Log in
Temeke Youth Development Network

Temeke Youth Development Network

Temeke/Chang'ombe, Tanzania

Parts of this page are in Swahili. Edit translations

TEYODEN yafanya ufuatiliaji katika vituo vya vijana vya kata,zoezi linalokamilisha robo ya kwanza ya mradi wa kuongeza ari ya uwajibikaji wa vijana katika shughuli

kijamii na maendeleo manispaa ya Temeke. 

TEYODEN wafanya mkutano na wadau wa maendeleo ya vijana manispaa ya Temeke

Katika kujiandaa na  utekelezaji wa mradi wa kuongeza ari ya uwajibikaji wa vijana katika ushiriki na ushirikishwaji katika shughuli za kijamii na kimaendeleo ,leo TEYODEN imeanza utekelezaji huo kwa kufanya kikao na wadau wa maendeleo ya vijana katika manispaa ya Temeke,ambapo jumla ya washiriki 26 waliotakiwa kuhudhuria kikao hicho wote walihudhuria.Kulikuwa na maafisa wanne kutoka manispaa ya Temeke,maafisa watendaji 12 kutoka kata 12 za mradi huu na maafisa maendeleo ya jamii ngazi ya kata walioalikwa miongoni mwa kata  hizo za mradi,walikuwa 4.

Mradi huu utatekelezwa katika kipindi cha miezi 12 na jumla ya shughuli 10 zitatekelezwa,ambazo ni pamoja na kikao hiki ambacho tayari kimefanyika  leo,mafunzo kwa vijana 40 kutoka katika kata 12 juu ya stadi za maisha na sera ya maendeleo ya vijana ya mwaka 2007,ufuatiliaji na ukusanyaji takwimu za matokeo ya mradi,kutengeneza majukwaa 12 ya vijana,kuendesha midahalo 4 ya vijana ambayo itaibua changamoto zinazowakabili,kufanya ufatiliaji wa  shughuli hizona ukusanyaji wa matokeo ya mradi,uanzishwaji wa kizio cha kumbukumbu(database),utengenezaji na usambazaji wa vipeperushi elimishi,uendeshaji wa matamasha 4 ya wazi(road show) juu ya ushiriki na ushirikishwaji wa vijana katika masuala ya kijamii na kimaendeleo na ufanyaji wa tathmini ambayo itafanywa na mtathmini wa nje (external evaluator).

Mradi huu utatekelezwa katika vipindi vinne yaani miezi mitatu mitatu.Mradi huu umefadhiliwa na The Foundation for Civil Society(FCS) na utagharimu shilingi milioni 35 katika kipindi chote cha utekelezaji wa mradi.

TEYODEN yaendesha mafunzo ya stadi za maisha na sera ya maendeleo ya vijana ya mwaka 2007

Katika kutekeleza mradi wa ukuongeza ari kwa vijana katika ushiriki na ushirikishwaji wa vijana katika shughuli za kijamii,TEYODEN inaendesha mafunzo ya siku sita kwa vijana wawakilishi kutoka kata 12 za mradi huu ambao umefadhiliwa na The Foundation for Civil Society wenye thamani ya shilingi miliono 35 na mradi huo utakuwa na shughuli takribani kumi za kutekelezwa katika kipindi cha mwaka mmoja.

TEYODEN wafanya mkutano na wadau wa maendeleo ya vijana manispaa ya Temeke

Katika kujiandaa na  utekelezaji wa mradi wa kuongeza ari ya uwajibikaji wa vijana katika ushiriki na ushirikishwaji katika shughuli za kijamii na kimaendeleo ,leo TEYODEN imeanza utekelezaji huo kwa kufanya kikao na wadau wa maendeleo ya vijana katika manispaa ya Temeke,ambapo jumla ya washiriki 26 waliotakiwa kuhudhuria kikao hicho wote walihudhuria.Kulikuwa na maafisa wanne kutoka manispaa ya Temeke,maafisa watendaji 12 kutoka kata 12 za mradi huu na maafisa maendeleo ya jamii ngazi ya kata walioalikwa miongoni mwa kata  hizo za mradi,walikuwa 4.

