Log in
YOUTH EDUCATION THROUGH SPORTS TANZANIA

YOUTH EDUCATION THROUGH SPORTS TANZANIA

Mbeya , Tanzania

Parts of this page are in Swahili. Edit translations

Madarasa ya elimu ya awali bado kizungumkuti 

Hili ni darasa la awali lililopo katika kijiji cha Mkali B, kilichopo wilaya ya Nyasa, mkoani Ruvuma. 




SERIKALI imefanya kosa kubwa la kiufundi kuhusu uamuzi wake wa kuanzisha madarasa ya elimu ya awali katika shule za msingi nchini.

Kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Serikali iliagiza kila shule ya msingi kuwa na darasa la elimu ya awali, lakini ikasahau kuziwezesha shule hizo kirasiliamali na hata kutoa mwongozo wa uendeshaji wake.

Jukumu hilo sasa liko chini ya wazazi wenyewe kupitia kamati za shule na walimu wakuu wa shule za msingi.

Uchunguzi wa hivi karibuni wa  Mwananchi katika shule za kata ya Liuli iliyopo wilaya ya Nyasa, mkoani Ruvuma, umebaini kuwapo kwa mazingira ya kusikitisha katika yanayoitwa madarasa ya elimu ya awali.

Hata walimu wanaofundisha watoto hao ni wa kuokota, huku wakiwa hawana mafunzo maalumu ya ualimu kwa watoto. Baadhi ya walimu ni vijana waliohitimu kidato cha nne  na kupata daraja sifuri.

Hawa ndio watu waliokabidhiwa jukumu la kuwapika watoto kwa minajili ya kuwaandaa kuingia darasa la kwanza.

Wadau wa elimu wanasema bado Serikali haijaipa elimu hiyo msukumo unaostahiki kama inavyofanya katika madaraja ya elimu ya msingi, sekondari, elimu ya juu na ufundi.

Kwa mfano, mdau wa elimu na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mkali iliyopo wilayani Nyasa, Erasmus Haule, anasema bado Serikali haijatangaza elimu hiyo kuwa ni ya lazima, jambo linalosababisha wazazi kutohamasika kusomesha watoto wao katika madarasa ya elimu ya awali.

‘’Hakuna sheria inayowabana wazazi kupeleka watoto katika shule za awali. Kuna siasa hapo na ndio inayofanya elimu hii ikose nguvu,’’anasema.

Aidha, kwa sababu ya Serikali kutojiingiza moja kwa moja katika uendeshaji wa elimu hiyo kama ilivyo katika madaraja mengine ya elimu, wazazi wamebebeshwa mzigo wa kujenga madarasa na kulipa mishahara ya walimu.

Kwa kukosa uwezo wa rasilimali, wazazi wameshindwa kujenga  madarasa hayo, hivyo kuponea madarasa yanayotumiwa na wanafunzi wa shule za msingi. Hata posho za walimu, japo ni ndogo bado inabidi wazazi washikane  mashati kuchangia.

“Tatizo kubwa ni namna ya kuwalipa walimu, Tunaiomba serikali ilichukue darasa la awali kama ilivyo kwa darasa la kwanza, isiwaachie wananchi, ‘’anasema Diwani wa kata ya Liuli, Charles Chawila.


November 2, 2012
« Previous Next »

Add a comment

Your name:
Your location:
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.