Log in
Temeke Youth Development Network

Temeke Youth Development Network

Temeke/Chang'ombe, Tanzania

Parts of this page are in Swahili. Edit translations

TEYODEN na TYVA waongeza nafasi za ushirikiano

TEYODEN na Tanzania Youth Vision Association(TYVA),leo walifanya mkutano wa kuzindua ajenda ya vijana 2010,wakishirikisha asasi nyingine za vijana katika ukumbi wa Karimjee leo ambapo mada ilwasilishwa na mkurugenzi wa hakielimu,Bibi Annastazia Rugaba ambaye pia alibainsha changamoto zinazowakabili vijana kuelekea uchaguzi mkuu na katika harakati za kujikomboa kiuchumi,kisiasa na kiafya.

Kisha baada ya mawasilisho hayo,vijana walipata nafasi ya kufanya majadiliano yaliyopelekea kuwepo kwa maazimio ambayo baadaye yatapelekwa kwa makatibu wa vyama vya siasa nchini,yakipendekeza nini kifanyike kwa ajili ya vijana,mara chama chochote kitakachoingia madarakani kitapaswa kiyafanyie kazi.

Katika mojawapo ya maazimio hayo ni kuhusu kuwepo kwa ufuatiliaji wa mapendekezo hayo hata baada ya uchaguzi kwa wale waliochaguliwa.

TEYODEN washiriki katika siku ya vijana kimataifa Agosti 12

Katika kuendeleza sera yake ya ushirikiano na mashirika mengine ya vijana TEYODEN ilishiriki katika maadhimisho na shirika la vijana la Umoja wa Mataifa (YUNA) kaika kuadhimisha siku ya vijana kimataifa.Maadhimisho hayo yalifanyika katika ukumbi wa Apeadu  unaomilkiwa na Umoja wa Mataifa.

Siku hiyo ya vijana ilienda sanjatri na uzinduzi wa mwaka kijana uliozinduliwa na wazirti wa kazi,Ajira na maendeleo ya vijana,mheshimiwa Al-Haji Juma Athuman Kapuya,ambapo alibainisha changamoto zinazowakabili viaja katika ajira kuwa ni pamoja na kutokuwa waaminfu pale wanapopata ajira,kutofanya kazi kwa kujituma,uadilifu katika maeneo ya kazi na kukosa ujzi unaopelekea kutokujiamini wakati wanapokuwa kwenye usaili wakazi.

Kauli mbiu ya mwaka huu ilikuwa ni "mwaka wetu,Sauti yetu", iliyokuwa na kchwa cha habari,"Majdiliano na makubaliano ya pamoja".

Kamati ya Utendaji TEYODEN yajipanga kutekeleza mradi wa Utetezi wa Mabinti wanaofanya kazi kwenye baa

Katika ile hali ya kuwajali wasichana wanaofanya kazi kwenye baa mbalimbali hapa jijini Dar Es Salaam,TEYODEN imeonelea ni vema ikajitahidi kuwatafutia suluhu ya maonevu wanayofanyiwa na wamiliki wa baa.

Katika kikao cha kamati ya utendaji kilichofanyika jumamosi ya tarehe 12 Juni 2010 katika ofisi za TEYODEN,kikihudhuriwa na mwakilishi kutoka Taasisi ya Maendeleo Shirikishi kwa vijana Arusha ( TAMASHA) yenye makao yake makuu katika jiji la Arusha,kaka Churchill Winston ambao ndio watakaokuwa wafadhili wa mradi huo na TEYODEN wakiwa ni wataalamu watafanya utafiti katika kata nne za manispaa ya Temeke ambazo ni Kurasini,Azimio, Keko na Mbagala katka baa zote zilizopo katika katika kata hizo ili kbaini ni changamoto zipi wanazokabiliana nazo mabinti hawa na jinsi ya kuzitatua wakiwashirikisha wamiliki wa baa hizo,wadau wa maendeleo katika manispaa ya Temeke na vijana mbalimbali.

Kabla ya kuingia katika mchakato huu kwanza yatakuwepo mafunzo ya namna ya kufanya utafiti huo.Mradi huo utakuwa ni wa mwaka mmoja.Kinachosubiriwa kwa sasa ni kibali kutoka wizara ya Sayansi naTeknolojia ambacho huenda kinatarajiwa kupatikana ndani ya mwezi huu.

TEYODEN itaendelea kushirikiana na mashirika mengine ikiwa ni katika kuimarisha mahusiano yake na asasi nyingine ndani na nje ya nchi.
TAARIFA YA MTANDAO WA VIJANA MANISPAA YA TEMEKE KWA KIPINDI CHA UTEKELEZAJI CHA MEI JUNI 2009.

KUTOKA: MTANDAO WA MAENDELEO YA VIJANA MANISPAA YA TEMEKE (TEYODEN)
KWENDA KWA: MKURUGENZI WA HALMASHAURI MANISPAA YA TEMEKE

1.0 UTANGULIZI
Temeke Youth Development Network (TEYODEN) ni Mtandao wa Maendeleo ya Vijana unaoendeshwa na vijana wenyewe miongoni mwa mitandao 19 iliyotokana na programu ya vijana nje ya shule iliyotekelezwa na Halmashauri 19 nchini Tanzania kwa ufadhili wa UNICEF. Mtandao umesajiriwa chini ya ofisi ya Makamu wa Raisi, namba ya usajiri ni OONGO/0170.TEYODEN inasimamia na kuratibu shughuli zake katika vituo 24 vya vijana vilivyopo katika kata 24 za Manispaa ya Temeke.

1.1 Dira ya TEYODEN
Kuwa Mtandao bora wa Maendeleo ya vijana Tanzania unaowezesha vijana kuwajibika vya kutosha katika kubadili tabia hatarishi na kujiletea
katika vituo vya vijana vya kata na asasi wanachama wa TEYODEN.

1.3 Lengo kuu la TEYODEN
Kuchangia juhudi za kuleta maendeleo endelevu na thabiti ya tabia na mienendo ya vijana katika mahusiano yao hususani katika masuala ya ngono ili kupunguza kasi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi na kutekeleza mkakati wa kupunguza umasikini ili kufikia malengoya milenia (MDG`s)

2.0 SHUGHULI ZILIZOFANYIKA
• Katika miezi 3-(Julay -sept)ya utekelezaji, shughuli zifuatazo zilitekelezwa:

2.1 Ufuatiliaji wa shughuli za vijana baada ya mafunzo ya kujenga uwezo
Baada ya mchakato wa mafunzo ya kujenga uwezo vijana wawakilishi walirudi katika kata zao na kufanya utekelezaji katika kata zao.
Katika ziara ya ufuatiliaji wa matokeo makuu ya mradi (project impact) mambo yafuatayo yalijitokeza
Vijana wanaendeleza matunda ya mradi kwa kuendeleza dhana ya kujitegemea mfano kata ya Vituka, Charambe, Azimio na miburani wapo katika michakato ya kufungua akaunti japo kuwa benki zinamasharti magumu kwa vikundi vidogo vya kijamii.

2.2 Uibuaji wa mradi wa kuamsha ari ya uwajibikaji na ushiriki wa vijana katika masuala ya kijamii na kimaendeleo.
Katika kipindi cha utekelezaji wa taarifa idara ya tafiti na takwimu iliendesha vikao 4 vya vijana vya kuibua mradi wa kiwango cha kati na kuuwasilisha The Foundation for civil society kwaajili ya maamuzi ya kupatiwa fedha.mradi huu unajulikana kama kuongeza ari ya uwajibikaji kwa vijana katika shughuli za kijamii na maendeleo manispaa ya Temeke.

2.3 Mjadala wa vijana centre 1
Kama ilivyo kawaida kwa vijana wa TEYODEN kufanya midahalo kila jumamosi mbili katika mwezi.katika kipindi cha taarifa vijana walifanya midahalo 6 na wastani wa vijana 120 walishiriki katika midahalo hiyo.

2.4 Mafunzo ya kujenga uwezo wa watendaji wa TEYODEN.

Katika kipindi cha taarifa viongozi na wanachama wa TEYODEN walipata nafasi ya kuhudhuria mafunzo ndani na nje ya mkoa wa Daresalaam kama ifutavyo:-

Ushiriki wa vijana 30 katika mafunzo ya ujasiriamali ukumbi wa vijana centre ilala
Lengo la mafunzo -
Lengo la mafunzo haya ni kuinua uelewa wa vijana katika stadi za ujasiriamali ili kukuza biashara zao na kujiepusha na makundi rika na kuondoa uamsikini miongoni mwao.

Ushiriki wa vijana 30 katika mafunzo ya ujasiriamali yaliyoandaliwa na Safer Cities kupitia Sustainability Cities.yalioyofanyika katika ukumbi wa karimjee.
Lengo la mafunzo -
Lengo la mafunzo haya ni kuinua uelewa wa vijana katika stadi za ujasiriamali ili kukuza biashara zao na kujiepusha na makundi rika na kuondoa uamsikini miongoni mwao.

Ushiriki wa mweka hazina wa TEYODEN katika mafunzo ya uhasibu MTCDC chini ya ufadhili wa The Foundation for Civil Society.
Lengo la mafunzo:-
Lengo la mafunzo haya ni kuwezesha washiriki kuwa na uwezo wa washriki kuendesha shughuli za mahesabu katika Asasi zao kwa uwazi na uwajibikaji.

Ushriki wa mwakilishi mmoja kutoka TEYODEN katika mafunzo ya ushiriki na ushirikishwaji wa vijana katika shughuli za kijamii mafunzo yaliyofanyikia morogoro.
Lengo la mafunzo:-
Lengo la mafunzo haya ni kuwezesha washiriki kujua haki na wajibu wa jamii kushiriki katika shughuli za kijamii na kuwa wawezeshaji kwa vijana wengine

Ushiriki wa mwakilishi mmoja wa TEYODEN katika mafunzo ya mbinu za kutunisha mfuko wa asasi yaliyofanyika mbezi garden jijini Daresalaam kwa ufadhili wa The Foundation For Civil Society.

2.5 Ushiriki wa mwakilishi mmoja wa TEYODEN katika safari ya upandaji mlima iliyoandaliwa na Kilimanjaro initiative kupitia Safer Cities.

2.6 Uandishi na uwakilishi wa Andiko la miradi kwa wafadhili
TEYODEN katika kipindi cha utekelezaji wa taarifa hii imeibua kutayarisha na kuwasilisha maombi yafutayo ya fedha:-

-Mradi wa uchimbaji wa kisima cha umwagiliaji katika kambi ya vijana ya Somangira. Mradi huu umewasilisha katika ubalozi wa ujerumani.

- Mradi wa kudarizi na ushonaji kwa vijana wa kike walio nje ya shule 80 kutoka kata 5 za Azimio, Makangarawe, Sandali, Vituka na Tandika.Mradi huu umewasilishwa katika ofisi za ubalozi wa Ujerumani.

3.0 KAZI ZILIZOPANGWA KUFANYIKA
3.1 TEYODEN imepanga kufanya mambo yafuatayo:-

-Kufanya uhamasishaji kwa vijana kuhusu uibuaji wa vijana na watoto wanaofanyiwa ukatili.

-Uhamasishaji kwa vijana katika ushiriki wa nane nane ngazi ya wilaya na ngazi kanda.