Mradi huu utatekelezwa katika kipindi cha miezi 12 na jumla ya shughuli 10 zitatekelezwa,ambazo ni pamoja na kikao hiki ambacho tayari kimefanyika  leo,mafunzo kwa vijana 40 kutoka katika kata 12 juu ya stadi za maisha na sera ya maendeleo ya vijana ya mwaka 2007,ufuatiliaji na ukusanyaji takwimu za matokeo ya mradi,kutengeneza majukwaa 12 ya vijana,kuendesha midahalo 4 ya vijana ambayo itaibua changamoto zinazowakabili,kufanya ufatiliaji wa  shughuli hizona ukusanyaji wa matokeo ya mradi,uanzishwaji wa kizio cha kumbukumbu(database),utengenezaji na usambazaji wa vipeperushi elimishi,uendeshaji wa matamasha 4 ya wazi(road show) juu ya ushiriki na ushirikishwaji wa vijana katika masuala ya kijamii na kimaendeleo na ufanyaji wa tathmini ambayo itafanywa na mtathmini wa nje (external evaluator).

 

TEYODEN yashiriki kwenye mkutano wa wadau Morogoro

Hivi karibuni ulifanyika mkutano wa awadu nwa maendeleo ya vijana pale mjini Morogor wakiupitia mkataba wa vijana wa Afrika na mkakati wa ushiriki na ushikishwaji wa vijana katika shughuli za kijamii.

Katika mkutano huo jumla ya washiriki 30 kutoka asasi za vijana na wawakilishi kutoka wizara za maendeleo ya jamii,jinsia na watto,wizara ya kilimo na wizara ya elimu na mafunzo walihudhuria mkutano huo.

Wadau waliupitia mkataba huo na kutoa mapendekezo ya kuuboresha ili uweze kuendana na mahitaji ya vijana wa kitanzania na mkakati huo pia.

TEYODEN yajiandaa kuendesha mafunzo ya uanzishaji wa VICOBA Temeke

Katika kupambana na umaskini TEYODEN itaendesha mafunzo kupitia midahalo ya kila wiki kwa vijana wake juu ya uanzishaji wa benki za kijamii,maarufu kama VICOBA.

Mafunzo hayo yataendeshwa kwa njia ya midahalo na  mwezeshaji Gabriel Gesine aliyehudhuria mafunzo ya uanzishaji wa VICOBA yaliyoendeshwa na WWF ofisi ya Tanzania pale Maili Moja,Kibaha.

Mafunzo hayo yalihusisha juu ya uanzishaji wa vikundi,uongozi katika vikundi hivyo,uchaguzi huru,kanuni  na taratibu za ununuzi wa hisa na jinsi ya kukopa,mfuko wa jamii,uundaji wa katiba ya kikundi,utunzaji wa kumbukumbu za mahesabu,ununuzi wa hisa kwa mara ya kwanza,utoaji wa mikopo,ulipaji wa mikopo na jinsi ya utunzaji wa kumbukumbu za kila siku.


 


TEYODEN KWA NA KITUO CHA VIJANA CHA MAKANGARAWE WAFANYA TAMASHA KUHADHIMISHA SIKU YA UKIMWI DUNIANI KATIKA VIWANJA VYA MAKANGARAWE.

Maneno ya utangulizi

Kwanza kabisa napenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza vijana wa kituo cha vijana cha Mangarawe. Jamani si mnajua kwamba sio rahisi sana kufanya kama wenzetu wa Makangarawe walivyofanya,basi tuwape ongera zao.Kwa kweli wamefanya kazi nzuri.Ongera bwana Ismail Mnikite.

Maadhimisho haya yalikuwa ya siku ya UKIMWI duniani huja

Kazi zilizofanyika

 

 

 

TAARIFA YA USHIRIKI KATIKA WIKI YA VIJANA NA MAADHIMISHO YA KUMBUKUMBU YA KIFO CHA MWALIMU NYERERE YALIYOFANYIKA MKOA WA KIGOMA TAREHE 8-14 OCTOBER 2010.

 1.0 UTANGULIZI

TEYODEN kila mwaka imekuwa ikipata nafasi ya kushiriki katika maadhimishomya wiki ya vijana yanayokwenda sambamba na sherehe za kuzima mwenge na siku ambayo baba wa taifa la Tanzania, mwalimu Julius Kambarage Nyerere alifariki Dunia. Wiki hii inawaleta pamoja vijana kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania katika kumuenzi baba wa taifa katika yale aliyoyahimiza kutendeka hasa katika kupiga vita ukabila na kudumisha umoja wa kitaifa hivyo basi vijana hupata nafasi ya kuonyesha kazi zao  za mikono, ujuzi wao na vilevile huduma wanazozitoa katika jamii.

