Log in
Temeke Youth Development Network

Temeke Youth Development Network

Temeke/Chang'ombe, Tanzania

Parts of this page are in Swahili. Edit translations

TEYODEN yajiandaa kuendesha mafunzo ya uanzishaji wa VICOBA Temeke

Katika kupambana na umaskini TEYODEN itaendesha mafunzo kupitia midahalo ya kila wiki kwa vijana wake juu ya uanzishaji wa benki za kijamii,maarufu kama VICOBA.

Mafunzo hayo yataendeshwa kwa njia ya midahalo na  mwezeshaji Gabriel Gesine aliyehudhuria mafunzo ya uanzishaji wa VICOBA yaliyoendeshwa na WWF ofisi ya Tanzania pale Maili Moja,Kibaha.

Mafunzo hayo yalihusisha juu ya uanzishaji wa vikundi,uongozi katika vikundi hivyo,uchaguzi huru,kanuni  na taratibu za ununuzi wa hisa na jinsi ya kukopa,mfuko wa jamii,uundaji wa katiba ya kikundi,utunzaji wa kumbukumbu za mahesabu,ununuzi wa hisa kwa mara ya kwanza,utoaji wa mikopo,ulipaji wa mikopo na jinsi ya utunzaji wa kumbukumbu za kila siku.


 


TEYODEN KWA NA KITUO CHA VIJANA CHA MAKANGARAWE WAFANYA TAMASHA KUHADHIMISHA SIKU YA UKIMWI DUNIANI KATIKA VIWANJA VYA MAKANGARAWE.

Maneno ya utangulizi

Kwanza kabisa napenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza vijana wa kituo cha vijana cha Mangarawe. Jamani si mnajua kwamba sio rahisi sana kufanya kama wenzetu wa Makangarawe walivyofanya,basi tuwape ongera zao.Kwa kweli wamefanya kazi nzuri.Ongera bwana Ismail Mnikite.

Maadhimisho haya yalikuwa ya siku ya UKIMWI duniani huja

Kazi zilizofanyika

 

 

 

TAARIFA YA USHIRIKI KATIKA WIKI YA VIJANA NA MAADHIMISHO YA KUMBUKUMBU YA KIFO CHA MWALIMU NYERERE YALIYOFANYIKA MKOA WA KIGOMA TAREHE 8-14 OCTOBER 2010.

 1.0 UTANGULIZI

TEYODEN kila mwaka imekuwa ikipata nafasi ya kushiriki katika maadhimishomya wiki ya vijana yanayokwenda sambamba na sherehe za kuzima mwenge na siku ambayo baba wa taifa la Tanzania, mwalimu Julius Kambarage Nyerere alifariki Dunia. Wiki hii inawaleta pamoja vijana kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania katika kumuenzi baba wa taifa katika yale aliyoyahimiza kutendeka hasa katika kupiga vita ukabila na kudumisha umoja wa kitaifa hivyo basi vijana hupata nafasi ya kuonyesha kazi zao  za mikono, ujuzi wao na vilevile huduma wanazozitoa katika jamii.

 TEYODEN ilipata nafasi ya kuwakilishwa na kijana mmoja ambae ni katibu mkuu bwana YUSUPH KUTEGWA katika taarifa hii utapata nafasi ya kupata maelezo ya mchakato wa uwakilishi wa TEYODEN katika maadhimisho haya toka tarehe 8-14 Oktoba ya 2010.Pia itaonyesha mafanikio changamoto pamoja na mapendekezo ya mwakilishi ili kuboresha ushiriki wa mwakani.

2.0 MCHAKATO WA MAADHIMISHO

2.1 Malengo ya ushiriki wa TEYODEN katika maadhimisho

·        Kuonyesha shughuli za mikono za vijana wa manispaa ya Temeke hasa wanachama wa TEYODEN.\

·        Kubadilishana ujuzi na uzoefu wa jinsi ya kufanya shughuli ujasiriamali na utoaji wa huduma kwa vijana.

·        Kujenga mtandao wa kubadilishana uzoefu na kupata taarifa mpya.