-Uhamasishaji wa vijana katika ushiriki wa mkutano wa kambi ya dunia utakaofanyika kuanzia tarehe 21/7/2009 hadi 27/8/2009 katika ukumbi wa sabasaba karume hall.

-Ushiriki wa vijana katika shughuli za uvuvi katika pwani ya bahari ya hindi maeneo ya vijibweni.

4.0 :HITIMISHO
TEYODEN inaamini kuwa mabadiliko kwa vijana yatakayochangia maendeleo ya vijana yanawezekana kama vijana wanapewa uzito unaostahili katika kupanga, kutekeleza, kufuatilia na kutathmini shughuli zinazowahusu. Viongozi wa TEYODEN na vijana siku hadi siku wamekuwa wakiongezewa uwezo katika kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ipasavyo.Hivyo tunawashauri wadau kutumia fursa hii adimu kwa kuwatumia ili kutatua matatizo ya vijana yanayowakabili .
TAARIFA YA MTANDAO WA VIJANA MANISPAA YA TEMEKE KWA KIPINDI CHA UTEKELEZAJI CHA OKT-DES 2009.

KUTOKA: MTANDAO WA MAENDELEO YA VIJANA MANISPAA YA TEMEKE (TEYODEN)
KWENDA KWA: MKURUGENZI WA HALMASHAURI MANISPAA YA TEMEKE

1.0 UTANGULIZI
Temeke Youth Development Network (TEYODEN) ni Mtandao wa Maendeleo ya Vijana unaoendeshwa na vijana wenyewe miongoni mwa mitandao 19 iliyotokana na programu ya vijana nje ya shule iliyotekelezwa na Halmashauri 19 nchini Tanzania kwa ufadhili wa UNICEF. Mtandao umesajiriwa chini ya ofisi ya Makamu wa Raisi, namba ya usajiri ni OONGO/0170.TEYODEN inasimamia na kuratibu shughuli zake katika vituo 24 vya vijana vilivyopo katika kata 24 za Manispaa ya Temeke.
1.1 Dira ya TEYODEN
Kuwa Mtandao bora wa Maendeleo ya vijana Tanzania unaowezesha vijana kuwajibika vya kutosha katika kubadili tabia hatarishi na kujiletea
katika vituo vya vijana vya kata na asasi wanachama wa TEYODEN.
1.3 Lengo kuu la TEYODEN
Kuchangia juhudi za kuleta maendeleo endelevu na thabiti ya tabia na mienendo ya vijana katika mahusiano yao hususani katika masuala ya ngono ili kupunguza kasi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi na kutekeleza mkakati wa kupunguza umasikini ili kufikia malengoya milenia (MDG`s)
2.0 SHUGHULI ZILIZOFANYIKA
• Katika miezi 3-(OKT-DES)ya utekelezaji, shughuli zifuatazo zilitekelezwa:

2.1 Ushiriki wa vijana siku ya UKIMWI duniani tarehe 1/12/2009.
Vijana takribani 300 walishiriki katika maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani .TEYODEN ilipata nafasi ya banda kuonyesha shughuli zake.Shughuli zilizoonyeshwa ni pamoja habari na stadi za maisha ambazo ni muhimu katika kufanya mabadiliko kwa vijana na kujiepusha na maambukizi ya VVU na UKIMWI.

2.2 Ushiriki wa vijana wiki ya vijana tarehe 14/10/2009
Vijana walipata nafasi ya kushiriki katika maadhimisho ya wiki ya vijana ambapo shughuli za msingi katika siku hii ilikuwa ni kuwasisitiza vijana kujiepusha na maambukizi kupima na kujua afya zao.Jumbe mbalimbali kuhusu UKIMWI zilitolewa kupitia ngoma maigizo na muziki wa kizazi kipya.

2.3 Mjadala wa vijana centre 1.
Kama ilivyo kawaida kwa vijana wa TEYODEN kufanya midahalo kila jumamosi mbili katika mwezi.katika kipindi cha taarifa vijana walifanya midahalo 4 na wastani wa vijana 96 walishiriki katika midahalo hiyo.

2.4 Vikao mikutanona warsha za kuoneza uwezo wa vijana na watendaji wa TEYODEN.
Katika kipindi chautekelezajitaarifa hii viongozi wanachama na walengwa wa TEYODEN walipata nafasi ya kushiriki shughuli mbalimbali kaaifutavyo:-

1.) Kiongozi mmoja(katibu) kutoka TEYODEN alipata nafasi ya kushiriki katika kikao cha wadau cha kupitia moduli ya stadi za maisha( 29/12/2009-1/1/2010) iliyofanyiwa marekebisho ya mwisho kabla ya kupigwa chapa na kuanza kutumika.Katika hiki yaliangaliwa mapungufu ya oduli hiyo ili kuendena sawa na mkabala wa stadi za maisha.

2.5kufanya matamasha 3 kwa ushirikiano wa asasi ya FEMINA
TEYODEN kwa kushrikiana na asasi FEMA tulifanikiwa kuendesha matamasha 3 katika kata za Somangila, Mbagala na Azimio.

1.) Lengo la matamasha haya lilikuwa ni:-
Kuwezesha vijana wengi zaidi katika kata zilizopendekezwa kupata nafasi ya kutafakari kwa kina shughuli za ujasiriali ni jinsi zinavyoweza kumuepusha na maambukizim ya V.V.U na UKIMWI.
2.) Shughuli na zilizotumika katika matamasaha hayo:-
Shughuli za maigizo ngoma na muziki wa kizazi kipya

3.) Mafanikio
Vijana walipata nafasi ya kipekee katika kutafakari VVU na UKIMWI na jinsi ya kujiepusha nazo kwa njia ya kujishughulisha na shughuliza uzalishaji mali.Takribani vijana 1500 walijitokeza katika matamasha hayo.

3.0 KAZI ZILIZOPANGWA KUFANYIKA MWAKA 2010
3.1 TEYODEN imepanga kufanya shughuli zifuatazo katika mwaka 2010
1.) Kutekeleza mradi wa kuamsha ari uwajibikaji na ushiriki wa vijana katika shughuli za maendeleo na za kijamii.

4.0 HITIMISHO
TEYODEN inaamini kuwa mabadiliko kwa vijana yatakayochangia maendeleo ya vijana yanawezekana kama vijana wanapewa uzito unaostahili katika kupanga, kutekeleza, kufuatilia na kutathmini shughuli za maendeleo. Viongozi wa TEYODEN na vijana siku hadi siku wamekuwa wakiongezewa uwezo katika kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ipasavyo.Hivyo tunawashauri wadau kutumia fursa hii adimu kwa kuwatumia ili kutatua matatizo ya vijana.vijana tukijiwezesha na kuwezeshwa tunaweza.
TAARIFA YA MTANDAO WA VIJANA MANISPAA YA TEMEKE KWA KIPINDI CHA UTEKELEZAJI CHA JULAY-SEPT 2009.

KUTOKA: MTANDAO WA MAENDELEO YA VIJANA MANISPAA YA TEMEKE (TEYODEN)
KWENDA KWA: MKURUGENZI WA HALMASHAURI MANISPAA YA TEMEKE

1.0 UTANGULIZI
Temeke Youth Development Network (TEYODEN) ni Mtandao wa Maendeleo ya Vijana unaoendeshwa na vijana wenyewe miongoni mwa mitandao 19 iliyotokana na programu ya vijana nje ya shule iliyotekelezwa na Halmashauri 19 nchini Tanzania kwa ufadhili wa UNICEF. Mtandao umesajiriwa chini ya ofisi ya Makamu wa Raisi, namba ya usajiri ni OONGO/0170.TEYODEN inasimamia na kuratibu shughuli zake katika vituo 24 vya vijana vilivyopo katika kata 24 za Manispaa ya Temeke.
1.1 Dira ya TEYODEN
Kuwa Mtandao bora wa Maendeleo ya vijana Tanzania unaowezesha vijana kuwajibika vya kutosha katika kubadili tabia hatarishi na kujiletea
katika vituo vya vijana vya kata na asasi wanachama wa TEYODEN.
1.3 Lengo kuu la TEYODEN
Kuchangia juhudi za kuleta maendeleo endelevu na thabiti ya tabia na mienendo ya vijana katika mahusiano yao hususani katika masuala ya ngono ili kupunguza kasi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi na kutekeleza mkakati wa kupunguza umasikini ili kufikia malengoya milenia (MDG`s)
2.0 SHUGHULI ZILIZOFANYIKA
• Katika miezi 3-(Julay -sept)ya utekelezaji, shughuli zifuatazo zilitekelezwa:

2.1 Utafiti kwa vijana juu ya uwajibikaji na ushiriki wa vijana katika shughuli za jamii na maendeleo.
TEYODEN imefanya utafiti shirikishi kuhusu uwajibikaji na ushiriki wa vijana katika vikao vya maendeleo na shughuli za kijamii na maendeleo.Utafiti huu umetokana maoni ya The Foundation For Civil kuwa ni vyema kufanya tafiti ili kujua hali ya uwajibikaji na ushiriki wa vijana kabla ya kuwasilisha tena mradi.Matokeo ya utafiti uliofanywa kwa Mukhtasari ni kama ifuatavyo:-
• 61.7% ya walengwa wa utafiti walionyesha uelewa kuhusu maana ya uwajibikaji na 38.3 % walionyesha kutoelewa maana ya uwajibikaji na dhana nzima ya uwajibikaji kwa vijana.
• 50% ya walengwa walionyesha kuwa kuna uwajibikaji hafifu kwa vijana katika mitaa na kata wanakoishi na 47% ya vijana wahojiwa walisema kuwa kuna uwajibikaji wa wastani miongoni mwa vijana katika mitaa wanayoishi.
• 85.3% ya vijana walisema hawashiriki katika vikao na shughuli za maendeleo ngazi ya kata na 14.7% tu ya vijana wanashiriki katika vikao na shughuli za kijamii na kimaendeleo ngazi ya kata.
• 73.5% vijana waliohojiwa walisema hawashiriki vikao na shughuli za kimaendeleo ngazi ya mtaa na 26.5% walisema wanashiriki katika vikao na shughuli za kimaendeleo na jamii ngazi ya mitaa.
• 67.6% ya vijana walisema hawashiriki katika shughuli za kujitolea na 32.4% za vijana walisema wanashiriki katika shughuli za kujitolea ngazi ya manispaa na kata.
• 76.5% ya vijana walisema wanashiriki katika vikao vya vijana katika vituo vya kata na 23.5% wanashiriki ipasavyo katika vikao vya vituo vya vijana vya kata.
• 76.5% ya vijana walihojiwa walisema vijana wanapaswa na ni muhimu sana kushiriki na kushirikishwa katika kufanya maamuzi ya kujamii na kimaendeleo,20.6% ni muhimu na 2.9% si muhimu sana kwa kuwa haina matokeo yoyote.
Maazimio ya vijana kutokana na utafiti huu ni kuanzisha kwa mradi au mpango maalum utakaowezesha vijana kujua umuhimu wa uwajibikaji na ushiriki wao katika shughuli za kijamii na maendeleo.Andiko la mradi limeandikwa upya na kuwasilishwa katika ofisi za Foundation.

