Log in
Tanzania Educational Motivation Alliance-TEMOA

Tanzania Educational Motivation Alliance-TEMOA

Kyela, Tanzania

Parts of this page are in Swahili. Edit translations

TEMOA ni shirika lisilo la kiserikali lililosajiliwa nchini Tanzania kufanya kazi za kiraia chini ya sheria ya mashirika yasiyo ya kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002. shirika lilisajiliwa na mamlaka inayohusika na usajili wa mashirika yasiyo ya kiserikali yaani wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia na watoto tar 08/12/2014 na kupewa namba ya usajiliĀ 00NGO/00007662. Temoa ilianzishwa mwezi wa tatu mwaka 2014 na kikundi cha vijana kwa lengo la kuhamasisha maendeleo ya elimu wilayani kyela. kabla haijawa temoa, ilikuwa na jina la awali ambalo lilikuwa ni academic talented tenth association (ACTTA) ambalo kupitia mijadala halali ya vikao vya kikundi wakati huo kabla hakijapata usajili ilipendekezwa vinginevyo na hivy kuwa Tanzania Educational Motivation Alliance yaani (TEMOA). Sababu za mabadiliko haya zilikuwa nyingi na kubwa zaidi ililkuwa ni kubadilika kwa eneo la kufanyia kazi (area of operation) ambapo sasa badala ya kuwa asasi ya kiwilaya ilikubaliwa kuwa tufanye kazi nchi nzima ya tanzania bara.

Mpaka kufika mwaka 2015 shirika limekua kwa kiasi kikubwa hadi kupata uongozi wake ambapo shirika linaongozwa na kamati tendaji (executive committee) yenye viongozi watano ambao ni:-

1) mwenyekiti wa shirika-Mr.Benedict M bageni

2) katibu mkuu wa shirika-Mr. Festo Moses M

3) Mhazini wa shirika-Mr. Dominic Andongolile M

4) Makamu mwenyekiti- Mr. Wiliam Mnyehe

5) Naibu katibu mkuu- Mr. Alinanuswe Wiliam

MIPANGO YA SHIRIKA

Shirika liko katika zoezi la kuandaa mpango mkakati (Strategic plan) wa kuutekeleza kuanzia mwaka huu wa fedha. mpango huo utakuwa na mambo kadha wa kadha ambayo shirika linapanga kutekeleza ifikapo mwaka 2018. ni mpango wa miaka mitatu (3).

Aidha shirika linaendelea na mipango yake ya muda mfupi ambayo ilijiwekea kuanzia pale lilipoanzishwa. shughuli ambazo shirika linaendelea nazo ni pamoja na:-

1) kufanya utafiti juu ya ushiriki wa wazazi katika maendeleo ya elimu nchini tanzania. hii ni study iliyopangwa kufanyika kuanzia mwezi sept mwaka jana lakini zoezi lilishindwa kukamilika kufuatia changamoto ya fedha na hivyo lilisimamishwa katika hatua ya ukusanyaji wa taarifa kutoka kwa jamii. Shirika linaendelea kutafuta vyanzo vya fedha ili kufanikisha zoezi hili muhimu sana kwa shughuli za shirika kwani ndilo litakalotoa picha halisi ya ukubwa wa tatizo lenyewe la kukosekana kwa hamasa ya wazazi katika maendeleo ya elimu nchini. Zoezi hili linafanyika katika wilaya mbili za kyela na busokelo.

2) kuandaa project ya uhamasishaji na uelimishaji wa wanafunzi juu ya umuhimu wa elimu katika wilaya ya kyela. Peoject hii itakwenda kwa jina la Kyela Academic Champions Awards na ipo mbioni kuanza kwani pendekezo lake limekamilika na kinachofuata sasa ni kutafutia pesa kwa ajili ya utekelezaji wake.

3) kutafuta ofisi ya makao makuu ya shirika ambayo yatakuwa hapa wilayani kyela. na hili linategemea sana upatikanaji wa fedha za uedeshaji.

4) Kuandaa na kutekeleza mradi wa uelimishaji wa jamii juu ya umuhimu wa elimu katika jamii za vijijini utakaokwenda kwa jina la "MZAZI KAMA MDAU WA ELIMU, SHIRIKI KATIKA ELIMU" mradi huu utatekelezwa katika maeneo ya vijijini zaidi ikiwa na lengo la kuwaelimisha wazazi na wanajamii wote kushiriki katika kumsimamia mtoto kielimu.

IMANI YA SHIRIKA

Shirika linaamini kuwa ukosefu wa elimu ndicho chanzo kikuu cha matatizo katika jamii ikiwemo umasikini na uhalifu kama vile wizi, ujambazi, na kuporomoka kwa maadili katika jamii yetu. tunaamini pia kuwa kulalamika sana hakuwezi kuondoa matatizo tuliyonayo bali kuthubutu kwa vitendo ndio njia pekee ya kujikomboa. Mwisho shirika linaimani kubwa na kundi la vijana katika kuleta maendeleo katika jamii katika nyanja zote ikiwemo uchumi, utamaduni, kijamii na kisiasa. vijana ndio tegemeo la wazee na watoto duniani kote.