2.2 Shughuli zilizofanyika

Katika maadhimisho ya mwaka huu TEYODEN ilionyesha bidhaa  zilizogawaganyika kama ifuatavyo:-

 -Bidhaa za viwanda vidogovidogo nazo zilikuwa ni,majiko ya mkaa,majalo,vifaa vya kuchotea unga dukani,mifuniko,sahani za kukaangia na vijiko vya kukaangia samaki.

 -Bidhaa za ususi na hizi zilikuwa ni vikapu vizuri vya kinamama

-Nguo pia tulionyesha ubunifu  wa nguo nzuri za kinamama na watoto zilizofumwa kwa kutumia mikono. 

TEYODEN pia ilitoa elimu kwa vipeperushi,vijarida,vitabu na uraghibishi na elimu iliyotolewa ilihusu athari za dawa za kulevya,umuhimu wa ushiriki na ushirikishwaji wa vijana na V.V.U/UKIMWI.

3.0 MAFANIKIO

Katika safari hii TEYODEN imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kama ifuatavyo:-

1.     Imefanikiwa kuuza bidhaa zake na hasa kwa kuwa ilikuwa na bidhaa kwa kina mama na watoto.

2.     Wastani wa vijana 342 walitembelea banda na kupata elimu zilizokuwa zikitolewa na kuchukua vijarida na vipeperushi ili kujisomea wakiwa nyumbani.

3.     Tulipata nafasi ya kubadilishana mawazo na uzoefu na Kigoma Youth Network,Tume ya kuthibiti dawa za kulevya,FEMINA,VETA Kigoma,Vijana wa Halmashauri ya Singida,Poverty Fighters Group na TAYOHAG

4.     Lakini pia kufika Kigoma na kutoa huduma zetu ni uzoefu ambao utakumbukwa sana.

4.0 CHANGAMOTO

Katika utekelezaji wa jambo lolote huwa hakukosi changamoto hivyo basi katika uendeshaji wa shughuli zetu Kigoma changamoto kadhaa zilijitokeza.

1.      Chakula kilikuwa ni ghali arafu mafuta ya mawese yalisababisha ugojwa kwangu kama mshiriki wa maadhimisho yale.

2.      Shughuli za uchaguzi zilidhoofisha sherehe nzima kutokana na mwitikio wa watu kuwa mdogo.

5.0 MAPENDEKEZO

Kuna mapendekezo kidogo ambayo mimi kama mshiriki ningependa kuyatoa

1.      Wizara ,Halmashauri na taasisi zinazowezesha vijana zizingatie sana kuwa katika siku muhimu kama hii ushiriki wa vijana unahitajika sana na hivyo si vyema kuhamisha ofisi nzima badala ya vijana

 6.0 HITIMISHO  

Wiki ya vijana ni muhimu sana hasa katika kukutanisha vijana na kuwafanya wawehuru kubadilishana mawazo na uzefu katika kazi zao za kila siku na kuleta ufanisi katika shughuli wnazozifanya.Kila mdau na aweke rasilimali za kutosha kuruhusu vijana kote nchini kushiriki  siku hii muhimu sana kwa Taifa letu.      

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

    

TEYODEN na TYVA waongeza nafasi za ushirikiano

TEYODEN na Tanzania Youth Vision Association(TYVA),leo walifanya mkutano wa kuzindua ajenda ya vijana 2010,wakishirikisha asasi nyingine za vijana katika ukumbi wa Karimjee leo ambapo mada ilwasilishwa na mkurugenzi wa hakielimu,Bibi Annastazia Rugaba ambaye pia alibainsha changamoto zinazowakabili vijana kuelekea uchaguzi mkuu na katika harakati za kujikomboa kiuchumi,kisiasa na kiafya.

Kisha baada ya mawasilisho hayo,vijana walipata nafasi ya kufanya majadiliano yaliyopelekea kuwepo kwa maazimio ambayo baadaye yatapelekwa kwa makatibu wa vyama vya siasa nchini,yakipendekeza nini kifanyike kwa ajili ya vijana,mara chama chochote kitakachoingia madarakani kitapaswa kiyafanyie kazi.

Katika mojawapo ya maazimio hayo ni kuhusu kuwepo kwa ufuatiliaji wa mapendekezo hayo hata baada ya uchaguzi kwa wale waliochaguliwa.