2.2 Mradi wa uenezaji wa sera ya vijana wa Kituo cha vijana cha makangarawe.
Kituo cha vijana cha kata ya makangarawe kimeibua mradi wa kueneza sera ya vijana kwa vijana katika kata hiyo.Mradi huu umepata bahati ya kufadhiliwa na taasisi ya The Foundation For Civil Society.Mradi huu unategemewa kutekelezwa katika kipindi cha miezi 3 kuanzia mwishoni mwa Oktoba na kumalizika mwishoni mwa Disemba.

2.3 Mjadala wa vijana centre 1.
Kama ilivyo kawaida kwa vijana wa TEYODEN kufanya midahalo kila jumamosi mbili katika mwezi.katika kipindi cha taarifa vijana walifanya midahalo 6 na wastani wa vijana 107 walishiriki katika midahalo hiyo.

2.4 Mafunzo ya kujenga uwezo wa Viongozi na watendaji wa TEYODEN.
Katika kipindi cha taarifa viongozi na wanachama wa TEYODEN walipata nafasi ya kuhudhuria mafunzo ndani na nje ya mkoa wa Daresalaam kama ifutavyo:-

1.) Mafunzo ya uendelezaji wa Asasi za kiraia(Organisational Development)
Lengo la mafunzo -
Lengo la mafunzo haya ni kuinua uelewa wa wawakilishi wa asasi za kiraia kuhusu mbinu za kuendeleza asasi zao kwa kufuata mwelekeo na shughuli zenye mafanikio kwa jamii.
TEYODEN ilipata nafasi ya mwakilishi mmoja katika mafunzo haya.
2.) Ushiriki wa mweka hazina wa TEYODEN katika mafunzo ya uhasibu kwa mara ya pili hoteli ya Giraffee chini ya ufadhili wa The Foundation for Civil Society.
Lengo la mafunzo:-
Lengo la mafunzo haya ni kuwezesha wahasibu wa asasi za kiraia kuwa na uwezo wa kuendesha shughuli za mahesabu katika Asasi zao kwa uwazi na uwajibikaji.

3.) Kikao cha wadau wa elimu ya stadi za maisha kilichofanyika hoteli ya 88 mkoa wa Morogoro.
Lengo la kikao ni kupitia na kufanya marekebisho ya mwisho katika kitini cha kuwezeshea stadi za maisha kwa vijana walio nje ya shule Tanzania.
TEYODEN ilipata nafasi ya kuwakilishwa na katibu mkuu katika mkutano huo.
4.) Mafunzo ya kutengeneza sabuni ya maji.
Lengo la mafunzo ni kuwezesha vijana kuwa na uwezo wa kutengeneza sabuni ya maji ili kuinua kipato chao na kujiepusha na tabia hatarishi zinazoweza kuwapelekea katika maambukizi ya VVU.

Katika mafunzo haya vijana 12 kutoka kata ya Vituka walipata nafasi ya kushiriki.
5.) Mafunzo ya stadi za maisha yaliyofanyika ofisi ya afisa mtendaji kata changombe.

Lengo la mafunzo ni kuwezesha vijana wapatao 40 kuwa wawezeshaji wa stadi za maisha kwa vijana wenzao katika kata za Charambe,Temeke na kisarawe II.
6. Shughuli ya ufuatiliaji na usimamizi wa shughuli za vijana Manispaa ya Temeke.Katika shughuli hii taasisi za vijana 81 zilitembelewa.
2.5 Mikutano na shughuli nyingine vijana walizoshiriki.
1. Vijana 10 walishiriki katika siku ya vijana ya kimataifa katika ukumbi wa elimu ya atu wazima shughuli iliyoratibiwa na wizara ya kazi ajira na maendeleo ya vijana.
2. Ushiriki wa vijana katika vikao vya vijana ofisi za UNIC.Vijana zaidi ya 20 hushiriki katika vikao vya vijana katika kito cha habari cha umoja wa mataifa kufanya mijadala na vijana wengine nje ya Temeke.
3.Ushiriki wa vijana 4 katika mkutano wa kambi ya dunia uliofanyika kuanzia tarehe 21/7/2009 hadi 27/8/2009 katika ukumbi wa sabasaba karume hall.

3.0 KAZI ZILIZOPANGWA KUFANYIKA
3.1 TEYODEN imepanga kufanya mambo yafuatayo:-
1.) Kutekeleza mradi wa ushonaji na kudarizi kwa vijana wa kike 80 kutoka kata za Azimio,Makangarawe,Sandali na Vituka mwezi wa 12 baada ya kupata fedha kutoka ubalozi wa Ujerumani.

4.0 :HITIMISHO
TEYODEN inaamini kuwa mabadiliko kwa vijana yatakayochangia maendeleo ya vijana yanawezekana kama vijana wanapewa uzito unaostahili katika kupanga, kutekeleza, kufuatilia na kutathmini shughuli za maendeleo. Viongozi wa TEYODEN na vijana siku hadi siku wamekuwa wakiongezewa uwezo katika kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ipasavyo.Hivyo tunawashauri wadau kutumia fursa hii adimu kwa kuwatumia ili kutatua matatizo ya vijana.vijana tukijiwezesha na kuwezeshwa tunaweza.
TAARIFA YA MTANDAO WA VIJANA MANISPAA YA TEMEKE KWA KIPINDI CHA UTEKELEZAJI CHA JAN-APRILI 2010
KUTOKA: MTANDAO WA MAENDELEO YA VIJANA MANISPAA YA TEMEKE (TEYODEN)
KWENDA KWA: MKURUGENZI WA HALMASHAURI MANISPAA YA TEMEKE
1.0 UTANGULIZI
TEYODEN katika kipindi cha utekelezaji cha taarifa hii imefanikiwa kutekeleza shughuli mablimbali.Taarifa hii inalengo la kueleza shughuli zilizofanyika,mafanikio changamoto na mapendekeozo ya vijana katika kipindi cha uutekelezaji wa taaifa hii.
2.0 SHUGHULI ZILIZOFANYIKA
1.1 Mjadala wa vijana centre 1.
Kama ilivyo kawaida kwa vijana wa TEYODEN kufanya midahalo kila jumamosi mbili katika mwezi.Katika kipindi cha taarifa vijana walifanya midahalo 8 na wastani wa vijana 247 walishiriki katika midahalo hiyo.
MADA IDADI YAVIJANA MASUALA YALIYOIBULIWA MAPENDEKEZO YA VIJANA
Kilimo kwanza 42 > Uelewa mdogo wa vijana kuhusu dhana nzima ya kilimo ya kwanza.
> Suala la upatikanaji wa rasilimali ardhi lilionekana kuwa ni changamoto miongoni mwa vijana.
> Upatikanaji wa mitaji kwa ajili uanzilishi wa kilimo /ununuzi wa pembejeo. > Kuinua uelewa juu ya Kilimo Kwanza ili kuwawezesha vijana kushiriki kwa kiwango kikubwa na kuondoa umasikini .
> Kutia mkazo wa utekelezaji wa Kilimo Kwanza kwa vijana.
> Kuwawezesha vijana katika upatikanaji wa rasilimali ardhi ili waweze kushiriki katika nyanja ya Kilimo kwa ujumla.
Uanzishaji na Uendeleaji wa SACCOS 49 > Kiwango cha fedha cha kuanzisha SACCOSS kimeonekana kuwa ni kikubwa na hivyo kuwakwamisha vijana wengi kushindwa kuanzisha kuendesha SACCOS hizo. >Vijana wajitolee kwa hali na mali ili kuanzisha SACCOS itasaidia sana kwa kuwafanya kupata mitaji katika shughuli za ujasiriamali.
> Uhamasishaji na elimu zaidi ya ujasiriamali kwa vijana inahitajika ili kuwavuta vijana wasio na taarifa na elimu ya ujasiriamali.
Usawa wa kijinsia 38 > Uelewa mdogo kwa vijana juu ya usawa wa kijinsia ilionekna kuwa ni changamoto kwa vijana walio wengi. > Ili kuendana na kutekeleza yaliyokubaliwa ktika mkutano wa Beijing, elimu zaid inahitajika kwa vijana katika suala la Usawa wa Jinsia.
VVU/UKIMWI katika maendeleo ya vijana. 50 > Katika sual hili, vijana waliibua changmoto ya upanukaji na kutandaa kwa elimu sahihi ya VVU/UKIMWI hivyo kuonekana kuwa bado ni changamoto kwa vijana > Elimu, uhamasishaji na usimmizi wa uwajibikaji unahitajika zaidi ili kuleta msisitizo kwa vijana.
> Vijna wajitolee na kuunda vikundi vya uhasishaji na utoaji elimu ili kuleta msukumo wa kuondokana na tatizo na kubakiza nguvukazi ya taifa.
vijana na Uchaguzi 31 > Vijana walio wengi wameonekana kuwa nyuma katika suala zima la uchaguzi kwa uchaguzi na kuona kuwa suala hilo ni la wazee na si vijna. > Elimu na uhasishaji pamoja na fursa za vijana katika uchaguzi inahitajika zaidi ili kuleta mvuto kwa vijana na kuibua ushiriki mzuri wa vijana.
ushiriki na ushirikishawaji wa vijana kijamii na kimaendeleo 37 > Katika kujadili mada hii, suala la imani limeonekana kuwa ni changamoto kwa vijana kwa kuwa vijana wengi wameonekana hawaaminiki katika kuleta mabdiliko ya kimaendeleo katika jamii. > Vijana wapewe fursa ya kushirikishwa katika mambo ya kimaendeleo ili waoneshe imani na uwezo wao.

Katika kipindi cha utekelezajitaarifa hii viongozi wanachama na walengwa wa TEYODEN walipata nafasi ya kushiriki shughuli mbalimbali kaaifutavyo:-
1.) Mafunzo ya Stadi za amaisha kwa Vijana 72 kwa kta 24 za manispaa ya Temeke na vijana 3 kutoka kila kata kwa muda wa siku 14.
2.) Mafunzo ya sera ya vijana yaliyofanyika katika kituo cha vijana cha Makangarawe yaliyoshirikisha vijna 40, aidha mafunzo hayo yalikuwa ya siku 3.
3.) Mafunzo ya kujenga uwezo kupitia taasisi ya vijana ya Sokoine katika kata ya Somangila, mafunzo hayo yalishirikisha vijana 22 kwa siku 5.
4.) Ziara ya vituo vya vijna vya kata ili kukagua uhai wa vituo.

5.) Kupokeas ugeni kutoka wizarani.