 TEYODEN ilipata nafasi ya kuwakilishwa na kijana mmoja ambae ni katibu mkuu bwana YUSUPH KUTEGWA katika taarifa hii utapata nafasi ya kupata maelezo ya mchakato wa uwakilishi wa TEYODEN katika maadhimisho haya toka tarehe 8-14 Oktoba ya 2010.Pia itaonyesha mafanikio changamoto pamoja na mapendekezo ya mwakilishi ili kuboresha ushiriki wa mwakani.

2.0 MCHAKATO WA MAADHIMISHO

2.1 Malengo ya ushiriki wa TEYODEN katika maadhimisho

·        Kuonyesha shughuli za mikono za vijana wa manispaa ya Temeke hasa wanachama wa TEYODEN.\

·        Kubadilishana ujuzi na uzoefu wa jinsi ya kufanya shughuli ujasiriamali na utoaji wa huduma kwa vijana.

·        Kujenga mtandao wa kubadilishana uzoefu na kupata taarifa mpya.

2.2 Shughuli zilizofanyika

Katika maadhimisho ya mwaka huu TEYODEN ilionyesha bidhaa  zilizogawaganyika kama ifuatavyo:-

 -Bidhaa za viwanda vidogovidogo nazo zilikuwa ni,majiko ya mkaa,majalo,vifaa vya kuchotea unga dukani,mifuniko,sahani za kukaangia na vijiko vya kukaangia samaki.

 -Bidhaa za ususi na hizi zilikuwa ni vikapu vizuri vya kinamama

-Nguo pia tulionyesha ubunifu  wa nguo nzuri za kinamama na watoto zilizofumwa kwa kutumia mikono. 

TEYODEN pia ilitoa elimu kwa vipeperushi,vijarida,vitabu na uraghibishi na elimu iliyotolewa ilihusu athari za dawa za kulevya,umuhimu wa ushiriki na ushirikishwaji wa vijana na V.V.U/UKIMWI.

3.0 MAFANIKIO

Katika safari hii TEYODEN imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kama ifuatavyo:-

1.     Imefanikiwa kuuza bidhaa zake na hasa kwa kuwa ilikuwa na bidhaa kwa kina mama na watoto.

2.     Wastani wa vijana 342 walitembelea banda na kupata elimu zilizokuwa zikitolewa na kuchukua vijarida na vipeperushi ili kujisomea wakiwa nyumbani.

3.     Tulipata nafasi ya kubadilishana mawazo na uzoefu na Kigoma Youth Network,Tume ya kuthibiti dawa za kulevya,FEMINA,VETA Kigoma,Vijana wa Halmashauri ya Singida,Poverty Fighters Group na TAYOHAG

4.     Lakini pia kufika Kigoma na kutoa huduma zetu ni uzoefu ambao utakumbukwa sana.

4.0 CHANGAMOTO

Katika utekelezaji wa jambo lolote huwa hakukosi changamoto hivyo basi katika uendeshaji wa shughuli zetu Kigoma changamoto kadhaa zilijitokeza.

1.      Chakula kilikuwa ni ghali arafu mafuta ya mawese yalisababisha ugojwa kwangu kama mshiriki wa maadhimisho yale.

2.      Shughuli za uchaguzi zilidhoofisha sherehe nzima kutokana na mwitikio wa watu kuwa mdogo.

5.0 MAPENDEKEZO

Kuna mapendekezo kidogo ambayo mimi kama mshiriki ningependa kuyatoa

1.      Wizara ,Halmashauri na taasisi zinazowezesha vijana zizingatie sana kuwa katika siku muhimu kama hii ushiriki wa vijana unahitajika sana na hivyo si vyema kuhamisha ofisi nzima badala ya vijana

 6.0 HITIMISHO  

Wiki ya vijana ni muhimu sana hasa katika kukutanisha vijana na kuwafanya wawehuru kubadilishana mawazo na uzefu katika kazi zao za kila siku na kuleta ufanisi katika shughuli wnazozifanya.Kila mdau na aweke rasilimali za kutosha kuruhusu vijana kote nchini kushiriki  siku hii muhimu sana kwa Taifa letu.