 

 

 

 

 

 

TEYODEN washiriki katika siku ya vijana kimataifa Agosti 12

Katika kuendeleza sera yake ya ushirikiano na mashirika mengine ya vijana TEYODEN ilishiriki katika maadhimisho na shirika la vijana la Umoja wa Mataifa (YUNA) kaika kuadhimisha siku ya vijana kimataifa.Maadhimisho hayo yalifanyika katika ukumbi wa Apeadu  unaomilkiwa na Umoja wa Mataifa.

Siku hiyo ya vijana ilienda sanjatri na uzinduzi wa mwaka kijana uliozinduliwa na wazirti wa kazi,Ajira na maendeleo ya vijana,mheshimiwa Al-Haji Juma Athuman Kapuya,ambapo alibainisha changamoto zinazowakabili viaja katika ajira kuwa ni pamoja na kutokuwa waaminfu pale wanapopata ajira,kutofanya kazi kwa kujituma,uadilifu katika maeneo ya kazi na kukosa ujzi unaopelekea kutokujiamini wakati wanapokuwa kwenye usaili wakazi.

Kauli mbiu ya mwaka huu ilikuwa ni "mwaka wetu,Sauti yetu", iliyokuwa na kchwa cha habari,"Majdiliano na makubaliano ya pamoja".

 

 

 

 

 

Kamati ya Utendaji TEYODEN yajipanga kutekeleza mradi wa Utetezi wa Mabinti wanaofanya kazi kwenye baa

Katika ile hali ya kuwajali wasichana wanaofanya kazi kwenye baa mbalimbali hapa jijini Dar Es Salaam,TEYODEN imeonelea ni vema ikajitahidi kuwatafutia suluhu ya maonevu wanayofanyiwa na wamiliki wa baa.

Katika kikao cha kamati ya utendaji kilichofanyika jumamosi ya tarehe 12 Juni 2010 katika ofisi za TEYODEN,kikihudhuriwa na mwakilishi kutoka Taasisi ya Maendeleo Shirikishi kwa vijana Arusha ( TAMASHA) yenye makao yake makuu katika jiji la Arusha,kaka Churchill Winston ambao ndio watakaokuwa wafadhili wa mradi huo na TEYODEN wakiwa ni wataalamu watafanya utafiti katika kata nne za manispaa ya Temeke ambazo ni Kurasini,Azimio, Keko na Mbagala katka baa zote zilizopo katika katika kata hizo ili kbaini ni changamoto zipi wanazokabiliana nazo mabinti hawa na jinsi ya kuzitatua wakiwashirikisha wamiliki wa baa hizo,wadau wa maendeleo katika manispaa ya Temeke na vijana mbalimbali.

Kabla ya kuingia katika mchakato huu kwanza yatakuwepo mafunzo ya namna ya kufanya utafiti huo.Mradi huo utakuwa ni wa mwaka mmoja.Kinachosubiriwa kwa sasa ni kibali kutoka wizara ya Sayansi naTeknolojia ambacho huenda kinatarajiwa kupatikana ndani ya mwezi huu.

TEYODEN itaendelea kushirikiana na mashirika mengine ikiwa ni katika kuimarisha mahusiano yake na asasi nyingine ndani na nje ya nchi.
TAARIFA YA MTANDAO WA VIJANA MANISPAA YA TEMEKE KWA KIPINDI CHA UTEKELEZAJI CHA MEI JUNI 2009.

KUTOKA: MTANDAO WA MAENDELEO YA VIJANA MANISPAA YA TEMEKE (TEYODEN)
KWENDA KWA: MKURUGENZI WA HALMASHAURI MANISPAA YA TEMEKE

1.0 UTANGULIZI
Temeke Youth Development Network (TEYODEN) ni Mtandao wa Maendeleo ya Vijana unaoendeshwa na vijana wenyewe miongoni mwa mitandao 19 iliyotokana na programu ya vijana nje ya shule iliyotekelezwa na Halmashauri 19 nchini Tanzania kwa ufadhili wa UNICEF. Mtandao umesajiriwa chini ya ofisi ya Makamu wa Raisi, namba ya usajiri ni OONGO/0170.TEYODEN inasimamia na kuratibu shughuli zake katika vituo 24 vya vijana vilivyopo katika kata 24 za Manispaa ya Temeke.