Aidha katika shughuli zote, vijana / walengwa walipata fursa ya kuwezeshwa na kushiriki katika mambo mbalimbali ya vijana.
`
4.0 HITIMISHO
TEYODEN inaamini kuwa mabadiliko kwa vijana yatakayochangia maendeleo ya vijana yanawezekana kama vijana wanapewa uzito na fursa zinaostahili katika kupanga, kutekeleza, kufuatilia na kutathmini shughuli za maendeleo. Viongozi wa TEYODEN na vijana siku hadi siku wamekuwa wakiongezewa uwezo katika kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ipasavyo. Hivyo tunawashauri wadau kutumia fursa hii adimu kwa kuwatumia ili kutatua matatizo ya vijana.vijana tukijiwezesha na kuwezeshwa tunaweza.
2.0 SHUGHULI ZILIZOFANYIKA
• Katika miezi 3-(Julay -sept)ya utekelezaji, shughuli zifuatazo zilitekelezwa:

2.1 Utafiti kwa vijana juu ya uwajibikaji na ushiriki wa vijana katika shughuli za jamii na maendeleo.
TEYODEN imefanya utafiti shirikishi kuhusu uwajibikaji na ushiriki wa vijana katika vikao vya maendeleo na shughuli za kijamii na maendeleo.Utafiti huu umetokana maoni ya The Foundation For Civil kuwa ni vyema kufanya tafiti ili kujua hali ya uwajibikaji na ushiriki wa vijana kabla ya kuwasilisha tena mradi.Matokeo ya utafiti uliofanywa kwa Mukhtasari ni kama ifuatavyo:-
• 61.7% ya walengwa wa utafiti walionyesha uelewa kuhusu maana ya uwajibikaji na 38.3 % walionyesha kutoelewa maana ya uwajibikaji na dhana nzima ya uwajibikaji kwa vijana.
• 50% ya walengwa walionyesha kuwa kuna uwajibikaji hafifu kwa vijana katika mitaa na kata wanakoishi na 47% ya vijana wahojiwa walisema kuwa kuna uwajibikaji wa wastani miongoni mwa vijana katika mitaa wanayoishi.
• 85.3% ya vijana walisema hawashiriki katika vikao na shughuli za maendeleo ngazi ya kata na 14.7% tu ya vijana wanashiriki katika vikao na shughuli za kijamii na kimaendeleo ngazi ya kata.
• 73.5% vijana waliohojiwa walisema hawashiriki vikao na shughuli za kimaendeleo ngazi ya mtaa na 26.5% walisema wanashiriki katika vikao na shughuli za kimaendeleo na jamii ngazi ya mitaa.
• 67.6% ya vijana walisema hawashiriki katika shughuli za kujitolea na 32.4% za vijana walisema wanashiriki katika shughuli za kujitolea ngazi ya manispaa na kata.
• 76.5% ya vijana walisema wanashiriki katika vikao vya vijana katika vituo vya kata na 23.5% wanashiriki ipasavyo katika vikao vya vituo vya vijana vya kata.
• 76.5% ya vijana walihojiwa walisema vijana wanapaswa na ni muhimu sana kushiriki na kushirikishwa katika kufanya maamuzi ya kujamii na kimaendeleo,20.6% ni muhimu na 2.9% si muhimu sana kwa kuwa haina matokeo yoyote.
Maazimio ya vijana kutokana na utafiti huu ni kuanzisha kwa mradi au mpango maalum utakaowezesha vijana kujua umuhimu wa uwajibikaji na ushiriki wao katika shughuli za kijamii na maendeleo.Andiko la mradi limeandikwa upya na kuwasilishwa katika ofisi za Foundation.

2.2 Mradi wa uenezaji wa sera ya vijana wa Kituo cha vijana cha makangarawe.
Kituo cha vijana cha kata ya makangarawe kimeibua mradi wa kueneza sera ya vijana kwa vijana katika kata hiyo.Mradi huu umepata bahati ya kufadhiliwa na taasisi ya The Foundation For Civil Society.Mradi huu unategemewa kutekelezwa katika kipindi cha miezi 3 kuanzia mwishoni mwa Oktoba na kumalizika mwishoni mwa Disemba.

2.3 Mjadala wa vijana centre 1.
Kama ilivyo kawaida kwa vijana wa TEYODEN kufanya midahalo kila jumamosi mbili katika mwezi.katika kipindi cha taarifa vijana walifanya midahalo 6 na wastani wa vijana 107 walishiriki katika midahalo hiyo.
TAARIFA FUPI YA MTANDAO WA VIJANA MANISPAA YA TEMEKE KWA KIPINDI CHA UTEKELEZAJI CHA JAN –MACHI 2009.

KUTOKA: MTANDAO WA MAENDELEO YA VIJANA MANISPAA YA TEMEKE (TEYODEN)
KWENDA KWA: MKURUGENZI WA HALMASHAURI MANISPAA YA TEMEKE

1.0 UTANGULIZI
Temeke Youth Development Network (TEYODEN) ni Mtandao wa Maendeleo ya Vijana unaoendeshwa na vijana wenyewe miongoni mwa mitandao 19 iliyotokana na programu ya vijana nje ya shule iliyotekelezwa na Halmashauri 19 nchini Tanzania kwa ufadhili wa UNICEF. Mtandao umesajiriwa chini ya ofisi ya Makamu wa Raisi, namba ya usajiri ni OONGO/0170.TEYODEN inasimamia na kuratibu shughuli zake katika vituo 24 vya vijana vilivyopo katika kata 24 za Manispaa ya Temeke.

1.1 Dira ya TEYODEN
Kuwa Mtandao bora wa Maendeleo ya vijana Tanzania unaowezesha vijana kuwajibika vya kutosha katika kubadili tabia hatarishi na kujiletea maendeleo endelevu.

1.2 Dhamira ya TEYODEN
Kutoa miongozo ya utekelezaji, kusimamia na kuratibu shughuli za vijana katika vituo vya vijana vya kata na asasi wanachama wa TEYODEN.

1.3 Lengo kuu la TEYODEN
Kuchangia juhudi za kuleta maendeleo endelevu na thabiti ya tabia na mienendo ya vijana katika mahusiano yao hususani katika masuala ya ngono ili kupunguza kasi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi na kutekeleza mkakati wa kupunguza umasikini ili kufikia malengoya milenia (MDG`s)

2.0 SHUGHULI ZILIZOFANYIKA
• Katika miezi 3 ya utekelezaji, shughuli zifuatazo zilitekelezwa:

2.1 Mradi wa kujenga uwezo kwa vituo vya vijana
Katika katika utekelezaji wa shughuli za mradi:
2.1.1 Uteuzi wa watumishi wa mradi
Kabla kuanza utekelezaji wa mradi kamati ya utendaji ya TEYODEN iliteua na kuthibitisha kamati ya mradi.Swaka Abasi(Mwenyekiti) kuwa msimamizi wa mradi,Yusuph Kutegwa (katibu mtendaji)kuwa mratibu wa mradi,Gabriel Gesine(Mweka hazina) kuwa mhasibu wa mradi,Siwazuri Mussa,Zabibu Abdalah,Kaisali Mgawe na Ismail Mnikite(wajumbe) kuwa katika kamati ya ufuatiliaji na tathmini.

2.1.2 Utambulisho wa mradi
Mradi umetambulishwa tarehe 30/01/2009 kwa kufanya kikao cha wadau 28 ambao ni Mchumi wa manispaa ya Temeke, Afisa Maendeleo ya Jamii, Afisa Maendeleo ya Vijana,mratibu wa UKIMWI ambaye aliwakilishwa na Mratibu wa CSPD na maafisa watendaji 24 kutoka kata zote za Halmashauri ya Manispaa ya Temeke.
Wadau hawa walishauri kuwa ili mradi uwe endelevu, mambo yafuatayo yazingatiwe:
• Vijana wawe karibu na ofisi za kata
• Vijana wasisitizwe juu ya dhana ya kujitolea
• Vijana wasikubali kushawishiwa kisiasa
• Timu ya mradi izingatie ratiba ya kazi(mpango kazi uwe wa uhalisia),kuwe na mkakati wa kuwabana washiriki baada ya mafunzo kutekeleza majukumu yao
• TEYODEN iwezeshe upatikanaji wa vitendea kazi katika vituo vya vijana.
Pia waliahidi kutoa ushirikiano wa kutosha katika utekelezaji wa shughuli za vijana na kuwezesha kufikia malengo ya mradi yaliyokusudiwa.(Pichani kushoto)maafisa watendaji wa kata/washiriki wa utambulisho wa mradi wakiwa katika picha ya pamoja na timu ya mradi.(Picha ya kulia katikati)Afisa mtendaji wa kata ya Keko,Johnson Makaranga akitoa maoni kwa kamati ya mradi .

2.1.3 Usajiri na uhakiki wa walengwa
Shughuli hii ilifanywa kwa kuwasilisha barua kwa wenyeviti wa vituo vyote 24 vya vijana katika kata 24 za mradi iliyowataka kuteua walengwa 2 (me na ke) kuhudhuria mafunzo.Tarehe 2/2/2009 kilifanyika kikao cha pamoja kati ya kamati ya mradi na walengwa.Vijana 53 walihudhuria lakini Vigezo vya uteuzi vilitumika na kupata vijana 48, wawili kutoka kila kata kwa ajili ya mafunzo hayo.

Viongozi wa vituo vya vijana vya kata wakisubiri kupewa barua rasmi za mwaliko wa mafunzo ya kujenga uwezo baada ya kuhakikiwa na kusajiliwa.Katikati ni mwezeshaji wa mafunzo bi Caroline Damian kutoka Mtemvu Foundation.

2.1.4 Utayarishaji wa moduli ya kufundishia
Moduli moja ya kufundishia yenye sehemu nne ilitayarishwa ikiwa na mada zifuatazo:-
1. Uongozi
2. Jinsi ya uendelezaji asasi
3. Uchambuzi wa tatizo na malengo katika hatua za mzunguko wa mradi
4. Uandaaji wa malengo na shughuli za mradi
5. Utunishaji mfuko wa Asasi
6. Kujenga mahusiano na kuimarisha ushirikiano kati ya wadau (wahisani) na Asasi za kiraia
7. Ufuatiliaji na tathmini
8. Jinsi ya kukusanya takwimu na kuandika taarifa na
9. Maeneo ya ufanisi katika utekelezaji wa shughuli za vijana

2. 2.0 Mafunzo ya kujenga uwezo kwa vijana 48 kutoka vituo vya vijana 24 Manispaa ya Temeke.
Katika utekelezaji wa shughuli hii mafunzo ya siku 4 yaliendeshwa kwa vijana 48 Viongozi na watendaji kutoka vituo vya vijana 24 katika kata 24 za manispaa ya Temeke, wanafunzi 3 kutoka chuo cha Mwalimu Nyerere na mfanyakazi wa kujitolea (mjapani) wa JICA kutoka Ofisi ya Elimu ya Halmashauri ya Manispaa ya Temeke yakitanguliwa na ufunguzi na baadaye mada zilifundishwa kama ifuatavyo:

2.2.1 Ufunguzi wa mafunzo
Mafunzo yalifunguliwa na Afisa maendeleo ya jamii wa Manispaa ya Temeke tarehe 3/02/2009 na katika nasaha zake aliwataka vijana baada ya mafunzo kuboresha shughuli zao katika kata ili kurahisisha upatikanaji wa maendeleo na kupiga vita umasikini, pia aliwaeleza kuwa shughuli nyingi sasa zimeelekezwa kwa vijana kwa kuwa ni wadau muhimu wa maendeleo hivyo wahakikishe mafunzo yanafanyiwa kazi.

Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke mheshimiwa John Bwana akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kujenga uwezo wa vituo vya vijana vya kata.
• Mada zilizoendeshwa katika mafunzo ni:-
2.2.2 Uongozi
Madhumuni :-kuinua uelewa wa walengwa ili kutambua umuhimu na jinsi uongozi unavyoweza kubadili mifumo ya utekelezaji na kuruhusu maendeleo katika kata zao.

