukaa na kuwezeshana kielimu pekee.Zoezi hili la Vikao na vijana litaendelea katika kata za Azimio,Mtoni,Mbagala,Toangoma,Kibada,Vijibweni na pemba mnazi.
TEYODEN yafanya mafunzo ya VICOBA kwa wasichana 80 waliozaa chini ya umri na waliosahalika na jamii (Ma mama wadogo) kutoka katika kata 4 za Azimio,Mtoni,Kibada na Vijibweni.Pamoja na walengwa hao walikuwepo mentors(walezi wa wasichana katika kata) 16 nao wakipata elimu hiyo ya VICOBA.Mafunzo hayo yalitanguliwa na mafunzo ya mafunzo ya siku 2 kuhusu stadi za maisha na elimu ya ujasiriamali yaliyofanyika kwa wasichana katika kata nne za mradi zilizotajwa hapo awali.Akifungua mafunzo afisa wa maendeleo ya vijana wa Manispaa ya Temeke aliwataka vijana kuwa watulivu na wasikivu na kuyafanyia kazi mafunzo watakayopata ili waweze kuibua miradi katika vikundi vya watu 10 ambavyo vitawezeshwa mitaji na ofisi ya TEYODEN.
"Nawapongeza sana TEYODEN kwa kuwa na wazo la kubuni mradi huu kwa kuwa mwanzoni katika vikao vyao vya miradi iliyopita niliwasahuri kufanya mradi tangible(wenye matokeo ya kuonekana) haya ni matokeo ya kuufanyia kazi kwa vitendo ushauri niliyowapa."alisema bi Afisa vijana bi Anna Marrica
"Mradi huu wa mama wadogo waliosahaurika utawawezesha wasichana husika kupata elimu,kujadili changamoto za maisha yao ya kila siku na baadae kupatiwa mitaji kwaajili ya miradi yao itakayoibuliwa katika vikundi.Mtumie mitaji kwa shughuli zilizokusudiwa na si vinginevyo."aliongeza bi Anna Marrica
Wawezeshaji katika mafunzo haya walikuwa ni bwana Issa Tunduguru ambae ni Mkurugenzi wa Shirika la Poverty Fighting Tanzania na bwana Ally Manjasi ambae ni mkurugenzi wa Fedha wa shirika hilo.
Katika mafunzo hayo pia tulipata wageni kutoka chuo kikuu cha Dar-es-salaam na mwanafunzi kutoka ujerumani ambae yupo Tanzania kujifunza kwa vitendo kazi za kijamii.
MENTORS(walezi) wa wasichana wa mradi wa kujenga uwezo wa wasichana waliosahaurika wakiwa katika picha ya pamoja na msimamizi wa mradi,mratibu na wawezeshaji wa mafunzo hayo 