1.1 Dira ya TEYODEN
Kuwa Mtandao bora wa Maendeleo ya vijana Tanzania unaowezesha vijana kuwajibika vya kutosha katika kubadili tabia hatarishi na kujiletea
katika vituo vya vijana vya kata na asasi wanachama wa TEYODEN.

1.3 Lengo kuu la TEYODEN
Kuchangia juhudi za kuleta maendeleo endelevu na thabiti ya tabia na mienendo ya vijana katika mahusiano yao hususani katika masuala ya ngono ili kupunguza kasi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi na kutekeleza mkakati wa kupunguza umasikini ili kufikia malengoya milenia (MDG`s)

2.0 SHUGHULI ZILIZOFANYIKA
• Katika miezi 3-(Julay -sept)ya utekelezaji, shughuli zifuatazo zilitekelezwa:

2.1 Ufuatiliaji wa shughuli za vijana baada ya mafunzo ya kujenga uwezo
Baada ya mchakato wa mafunzo ya kujenga uwezo vijana wawakilishi walirudi katika kata zao na kufanya utekelezaji katika kata zao.
Katika ziara ya ufuatiliaji wa matokeo makuu ya mradi (project impact) mambo yafuatayo yalijitokeza
Vijana wanaendeleza matunda ya mradi kwa kuendeleza dhana ya kujitegemea mfano kata ya Vituka, Charambe, Azimio na miburani wapo katika michakato ya kufungua akaunti japo kuwa benki zinamasharti magumu kwa vikundi vidogo vya kijamii.

2.2 Uibuaji wa mradi wa kuamsha ari ya uwajibikaji na ushiriki wa vijana katika masuala ya kijamii na kimaendeleo.
Katika kipindi cha utekelezaji wa taarifa idara ya tafiti na takwimu iliendesha vikao 4 vya vijana vya kuibua mradi wa kiwango cha kati na kuuwasilisha The Foundation for civil society kwaajili ya maamuzi ya kupatiwa fedha.mradi huu unajulikana kama kuongeza ari ya uwajibikaji kwa vijana katika shughuli za kijamii na maendeleo manispaa ya Temeke.

2.3 Mjadala wa vijana centre 1
Kama ilivyo kawaida kwa vijana wa TEYODEN kufanya midahalo kila jumamosi mbili katika mwezi.katika kipindi cha taarifa vijana walifanya midahalo 6 na wastani wa vijana 120 walishiriki katika midahalo hiyo.

2.4 Mafunzo ya kujenga uwezo wa watendaji wa TEYODEN.

Katika kipindi cha taarifa viongozi na wanachama wa TEYODEN walipata nafasi ya kuhudhuria mafunzo ndani na nje ya mkoa wa Daresalaam kama ifutavyo:-

Ushiriki wa vijana 30 katika mafunzo ya ujasiriamali ukumbi wa vijana centre ilala
Lengo la mafunzo -
Lengo la mafunzo haya ni kuinua uelewa wa vijana katika stadi za ujasiriamali ili kukuza biashara zao na kujiepusha na makundi rika na kuondoa uamsikini miongoni mwao.

Ushiriki wa vijana 30 katika mafunzo ya ujasiriamali yaliyoandaliwa na Safer Cities kupitia Sustainability Cities.yalioyofanyika katika ukumbi wa karimjee.
Lengo la mafunzo -
Lengo la mafunzo haya ni kuinua uelewa wa vijana katika stadi za ujasiriamali ili kukuza biashara zao na kujiepusha na makundi rika na kuondoa uamsikini miongoni mwao.

Ushiriki wa mweka hazina wa TEYODEN katika mafunzo ya uhasibu MTCDC chini ya ufadhili wa The Foundation for Civil Society.
Lengo la mafunzo:-
Lengo la mafunzo haya ni kuwezesha washiriki kuwa na uwezo wa washriki kuendesha shughuli za mahesabu katika Asasi zao kwa uwazi na uwajibikaji.