Katika mada hii walengwa walijifunza Maana, aina,majukumu ya kila kiongozi pia kubainisha aina ya uongozi unaoweza kuleta maendeleo katika vituo vyao katika kata.

2.2.3 Jinsi ya uendelezaji asasi
Madhumuni;-Kuwawezesha washiriki kujua umuhimu wa uwepo wa asasi katika jamii ili kurahisisha upatikanaji wa maendeleo.

Mada zilizofundishwa katika kipengele hiki ni:
Maana ya uendelezaji Asasi, Manufaa ya uendelezaji asasi na Jinsi ya kutatua matatizo katika asasi.

2.2.4 Uchambuzi wa tatizo na malengo katika hatua za mzunguko wa mradi
Madhumuni: Kutambua tatizo na kupanga matatizo mengine yanayochangia tatizo kuu kwa kuyaelezea kufuata uzito, pia kuweza kutengeneza ainisho la mahitaji ya mradi.
Katika mada hiyo vipengele mbalimbali vilichambuliwa kuwapa wahusika ufahamu zaidi katika mada hiyo, vifuatayo ni baadhi ya vipengele hivyo
i) Umuhimu wa kuchambua tatizo na wakati wa kubuni mradi
ii) Namna ya kufanya katika uchambuzi wa tatizo
iii) Kupanga malengo ya mradi kwa kufuata tatizo lililoibuliwa
iv) Kupanga shughuli ili kufikia matokeo
v) Kutengeneza bajeti ya mradi

2.2.5 Tathmini na ufuatiliaji
Madhumuni:-kuinua uelewa wa walengwa juu ya dhana ya ufuatiliaji na tahmini katika utekelezaji wa mradi na waweze kutofautisha vipengele hivi viwili.
Katika kipengele hiki walengwa walijifunza, maana, umuhimu na totauti za ufuatiliaji na tathmini.

2.2.6 Utunishaji mfuko wa asasi
Madhumuni:-Kuinua uelewa wa washiriki kuhusu dhana na njia za utafutaji rasilimali na fedha ili kuwezesha vituo vyao kuendesha shughuli vizuri na kwa ufanisi.
Katika mada hii walengwa walijifunza, dhana ya utunishaji mfuko, njia mbalimabli za utunishaji mfuko na mwisho walijifunza namna ya kutengeneza mpango wa kutunisha mfuko.

2.6.7 Kujenga mahusiano na kuimarisha ushirikiano kati ya wadau(wahisani) na asasi za kiraia
Madhumuni;-Kuwezesha walengwa kuwa na mbinu za kujenga mahusiano na wadau wa maendeleo katika kata zao na nje ya kata zao.
Mada zilizohusishwa katika kipengele hiki ni, Maana na aina ya wadau, uimarishaji wa mahusiano, siri kuhusu mahusiano na utafiti kuhusu wafadhili.
2.6.8 Ukusanyaji takwimu na uandishi wa taarifa
Madhumuni:-Kuwezesha washiriki kutambua njia za ukusanyaji takwimu na uandishi wa taarifa za maendeleo ya vituo vyao.
Walengwa walijifunza, jinsi ya kukusanya takwimu kwa kutumia dodoso maalum na kuandika taarifa

Katika picha kushoto washiriki wa mafunzo wakiwa darasani: kulia washiriki wakiwa katika mijadala ya vikundi kabla ya kuwasilisha.

2.6.9 Mbinu zilizotumika wakati wa mafunzo
Wawezeshaji walitumia mbinu mbalimbali ili kuwafanya walengwa kuelewa ambazo ni pamoja na :-
1.) Hotuba
2.) Majadiliano ya vikundi na uwasilishaji
3.) Maswali na majibu
4.) Bungua bongo
5.) Visa mkasa
6.) Vichangamsha mwili(Energizer)
2.10 Mkakati uliowekwa ili kuhakikisha malengo ya mafunzo yanafanikiwa.
1.) Washiriki wote baada ya mafunzo watarudi katika kata zao na kutoa mshindo nyuma (feedback) kwa maafisa watendaji na vijana wenzao.
2.) Washiriki wote baada ya mafunzo wawezeshe vijana wengine kile walichojifunza katika kata ili vijana wenzao nao waweze kupata mafunzo waliyoyapata(walengwa).
3.) Kata zote 24 ziwe zinaleta taarifa zao za utekelezaji kila baada ya miezi 3.
2.3.0 Matokeo ya mradi
2.3.1 Matokeo ya awali yaliyopangwa
1. Walengwa wa mradi wamepewa uelewa katika kuanzisha kutekeleza kufuatilia na kutathimini miradi yao.
2. Uelewa wa walengwa kuhusu uongozi bora katika vituo vya vijana vya kata umetolewa.
3. Vijana wameinua uelewa wao katika mbinu za kutumia fursa walizonazo na wameweka mikakati mipya ya kutunisha mfuko wa maendeleo ya vituo vyao.
4. Walengwa wameelewa umuhimu wa mawasiliano,mahusiano na ushirikiano baina yao na wadau wa maendeleo.
5. Vijana wanaelewa jinsi ya kukusanya takwimu na kuandika taarifa za kazi.
2.3.2 Matokeo halisi
1. Walengwa kutoka kata 16 za mradi wanaelewa dhana nzima ya kuanzisha, kutekeleza, kufuatilia na kutathmini miradi yao, hata hivyo wameshaibua miradi katika kata zao.
2. Uelewa wa vijana kuhusu uongozi umekua hasa kwa kuwa ushiriki wa vijana umeongezeka karibu katika kata 18 za mradi.vikao na wanachama wao vimeongezeka angalau kikao 1 kwa wiki.
3. Vituo 13 tayari vimeshaibua miradi(ya kiuchumi au kutoa huduma) na wameweka mikakati ya utunishaji mfuko wa vituo vyao kwa kufanya miradi ya uzalishaji mali na utoaji wa huduma.
4. Karibu vituo 17 vimeanzisha mahusiano, ushirikiano na madiwani watendaji na maafisa maendeleo wa kata husika na wameahidi kushirikiana nao bega kwa bega.
5. Walengwa katika kata zipatazo 16 wanaelewa namna ya kukusanya takwimu na kuandika taarifa.

3.0 USIMAMIZI,UFUATILIAJI NA TATHIMINI YA MRADI
3.1 Usimamizi na ufuatiliaji
Usimamizi na ufuatiliaji ulifanyika katika kipindi chote cha miezi 3 ya utekelezaji mradi.Msimamizi, mratibu na timu ya ufutiliaji ya mradi walitembelea walengwa wa mradi katika kata zote 24 za mradi Manispaa ya Temeke.Katika shughuli ya ufuatiliaji timu ya mradi na walengwa walipata nafasi ya kubadilishana mawazo.
Muhimu: Kuwashauri na kuwakumbusha walengwa kuyaweka katika vitendo yale yote waliojifunza na kubwa kabisa kuwawezesha vijana wengine katika kata kuelewa kile ambacho wao wamejifunza.

3.2 Tathmini
Mkutano wa tathmini ulifanyika tarehe 16/03/2009 ukiwajumuisha, Afisa maendeleo ya vijana Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, maafisa watendaji 6 kamati ya mradi (watu 3) na wawakilishi 13 wa vijana waliopatiwa mafunzo (jumla ya wajumbe 22).Tathimini ilifanyika kwa njia ya fomu za maswali (dodoso) kwa nia ya kupata taarifa kuhusu mradi.Matokeo yake ni kama ifuatavyo:-

3.3 Mabadiliko ya mifumo
Mradi umechangia sana katika kubadili mifumo ya zamani ya vituo vya vijana katika kata na kuleta mifumo inayofaa na itakayochochea maendeleo.

3.3.1 Uongozi
Mifumo ya uongozi hasa katika maamuzi, ushiriki na ushirikishwaji wa vijana umebadilika na sasa unaruhusu vijana wenyewe kuamua kwa pamoja mambo yao na maazimio ya vikao yanapewa kipaumbele.

3.3.2 Uibuaji wa shughuli na miradi ya kituo.
Kabla ya mradi uibuaji wa miradi na shughuli za kituo ilikuwa mikononi mwa viongozi lakini baada ya mradi wanachama katika kata wametambua umuhimu wao na wanahusika katika michakato yote ya uibuaji wa shughuli na miradi ya kituo.

3.3.3 Utafutaji rasilimali za kuendeleza kituo
Vituo vya vijana kabla ya mradi vilikuwa vinategemea sana programmu na mipango kutoka TEYODEN makao makuu lakini sasa vituo vinatambua kuwa programu zinaanzia chini kwenda juu na hii inaturahisishia kazi hasa katika kupanga mipango na miradi ya vijana.Pia vituo vipatavyo 6 vipo katika michakato ya kufungua akaunti, ambavyo ni Azimio, Miburani na Toangoma.

3.3.4 Uandishi wa taarifa
Kabla ya mradi vituo visivyozidi 4 vilikuwa vinawasilisha taarifa kwa wadau na TEYODEN makao makuu baada ya mradi vituo 14 mpaka kipindi cha taarifa vinawasilisha taarifa.Lengo ni kufikia vituo vyote 24 viwasilishe taarifa kwa wadau mbalimbali wa maendeleo.

3.3.5 Mahusiano na ushikiano na wadau wengine
Kumekuwepo na mahusiano na ushirikiano wa karibu kati ya vituo vya vijana na Taasisi za serikali na za kimataifa kama vile Ofisi za Wilaya Maafisa watendaji wa kata, TACAIDS UNICEF, UNIC na wadau wengine kama kempu za vijana na taasisi zisizo za kiserikali kama FEMINA, SAHIBA SISTERS FOUNDATION, na FHI katika kata za mradi.

3.3.6 Kutokana na michakato ya vijana kujiendesha wenyewe wadau wamerejesha imani kuwa vijana wanaweza kubuni njia za kurahisisha maendeleo ya vijana wenzao.

3.4.0 Mabadiliko ya tabia na mitazamo miongoni mwa walengwa wa mradi
3.4.1 Walengwa wameongeza kujiamini na wameongeza uwajibikaji katika kata zao.
3.4.2 Walengwa wamekuwa chachu katika kushawishi vijana wengine katika utekelezaji wa shughuli ndani na nje ya kata
3.4.3 Mahusiano yamejengeka baina ya vijana ndani ya kata lengwa za mradi
3.4.4 Vijana waliopatiwa mafunzo wana mbinu za kufanya mahusiano na wadau wengine
3.3.6 Vijana waliopatiwa mafunzo wameongeza udadisi na ufuatiliaji katika shughuli zao
3.4.8 Walengwa wamebadili mitazamo ya kutegeme TEYODEN makao makuu kwa kila kitu

4.0 CHANGAMOTO ZILIZOJITOKEZA NA JINSI ZILIVYOTATULIWA
4.1 Changamoto
• Tabia za vijana za kuomba posho kwa kila kazi wanazozifanya hata zenye manufaa ya baadae kwao.
• Ukosefu wa ofisi za kudumu kwa vijana katika vituo vya kata
• Tabia za vijana katika vituo kutegemea viongozi wao kwa kila kitu
• Tabia ya vijana kutofuatilia rasilimali zao vizuri
4.2 Jinsi tulivyokabiliana nazo
• Kamati ya mradi iliweka bayana mapema kuwa hakutakuwa na posho na vijana walielewa.
• Kamati ya mradi imeweka jambo hili bayana kwa afisa maendeleo ya vijana wa manispaa ya Temeke na Maafisa watendaji na wametoa ahadi ya kulishughulikia
• Wakati wa ufuatiliaji tulikubalina kwa pamoja na walengwa pamoja na vijana ngazi ya kata kuwa wafanye kazi kwa pamoja.

5.0 MAFUNZO KUTOKANA NA UTEKELEZAJI WA MRADI
TEYODEN kutokana na utekelezaji wa mradi wa kujenga uwezo wa vituo vya vijana vya kata imejifunza kuwa:-

• Inawezekana kutekeleza miradi na kufikia malengo yaliyotarajiwa kama walengwa (vijana) watapewa nafasi ya kushiriki katika hatua zote za mradi kuanzia kubuni, kutekeleza kufuatilia na tathmini mradi husika.
• Vijana wakijengewa uwezo katika maeneo muhimu yatakayorahisisha shughuli zao wanakuwa na nafasi kubwa ya kufanya utekelezaji kwa ufanisi.
• Kwa kuwa vijana hufanya kundi kubwa la wakazi kufikia wastani wa 60% serikali na wadau wengine wakiendesha programu za maendeleo kwao itasaidia sana katika shughuli za kupunguza umasikini.

6.0 KUJENGA MAHUSIANO NA TAASISI NYINGINE
Kutokana na kujenga mahusiano na taasisi nyingine za nje TEYODEN imefanikiwa yafutayo:
6.1 Viongozi Yusuph Kutegwa (katibu Mtendaji wa Mtandao) na Gabriel Gesine (Mweka hazina) wamehudhuria Mafunzo ya utunishaji wa mfuko yalifanyika katika hoteli ya Mbezi garden nje kidogo ya jiji la Dar es salaam na yale ya usimamizi wa fedha yalifanyika katika chuo cha MS-TCDC jijini Arusha, mafunzo yote yalifanyika kuanzia tarehe 12- 16 Januari 2009.Katika mafunzo.Kutokana na mafunzo haya kiwango cha ufanisi katika utekelezaji wa TEYODEN utaongezeka.
6.2 Zabibu abdallah katibu msaidizi wa Mtandao alihudhulia mafunzo ya kuboresha maadili ya utendaji kwa viongozi wa umma, Dodoma kwa mwaliko wa Taasisi ya watiifu Sanaa Group.
6.3 Kupitia mwaliko wa UNICEF, TEYODEN ilishiriki katika Ziara ya mke wa Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Mrs Ban ki Moon aliyetembelea ofisi za WAMA 26/2/2009

7.0 HITIMISHO
7.1 Kuhusu mradi wa kujenga uwezo
Mradi umetekelezwa kwa kundi lengwa lenye uhitaji halisi kwa kuwa utekelezaji wake umewasaidia viongozi na watendaji wa kata za mradi.Hii ni kwa sababu kwa kujenga uwezo wa viongozi na watendaji wa vituo vya vijana vya kata katika kuanzisha kutekeleza,kufuatilia, kutathimini,kutafuta rasilimali na fedha kuwa na mbinu za uongozi na kuandika taarifa za kazi zao pamoja na ufuatiliaji na usimamizi wa karibu kutoka TEYODEN makao makuu kutaufanya mtandao huu uwe shirikishi na utendaji wake uwe wa ufanisi ukubwa na hivyo kupunguza umasikini kwa vijana, jamii ya Temeke na taifa kwa ujumla.

7.2 Kwa jumla
TEYODEN imeshajengewa uwezo katika maeneo tofauti hivyo kwa sasa watendaji wake wanaweza kutumika katika maeneo tofauti ya kiutendaji hivyo wadau wawatumie vijana hawa katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya vijana wenzao na kupunguza umasikini.

TAARIFA FUPI YA MTANDAO WA VIJANA MANISPAA YA TEMEKE KWA KIPINDI CHA UTEKELEZAJI CHA JAN –MACHI 2009.

KUTOKA: MTANDAO WA MAENDELEO YA VIJANA MANISPAA YA TEMEKE (TEYODEN)
KWENDA KWA: MKURUGENZI WA HALMASHAURI MANISPAA YA TEMEKE

1.0 UTANGULIZI
Temeke Youth Development Network (TEYODEN) ni Mtandao wa Maendeleo ya Vijana unaoendeshwa na vijana wenyewe miongoni mwa mitandao 19 iliyotokana na programu ya vijana nje ya shule iliyotekelezwa na Halmashauri 19 nchini Tanzania kwa ufadhili wa UNICEF. Mtandao umesajiriwa chini ya ofisi ya Makamu wa Raisi, namba ya usajiri ni OONGO/0170.TEYODEN inasimamia na kuratibu shughuli zake katika vituo 24 vya vijana vilivyopo katika kata 24 za Manispaa ya Temeke.

1.1 Dira ya TEYODEN
Kuwa Mtandao bora wa Maendeleo ya vijana Tanzania unaowezesha vijana kuwajibika vya kutosha katika kubadili tabia hatarishi na kujiletea maendeleo endelevu.

1.2 Dhamira ya TEYODEN
Kutoa miongozo ya utekelezaji, kusimamia na kuratibu shughuli za vijana katika vituo vya vijana vya kata na asasi wanachama wa TEYODEN.

1.3 Lengo kuu la TEYODEN
Kuchangia juhudi za kuleta maendeleo endelevu na thabiti ya tabia na mienendo ya vijana katika mahusiano yao hususani katika masuala ya ngono ili kupunguza kasi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi na kutekeleza mkakati wa kupunguza umasikini ili kufikia malengoya milenia (MDG`s)

2.0 SHUGHULI ZILIZOFANYIKA
• Katika miezi 3 ya utekelezaji, shughuli zifuatazo zilitekelezwa:

2.1 Mradi wa kujenga uwezo kwa vituo vya vijana
Katika katika utekelezaji wa shughuli za mradi:
2.1.1 Uteuzi wa watumishi wa mradi
Kabla kuanza utekelezaji wa mradi kamati ya utendaji ya TEYODEN iliteua na kuthibitisha kamati ya mradi.Swaka Abasi(Mwenyekiti) kuwa msimamizi wa mradi,Yusuph Kutegwa (katibu mtendaji)kuwa mratibu wa mradi,Gabriel Gesine(Mweka hazina) kuwa mhasibu wa mradi,Siwazuri Mussa,Zabibu Abdalah,Kaisali Mgawe na Ismail Mnikite(wajumbe) kuwa katika kamati ya ufuatiliaji na tathmini.

2.1.2 Utambulisho wa mradi
Mradi umetambulishwa tarehe 30/01/2009 kwa kufanya kikao cha wadau 28 ambao ni Mchumi wa manispaa ya Temeke, Afisa Maendeleo ya Jamii, Afisa Maendeleo ya Vijana,mratibu wa UKIMWI ambaye aliwakilishwa na Mratibu wa CSPD na maafisa watendaji 24 kutoka kata zote za Halmashauri ya Manispaa ya Temeke.
Wadau hawa walishauri kuwa ili mradi uwe endelevu, mambo yafuatayo yazingatiwe:
• Vijana wawe karibu na ofisi za kata
• Vijana wasisitizwe juu ya dhana ya kujitolea
• Vijana wasikubali kushawishiwa kisiasa
• Timu ya mradi izingatie ratiba ya kazi(mpango kazi uwe wa uhalisia),kuwe na mkakati wa kuwabana washiriki baada ya mafunzo kutekeleza majukumu yao
• TEYODEN iwezeshe upatikanaji wa vitendea kazi katika vituo vya vijana.
Pia waliahidi kutoa ushirikiano wa kutosha katika utekelezaji wa shughuli za vijana na kuwezesha kufikia malengo ya mradi yaliyokusudiwa.(Pichani kushoto)maafisa watendaji wa kata/washiriki wa utambulisho wa mradi wakiwa katika picha ya pamoja na timu ya mradi.(Picha ya kulia katikati)Afisa mtendaji wa kata ya Keko,Johnson Makaranga akitoa maoni kwa kamati ya mradi .

2.1.3 Usajiri na uhakiki wa walengwa
Shughuli hii ilifanywa kwa kuwasilisha barua kwa wenyeviti wa vituo vyote 24 vya vijana katika kata 24 za mradi iliyowataka kuteua walengwa 2 (me na ke) kuhudhuria mafunzo.Tarehe 2/2/2009 kilifanyika kikao cha pamoja kati ya kamati ya mradi na walengwa.Vijana 53 walihudhuria lakini Vigezo vya uteuzi vilitumika na kupata vijana 48, wawili kutoka kila kata kwa ajili ya mafunzo hayo.

Viongozi wa vituo vya vijana vya kata wakisubiri kupewa barua rasmi za mwaliko wa mafunzo ya kujenga uwezo baada ya kuhakikiwa na kusajiliwa.Katikati ni mwezeshaji wa mafunzo bi Caroline Damian kutoka Mtemvu Foundation.

2.1.4 Utayarishaji wa moduli ya kufundishia
Moduli moja ya kufundishia yenye sehemu nne ilitayarishwa ikiwa na mada zifuatazo:-
1. Uongozi
2. Jinsi ya uendelezaji asasi
3. Uchambuzi wa tatizo na malengo katika hatua za mzunguko wa mradi
4. Uandaaji wa malengo na shughuli za mradi
5. Utunishaji mfuko wa Asasi
6. Kujenga mahusiano na kuimarisha ushirikiano kati ya wadau (wahisani) na Asasi za kiraia
7. Ufuatiliaji na tathmini
8. Jinsi ya kukusanya takwimu na kuandika taarifa na
9. Maeneo ya ufanisi katika utekelezaji wa shughuli za vijana

2. 2.0 Mafunzo ya kujenga uwezo kwa vijana 48 kutoka vituo vya vijana 24 Manispaa ya Temeke.
Katika utekelezaji wa shughuli hii mafunzo ya siku 4 yaliendeshwa kwa vijana 48 Viongozi na watendaji kutoka vituo vya vijana 24 katika kata 24 za manispaa ya Temeke, wanafunzi 3 kutoka chuo cha Mwalimu Nyerere na mfanyakazi wa kujitolea (mjapani) wa JICA kutoka Ofisi ya Elimu ya Halmashauri ya Manispaa ya Temeke yakitanguliwa na ufunguzi na baadaye mada zilifundishwa kama ifuatavyo:

2.2.1 Ufunguzi wa mafunzo
Mafunzo yalifunguliwa na Afisa maendeleo ya jamii wa Manispaa ya Temeke tarehe 3/02/2009 na katika nasaha zake aliwataka vijana baada ya mafunzo kuboresha shughuli zao katika kata ili kurahisisha upatikanaji wa maendeleo na kupiga vita umasikini, pia aliwaeleza kuwa shughuli nyingi sasa zimeelekezwa kwa vijana kwa kuwa ni wadau muhimu wa maendeleo hivyo wahakikishe mafunzo yanafanyiwa kazi.

Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke mheshimiwa John Bwana akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kujenga uwezo wa vituo vya vijana vya kata.
• Mada zilizoendeshwa katika mafunzo ni:-
2.2.2 Uongozi
Madhumuni :-kuinua uelewa wa walengwa ili kutambua umuhimu na jinsi uongozi unavyoweza kubadili mifumo ya utekelezaji na kuruhusu maendeleo katika kata zao.