Ushriki wa mwakilishi mmoja kutoka TEYODEN katika mafunzo ya ushiriki na ushirikishwaji wa vijana katika shughuli za kijamii mafunzo yaliyofanyikia morogoro.
Lengo la mafunzo:-
Lengo la mafunzo haya ni kuwezesha washiriki kujua haki na wajibu wa jamii kushiriki katika shughuli za kijamii na kuwa wawezeshaji kwa vijana wengine

Ushiriki wa mwakilishi mmoja wa TEYODEN katika mafunzo ya mbinu za kutunisha mfuko wa asasi yaliyofanyika mbezi garden jijini Daresalaam kwa ufadhili wa The Foundation For Civil Society.

2.5 Ushiriki wa mwakilishi mmoja wa TEYODEN katika safari ya upandaji mlima iliyoandaliwa na Kilimanjaro initiative kupitia Safer Cities.

2.6 Uandishi na uwakilishi wa Andiko la miradi kwa wafadhili
TEYODEN katika kipindi cha utekelezaji wa taarifa hii imeibua kutayarisha na kuwasilisha maombi yafutayo ya fedha:-

-Mradi wa uchimbaji wa kisima cha umwagiliaji katika kambi ya vijana ya Somangira. Mradi huu umewasilisha katika ubalozi wa ujerumani.

- Mradi wa kudarizi na ushonaji kwa vijana wa kike walio nje ya shule 80 kutoka kata 5 za Azimio, Makangarawe, Sandali, Vituka na Tandika.Mradi huu umewasilishwa katika ofisi za ubalozi wa Ujerumani.

3.0 KAZI ZILIZOPANGWA KUFANYIKA
3.1 TEYODEN imepanga kufanya mambo yafuatayo:-

-Kufanya uhamasishaji kwa vijana kuhusu uibuaji wa vijana na watoto wanaofanyiwa ukatili.

-Uhamasishaji kwa vijana katika ushiriki wa nane nane ngazi ya wilaya na ngazi kanda.

-Uhamasishaji wa vijana katika ushiriki wa mkutano wa kambi ya dunia utakaofanyika kuanzia tarehe 21/7/2009 hadi 27/8/2009 katika ukumbi wa sabasaba karume hall.

-Ushiriki wa vijana katika shughuli za uvuvi katika pwani ya bahari ya hindi maeneo ya vijibweni.

4.0 :HITIMISHO
TEYODEN inaamini kuwa mabadiliko kwa vijana yatakayochangia maendeleo ya vijana yanawezekana kama vijana wanapewa uzito unaostahili katika kupanga, kutekeleza, kufuatilia na kutathmini shughuli zinazowahusu. Viongozi wa TEYODEN na vijana siku hadi siku wamekuwa wakiongezewa uwezo katika kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ipasavyo.Hivyo tunawashauri wadau kutumia fursa hii adimu kwa kuwatumia ili kutatua matatizo ya vijana yanayowakabili .
TAARIFA YA MTANDAO WA VIJANA MANISPAA YA TEMEKE KWA KIPINDI CHA UTEKELEZAJI CHA OKT-DES 2009.

KUTOKA: MTANDAO WA MAENDELEO YA VIJANA MANISPAA YA TEMEKE (TEYODEN)
KWENDA KWA: MKURUGENZI WA HALMASHAURI MANISPAA YA TEMEKE

1.0 UTANGULIZI
Temeke Youth Development Network (TEYODEN) ni Mtandao wa Maendeleo ya Vijana unaoendeshwa na vijana wenyewe miongoni mwa mitandao 19 iliyotokana na programu ya vijana nje ya shule iliyotekelezwa na Halmashauri 19 nchini Tanzania kwa ufadhili wa UNICEF. Mtandao umesajiriwa chini ya ofisi ya Makamu wa Raisi, namba ya usajiri ni OONGO/0170.TEYODEN inasimamia na kuratibu shughuli zake katika vituo 24 vya vijana vilivyopo katika kata 24 za Manispaa ya Temeke.
1.1 Dira ya TEYODEN
Kuwa Mtandao bora wa Maendeleo ya vijana Tanzania unaowezesha vijana kuwajibika vya kutosha katika kubadili tabia hatarishi na kujiletea
katika vituo vya vijana vya kata na asasi wanachama wa TEYODEN.
1.3 Lengo kuu la TEYODEN
Kuchangia juhudi za kuleta maendeleo endelevu na thabiti ya tabia na mienendo ya vijana katika mahusiano yao hususani katika masuala ya ngono ili kupunguza kasi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi na kutekeleza mkakati wa kupunguza umasikini ili kufikia malengoya milenia (MDG`s)
2.0 SHUGHULI ZILIZOFANYIKA
• Katika miezi 3-(OKT-DES)ya utekelezaji, shughuli zifuatazo zilitekelezwa:

2.1 Ushiriki wa vijana siku ya UKIMWI duniani tarehe 1/12/2009.
Vijana takribani 300 walishiriki katika maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani .TEYODEN ilipata nafasi ya banda kuonyesha shughuli zake.Shughuli zilizoonyeshwa ni pamoja habari na stadi za maisha ambazo ni muhimu katika kufanya mabadiliko kwa vijana na kujiepusha na maambukizi ya VVU na UKIMWI.

2.2 Ushiriki wa vijana wiki ya vijana tarehe 14/10/2009
Vijana walipata nafasi ya kushiriki katika maadhimisho ya wiki ya vijana ambapo shughuli za msingi katika siku hii ilikuwa ni kuwasisitiza vijana kujiepusha na maambukizi kupima na kujua afya zao.Jumbe mbalimbali kuhusu UKIMWI zilitolewa kupitia ngoma maigizo na muziki wa kizazi kipya.

2.3 Mjadala wa vijana centre 1.
Kama ilivyo kawaida kwa vijana wa TEYODEN kufanya midahalo kila jumamosi mbili katika mwezi.katika kipindi cha taarifa vijana walifanya midahalo 4 na wastani wa vijana 96 walishiriki katika midahalo hiyo.

2.4 Vikao mikutanona warsha za kuoneza uwezo wa vijana na watendaji wa TEYODEN.
Katika kipindi chautekelezajitaarifa hii viongozi wanachama na walengwa wa TEYODEN walipata nafasi ya kushiriki shughuli mbalimbali kaaifutavyo:-

1.) Kiongozi mmoja(katibu) kutoka TEYODEN alipata nafasi ya kushiriki katika kikao cha wadau cha kupitia moduli ya stadi za maisha( 29/12/2009-1/1/2010) iliyofanyiwa marekebisho ya mwisho kabla ya kupigwa chapa na kuanza kutumika.Katika hiki yaliangaliwa mapungufu ya oduli hiyo ili kuendena sawa na mkabala wa stadi za maisha.

2.5kufanya matamasha 3 kwa ushirikiano wa asasi ya FEMINA
TEYODEN kwa kushrikiana na asasi FEMA tulifanikiwa kuendesha matamasha 3 katika kata za Somangila, Mbagala na Azimio.

1.) Lengo la matamasha haya lilikuwa ni:-
Kuwezesha vijana wengi zaidi katika kata zilizopendekezwa kupata nafasi ya kutafakari kwa kina shughuli za ujasiriali ni jinsi zinavyoweza kumuepusha na maambukizim ya V.V.U na UKIMWI.
2.) Shughuli na zilizotumika katika matamasaha hayo:-
Shughuli za maigizo ngoma na muziki wa kizazi kipya

3.) Mafanikio
Vijana walipata nafasi ya kipekee katika kutafakari VVU na UKIMWI na jinsi ya kujiepusha nazo kwa njia ya kujishughulisha na shughuliza uzalishaji mali.Takribani vijana 1500 walijitokeza katika matamasha hayo.

3.0 KAZI ZILIZOPANGWA KUFANYIKA MWAKA 2010
3.1 TEYODEN imepanga kufanya shughuli zifuatazo katika mwaka 2010
1.) Kutekeleza mradi wa kuamsha ari uwajibikaji na ushiriki wa vijana katika shughuli za maendeleo na za kijamii.

4.0 HITIMISHO
TEYODEN inaamini kuwa mabadiliko kwa vijana yatakayochangia maendeleo ya vijana yanawezekana kama vijana wanapewa uzito unaostahili katika kupanga, kutekeleza, kufuatilia na kutathmini shughuli za maendeleo. Viongozi wa TEYODEN na vijana siku hadi siku wamekuwa wakiongezewa uwezo katika kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ipasavyo.Hivyo tunawashauri wadau kutumia fursa hii adimu kwa kuwatumia ili kutatua matatizo ya vijana.vijana tukijiwezesha na kuwezeshwa tunaweza.