Katika mada hii walengwa walijifunza Maana, aina,majukumu ya kila kiongozi pia kubainisha aina ya uongozi unaoweza kuleta maendeleo katika vituo vyao katika kata.

2.2.3 Jinsi ya uendelezaji asasi
Madhumuni;-Kuwawezesha washiriki kujua umuhimu wa uwepo wa asasi katika jamii ili kurahisisha upatikanaji wa maendeleo.

Mada zilizofundishwa katika kipengele hiki ni:
Maana ya uendelezaji Asasi, Manufaa ya uendelezaji asasi na Jinsi ya kutatua matatizo katika asasi.

2.2.4 Uchambuzi wa tatizo na malengo katika hatua za mzunguko wa mradi
Madhumuni: Kutambua tatizo na kupanga matatizo mengine yanayochangia tatizo kuu kwa kuyaelezea kufuata uzito, pia kuweza kutengeneza ainisho la mahitaji ya mradi.
Katika mada hiyo vipengele mbalimbali vilichambuliwa kuwapa wahusika ufahamu zaidi katika mada hiyo, vifuatayo ni baadhi ya vipengele hivyo
i) Umuhimu wa kuchambua tatizo na wakati wa kubuni mradi
ii) Namna ya kufanya katika uchambuzi wa tatizo
iii) Kupanga malengo ya mradi kwa kufuata tatizo lililoibuliwa
iv) Kupanga shughuli ili kufikia matokeo
v) Kutengeneza bajeti ya mradi

2.2.5 Tathmini na ufuatiliaji
Madhumuni:-kuinua uelewa wa walengwa juu ya dhana ya ufuatiliaji na tahmini katika utekelezaji wa mradi na waweze kutofautisha vipengele hivi viwili.
Katika kipengele hiki walengwa walijifunza, maana, umuhimu na totauti za ufuatiliaji na tathmini.

2.2.6 Utunishaji mfuko wa asasi
Madhumuni:-Kuinua uelewa wa washiriki kuhusu dhana na njia za utafutaji rasilimali na fedha ili kuwezesha vituo vyao kuendesha shughuli vizuri na kwa ufanisi.
Katika mada hii walengwa walijifunza, dhana ya utunishaji mfuko, njia mbalimabli za utunishaji mfuko na mwisho walijifunza namna ya kutengeneza mpango wa kutunisha mfuko.

2.6.7 Kujenga mahusiano na kuimarisha ushirikiano kati ya wadau(wahisani) na asasi za kiraia
Madhumuni;-Kuwezesha walengwa kuwa na mbinu za kujenga mahusiano na wadau wa maendeleo katika kata zao na nje ya kata zao.
Mada zilizohusishwa katika kipengele hiki ni, Maana na aina ya wadau, uimarishaji wa mahusiano, siri kuhusu mahusiano na utafiti kuhusu wafadhili.
2.6.8 Ukusanyaji takwimu na uandishi wa taarifa
Madhumuni:-Kuwezesha washiriki kutambua njia za ukusanyaji takwimu na uandishi wa taarifa za maendeleo ya vituo vyao.
Walengwa walijifunza, jinsi ya kukusanya takwimu kwa kutumia dodoso maalum na kuandika taarifa

Katika picha kushoto washiriki wa mafunzo wakiwa darasani: kulia washiriki wakiwa katika mijadala ya vikundi kabla ya kuwasilisha.

2.6.9 Mbinu zilizotumika wakati wa mafunzo
Wawezeshaji walitumia mbinu mbalimbali ili kuwafanya walengwa kuelewa ambazo ni pamoja na :-
1.) Hotuba
2.) Majadiliano ya vikundi na uwasilishaji
3.) Maswali na majibu
4.) Bungua bongo
5.) Visa mkasa
6.) Vichangamsha mwili(Energizer)
2.10 Mkakati uliowekwa ili kuhakikisha malengo ya mafunzo yanafanikiwa.
1.) Washiriki wote baada ya mafunzo watarudi katika kata zao na kutoa mshindo nyuma (feedback) kwa maafisa watendaji na vijana wenzao.
2.) Washiriki wote baada ya mafunzo wawezeshe vijana wengine kile walichojifunza katika kata ili vijana wenzao nao waweze kupata mafunzo waliyoyapata(walengwa).
3.) Kata zote 24 ziwe zinaleta taarifa zao za utekelezaji kila baada ya miezi 3.
2.3.0 Matokeo ya mradi
2.3.1 Matokeo ya awali yaliyopangwa
1. Walengwa wa mradi wamepewa uelewa katika kuanzisha kutekeleza kufuatilia na kutathimini miradi yao.
2. Uelewa wa walengwa kuhusu uongozi bora katika vituo vya vijana vya kata umetolewa.
3. Vijana wameinua uelewa wao katika mbinu za kutumia fursa walizonazo na wameweka mikakati mipya ya kutunisha mfuko wa maendeleo ya vituo vyao.
4. Walengwa wameelewa umuhimu wa mawasiliano,mahusiano na ushirikiano baina yao na wadau wa maendeleo.
5. Vijana wanaelewa jinsi ya kukusanya takwimu na kuandika taarifa za kazi.
2.3.2 Matokeo halisi
1. Walengwa kutoka kata 16 za mradi wanaelewa dhana nzima ya kuanzisha, kutekeleza, kufuatilia na kutathmini miradi yao, hata hivyo wameshaibua miradi katika kata zao.
2. Uelewa wa vijana kuhusu uongozi umekua hasa kwa kuwa ushiriki wa vijana umeongezeka karibu katika kata 18 za mradi.vikao na wanachama wao vimeongezeka angalau kikao 1 kwa wiki.
3. Vituo 13 tayari vimeshaibua miradi(ya kiuchumi au kutoa huduma) na wameweka mikakati ya utunishaji mfuko wa vituo vyao kwa kufanya miradi ya uzalishaji mali na utoaji wa huduma.
4. Karibu vituo 17 vimeanzisha mahusiano, ushirikiano na madiwani watendaji na maafisa maendeleo wa kata husika na wameahidi kushirikiana nao bega kwa bega.
5. Walengwa katika kata zipatazo 16 wanaelewa namna ya kukusanya takwimu na kuandika taarifa.

3.0 USIMAMIZI,UFUATILIAJI NA TATHIMINI YA MRADI
3.1 Usimamizi na ufuatiliaji
Usimamizi na ufuatiliaji ulifanyika katika kipindi chote cha miezi 3 ya utekelezaji mradi.Msimamizi, mratibu na timu ya ufutiliaji ya mradi walitembelea walengwa wa mradi katika kata zote 24 za mradi Manispaa ya Temeke.Katika shughuli ya ufuatiliaji timu ya mradi na walengwa walipata nafasi ya kubadilishana mawazo.
Muhimu: Kuwashauri na kuwakumbusha walengwa kuyaweka katika vitendo yale yote waliojifunza na kubwa kabisa kuwawezesha vijana wengine katika kata kuelewa kile ambacho wao wamejifunza.

3.2 Tathmini
Mkutano wa tathmini ulifanyika tarehe 16/03/2009 ukiwajumuisha, Afisa maendeleo ya vijana Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, maafisa watendaji 6 kamati ya mradi (watu 3) na wawakilishi 13 wa vijana waliopatiwa mafunzo (jumla ya wajumbe 22).Tathimini ilifanyika kwa njia ya fomu za maswali (dodoso) kwa nia ya kupata taarifa kuhusu mradi.Matokeo yake ni kama ifuatavyo:-

3.3 Mabadiliko ya mifumo
Mradi umechangia sana katika kubadili mifumo ya zamani ya vituo vya vijana katika kata na kuleta mifumo inayofaa na itakayochochea maendeleo.

3.3.1 Uongozi
Mifumo ya uongozi hasa katika maamuzi, ushiriki na ushirikishwaji wa vijana umebadilika na sasa unaruhusu vijana wenyewe kuamua kwa pamoja mambo yao na maazimio ya vikao yanapewa kipaumbele.

3.3.2 Uibuaji wa shughuli na miradi ya kituo.
Kabla ya mradi uibuaji wa miradi na shughuli za kituo ilikuwa mikononi mwa viongozi lakini baada ya mradi wanachama katika kata wametambua umuhimu wao na wanahusika katika michakato yote ya uibuaji wa shughuli na miradi ya kituo.

3.3.3 Utafutaji rasilimali za kuendeleza kituo
Vituo vya vijana kabla ya mradi vilikuwa vinategemea sana programmu na mipango kutoka TEYODEN makao makuu lakini sasa vituo vinatambua kuwa programu zinaanzia chini kwenda juu na hii inaturahisishia kazi hasa katika kupanga mipango na miradi ya vijana.Pia vituo vipatavyo 6 vipo katika michakato ya kufungua akaunti, ambavyo ni Azimio, Miburani na Toangoma.

3.3.4 Uandishi wa taarifa
Kabla ya mradi vituo visivyozidi 4 vilikuwa vinawasilisha taarifa kwa wadau na TEYODEN makao makuu baada ya mradi vituo 14 mpaka kipindi cha taarifa vinawasilisha taarifa.Lengo ni kufikia vituo vyote 24 viwasilishe taarifa kwa wadau mbalimbali wa maendeleo.

3.3.5 Mahusiano na ushikiano na wadau wengine
Kumekuwepo na mahusiano na ushirikiano wa karibu kati ya vituo vya vijana na Taasisi za serikali na za kimataifa kama vile Ofisi za Wilaya Maafisa watendaji wa kata, TACAIDS UNICEF, UNIC na wadau wengine kama kempu za vijana na taasisi zisizo za kiserikali kama FEMINA, SAHIBA SISTERS FOUNDATION, na FHI katika kata za mradi.

3.3.6 Kutokana na michakato ya vijana kujiendesha wenyewe wadau wamerejesha imani kuwa vijana wanaweza kubuni njia za kurahisisha maendeleo ya vijana wenzao.

3.4.0 Mabadiliko ya tabia na mitazamo miongoni mwa walengwa wa mradi
3.4.1 Walengwa wameongeza kujiamini na wameongeza uwajibikaji katika kata zao.
3.4.2 Walengwa wamekuwa chachu katika kushawishi vijana wengine katika utekelezaji wa shughuli ndani na nje ya kata
3.4.3 Mahusiano yamejengeka baina ya vijana ndani ya kata lengwa za mradi
3.4.4 Vijana waliopatiwa mafunzo wana mbinu za kufanya mahusiano na wadau wengine
3.3.6 Vijana waliopatiwa mafunzo wameongeza udadisi na ufuatiliaji katika shughuli zao
3.4.8 Walengwa wamebadili mitazamo ya kutegeme TEYODEN makao makuu kwa kila kitu

4.0 CHANGAMOTO ZILIZOJITOKEZA NA JINSI ZILIVYOTATULIWA
4.1 Changamoto
• Tabia za vijana za kuomba posho kwa kila kazi wanazozifanya hata zenye manufaa ya baadae kwao.
• Ukosefu wa ofisi za kudumu kwa vijana katika vituo vya kata
• Tabia za vijana katika vituo kutegemea viongozi wao kwa kila kitu
• Tabia ya vijana kutofuatilia rasilimali zao vizuri
4.2 Jinsi tulivyokabiliana nazo
• Kamati ya mradi iliweka bayana mapema kuwa hakutakuwa na posho na vijana walielewa.
• Kamati ya mradi imeweka jambo hili bayana kwa afisa maendeleo ya vijana wa manispaa ya Temeke na Maafisa watendaji na wametoa ahadi ya kulishughulikia
• Wakati wa ufuatiliaji tulikubalina kwa pamoja na walengwa pamoja na vijana ngazi ya kata kuwa wafanye kazi kwa pamoja.

5.0 MAFUNZO KUTOKANA NA UTEKELEZAJI WA MRADI
TEYODEN kutokana na utekelezaji wa mradi wa kujenga uwezo wa vituo vya vijana vya kata imejifunza kuwa:-

• Inawezekana kutekeleza miradi na kufikia malengo yaliyotarajiwa kama walengwa (vijana) watapewa nafasi ya kushiriki katika hatua zote za mradi kuanzia kubuni, kutekeleza kufuatilia na tathmini mradi husika.
• Vijana wakijengewa uwezo katika maeneo muhimu yatakayorahisisha shughuli zao wanakuwa na nafasi kubwa ya kufanya utekelezaji kwa ufanisi.
• Kwa kuwa vijana hufanya kundi kubwa la wakazi kufikia wastani wa 60% serikali na wadau wengine wakiendesha programu za maendeleo kwao itasaidia sana katika shughuli za kupunguza umasikini.

6.0 KUJENGA MAHUSIANO NA TAASISI NYINGINE
Kutokana na kujenga mahusiano na taasisi nyingine za nje TEYODEN imefanikiwa yafutayo:
6.1 Viongozi Yusuph Kutegwa (katibu Mtendaji wa Mtandao) na Gabriel Gesine (Mweka hazina) wamehudhuria Mafunzo ya utunishaji wa mfuko yalifanyika katika hoteli ya Mbezi garden nje kidogo ya jiji la Dar es salaam na yale ya usimamizi wa fedha yalifanyika katika chuo cha MS-TCDC jijini Arusha, mafunzo yote yalifanyika kuanzia tarehe 12- 16 Januari 2009.Katika mafunzo.Kutokana na mafunzo haya kiwango cha ufanisi katika utekelezaji wa TEYODEN utaongezeka.
6.2 Zabibu abdallah katibu msaidizi wa Mtandao alihudhulia mafunzo ya kuboresha maadili ya utendaji kwa viongozi wa umma, Dodoma kwa mwaliko wa Taasisi ya watiifu Sanaa Group.
6.3 Kupitia mwaliko wa UNICEF, TEYODEN ilishiriki katika Ziara ya mke wa Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Mrs Ban ki Moon aliyetembelea ofisi za WAMA 26/2/2009

7.0 HITIMISHO
7.1 Kuhusu mradi wa kujenga uwezo
Mradi umetekelezwa kwa kundi lengwa lenye uhitaji halisi kwa kuwa utekelezaji wake umewasaidia viongozi na watendaji wa kata za mradi.Hii ni kwa sababu kwa kujenga uwezo wa viongozi na watendaji wa vituo vya vijana vya kata katika kuanzisha kutekeleza,kufuatilia, kutathimini,kutafuta rasilimali na fedha kuwa na mbinu za uongozi na kuandika taarifa za kazi zao pamoja na ufuatiliaji na usimamizi wa karibu kutoka TEYODEN makao makuu kutaufanya mtandao huu uwe shirikishi na utendaji wake uwe wa ufanisi ukubwa na hivyo kupunguza umasikini kwa vijana, jamii ya Temeke na taifa kwa ujumla.

7.2 Kwa jumla
TEYODEN imeshajengewa uwezo katika maeneo tofauti hivyo kwa sasa watendaji wake wanaweza kutumika katika maeneo tofauti ya kiutendaji hivyo wadau wawatumie vijana hawa katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya vijana wenzao na kupunguza umasikini.

TAARIFA YA MTANDAO WA VIJANA MANISPAA YA TEMEKE KWA KIPINDI CHA UTEKELEZAJI CHA JAN-APRILI 2010
KUTOKA: MTANDAO WA MAENDELEO YA VIJANA MANISPAA YA TEMEKE (TEYODEN)
KWENDA KWA: MKURUGENZI WA HALMASHAURI MANISPAA YA TEMEKE
1.0 UTANGULIZI
TEYODEN katika kipindi cha utekelezaji cha taarifa hii imefanikiwa kutekeleza shughuli mablimbali.Taarifa hii inalengo la kueleza shughuli zilizofanyika,mafanikio changamoto na mapendekeozo ya vijana katika kipindi cha uutekelezaji wa taaifa hii.
2.0 SHUGHULI ZILIZOFANYIKA
1.1 Mjadala wa vijana centre 1.
Kama ilivyo kawaida kwa vijana wa TEYODEN kufanya midahalo kila jumamosi mbili katika mwezi.Katika kipindi cha taarifa vijana walifanya midahalo 8 na wastani wa vijana 247 walishiriki katika midahalo hiyo.
MADA IDADI YAVIJANA MASUALA YALIYOIBULIWA MAPENDEKEZO YA VIJANA
Kilimo kwanza 42 > Uelewa mdogo wa vijana kuhusu dhana nzima ya kilimo ya kwanza.
> Suala la upatikanaji wa rasilimali ardhi lilionekana kuwa ni changamoto miongoni mwa vijana.
> Upatikanaji wa mitaji kwa ajili uanzilishi wa kilimo /ununuzi wa pembejeo. > Kuinua uelewa juu ya Kilimo Kwanza ili kuwawezesha vijana kushiriki kwa kiwango kikubwa na kuondoa umasikini .
> Kutia mkazo wa utekelezaji wa Kilimo Kwanza kwa vijana.
> Kuwawezesha vijana katika upatikanaji wa rasilimali ardhi ili waweze kushiriki katika nyanja ya Kilimo kwa ujumla.
Uanzishaji na Uendeleaji wa SACCOS 49 > Kiwango cha fedha cha kuanzisha SACCOSS kimeonekana kuwa ni kikubwa na hivyo kuwakwamisha vijana wengi kushindwa kuanzisha kuendesha SACCOS hizo. >Vijana wajitolee kwa hali na mali ili kuanzisha SACCOS itasaidia sana kwa kuwafanya kupata mitaji katika shughuli za ujasiriamali.
> Uhamasishaji na elimu zaidi ya ujasiriamali kwa vijana inahitajika ili kuwavuta vijana wasio na taarifa na elimu ya ujasiriamali.
Usawa wa kijinsia 38 > Uelewa mdogo kwa vijana juu ya usawa wa kijinsia ilionekna kuwa ni changamoto kwa vijana walio wengi. > Ili kuendana na kutekeleza yaliyokubaliwa ktika mkutano wa Beijing, elimu zaid inahitajika kwa vijana katika suala la Usawa wa Jinsia.
VVU/UKIMWI katika maendeleo ya vijana. 50 > Katika sual hili, vijana waliibua changmoto ya upanukaji na kutandaa kwa elimu sahihi ya VVU/UKIMWI hivyo kuonekana kuwa bado ni changamoto kwa vijana > Elimu, uhamasishaji na usimmizi wa uwajibikaji unahitajika zaidi ili kuleta msisitizo kwa vijana.
> Vijna wajitolee na kuunda vikundi vya uhasishaji na utoaji elimu ili kuleta msukumo wa kuondokana na tatizo na kubakiza nguvukazi ya taifa.
vijana na Uchaguzi 31 > Vijana walio wengi wameonekana kuwa nyuma katika suala zima la uchaguzi kwa uchaguzi na kuona kuwa suala hilo ni la wazee na si vijna. > Elimu na uhasishaji pamoja na fursa za vijana katika uchaguzi inahitajika zaidi ili kuleta mvuto kwa vijana na kuibua ushiriki mzuri wa vijana.
ushiriki na ushirikishawaji wa vijana kijamii na kimaendeleo 37 > Katika kujadili mada hii, suala la imani limeonekana kuwa ni changamoto kwa vijana kwa kuwa vijana wengi wameonekana hawaaminiki katika kuleta mabdiliko ya kimaendeleo katika jamii. > Vijana wapewe fursa ya kushirikishwa katika mambo ya kimaendeleo ili waoneshe imani na uwezo wao.

Katika kipindi cha utekelezajitaarifa hii viongozi wanachama na walengwa wa TEYODEN walipata nafasi ya kushiriki shughuli mbalimbali kaaifutavyo:-
1.) Mafunzo ya Stadi za amaisha kwa Vijana 72 kwa kta 24 za manispaa ya Temeke na vijana 3 kutoka kila kata kwa muda wa siku 14.
2.) Mafunzo ya sera ya vijana yaliyofanyika katika kituo cha vijana cha Makangarawe yaliyoshirikisha vijna 40, aidha mafunzo hayo yalikuwa ya siku 3.
3.) Mafunzo ya kujenga uwezo kupitia taasisi ya vijana ya Sokoine katika kata ya Somangila, mafunzo hayo yalishirikisha vijana 22 kwa siku 5.
4.) Ziara ya vituo vya vijna vya kata ili kukagua uhai wa vituo.

5.) Kupokeas ugeni kutoka wizarani.

Aidha katika shughuli zote, vijana / walengwa walipata fursa ya kuwezeshwa na kushiriki katika mambo mbalimbali ya vijana.
`
4.0 HITIMISHO
TEYODEN inaamini kuwa mabadiliko kwa vijana yatakayochangia maendeleo ya vijana yanawezekana kama vijana wanapewa uzito na fursa zinaostahili katika kupanga, kutekeleza, kufuatilia na kutathmini shughuli za maendeleo. Viongozi wa TEYODEN na vijana siku hadi siku wamekuwa wakiongezewa uwezo katika kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ipasavyo. Hivyo tunawashauri wadau kutumia fursa hii adimu kwa kuwatumia ili kutatua matatizo ya vijana.vijana tukijiwezesha na kuwezeshwa tunaweza.

NAWASILISHA,
………………………
KATIBU MTENDAJI
TEYODEN
TEYODEN: WAAHIRISHA MDAHALO WA VIJANA LEO

Kutokana na kuwepo kwa mkutano wa vijana unaohusu changamoto zinazowakabili vijna katika shughuli za ujasiriamali ulioandaliwa na One Stop Youth Centre ( OSYC) cha Dar Es Salaam,leo TEYODEN haitakuwa na mdahalo wa vijana hadi wiki ijayo na mada itakuwa ni ileilie ilyokuwa ikiendelea wiki mbili zilizopita.Hivyo vijana wote na wadau mbalmbali mliokuwa mmealikwa kwa ajili ya kutoa ufafanuzi kuhusiana na mapambano dhidi ya ukimwi na changamoto zake mnaombwa radhi kwa usumbufu uliojitokeza.

Vijana zaidi ya 40 wa TEYODEN leo wataungana na vijana wenzao kutoka katika wilaya za Kinondoni na Ilala pale katika ukumbi wa Karimjee katika kuzijadili changamoto zinazowakabili katika suala zima la ujasiriamali ili kujikomboa kiuchumi.