Fungua
White Orange Youth

White Orange Youth

Moshi, Tanzania

Maeneo ya ukurasa huu ni kwa Kiingereza. Hariri tafsiri

 

POLICE GENDER DESK

TAARIFA FUPI YA DAWATI LA JINSIA NA WATOTO

POLISI WILAYA YA MOSHI:

 

                 Jukumu la Askari polisi ni kutekeleza sheria na kuhudumia watu, Kulinda watu na mali zao, kuwalinda wasio na hatia dhidi ya udanganyifu au vitisho. Wewe Askari polisi, Magereza, JWTZ na Wananchi wote, Pinga ukatili dhidi ya Watoto wa Tanzania na Afrika kwa ujumla.

MAFANIKIO YA DAWATI LA JINSIA NA WATOTO POLISI (W) MOSHI:

    

       Dawati la Jinsia na watoto limetambulika na limezidi kukua ndani na nje ya nchi. Kujulikana huko kumepelekea kuamsha hisia za jamii na kuwafanya wawe na mwamko wa kutafuta huduma za Dawati la Jinsia na Watoto.

           Aidha kumekuwa na wateja wengine wanaoelekezwa kuja polisi kitengo cha dawati la Jinsia na Watoto kupata huduma hii muhimu, pia wawezeshaji wa kwenda kufundisha masuala ya Haki za binadamu na mambo mengine kama vile;

  1. Maana ya Dawati la Jinsia na Watoto
  2. Kulawiti
  3. kupiga mtoto
  4. Kutelekeza mtoto/ familia.
  5. Kutupa mtoto.

Dawati la Jinsia na watoto Moshi polisi linatoa

mafunzo mbalimbali kwa wananchi vijijini mfano, 2/10/2012 tulikuwa Makami Juu na mada iliyofundishwa ni Polisi Jamii, Dawati la Jinsia na Watoto na Utii wa sheria bila shuruti.

 

         Eneo la Makami Juu lipo Marangu- Kilema. Eneo hilo wanawake na watoto wanakosa haki zao.Hivyo ni ombi letu mfike huko mtoe hata siku mbili itasaidia sana, watoto hawaendi shule, wanawake wanapigwa na waume

Zao.

MAJUKUMU YA BABA NA MAMA KATIKA FAMILIA:

  1. Kuwahakikishia watoto maisha salama na kuendelea kuwasimamia watoto ili kuondoa hatari ya kuumia mtoto/ watoto
  2. Kuwawezesha watoto ili wajilinde wenyewe wasichana/ wavulana na mazingira hatarishi ya Kingono na uonevu.
  3. Kuwa mfano mzuri wa mtu thabiti kati ya kile usemacho na ufanyacho.
  4. Mpe pongezi mtoto anapoonyesha tabia nzuri. Hii humsaidia mtoto kujifunza maadili mema.
  5. Kuendelea kuwa karibu na watoto, kuwapatia uhuru wa kuongea na kuyasikiliza maswali yao kwani na wao wana haki sawa katika jamii.
  6. Mtoto apate haki yake ya kupata chakula na malazi.

 

Asilimia hamsini ya watanzania ni watoto na watoto ni hazina. Kila mmoja ana thamani kwa familia yake, kwa jamii yake na kwa taifa lake kwa ujumla. Sisi sote tunalo jukumu la kutekeleza haki ya mtoto chini ya kifungu cha sheria No. 21 ya mwaka 2009, sheria ya kuwalinda watoto dhidi ya mazingira hatarishi na unyanyasaji inatueleza tunachopaswa kufanya tunapomkuta mtoto katika mazingira hatarishi.

HAKI ZA MTOTO.

  1. Watoto wana haki ya kupata uhuru sawa na watu wazima, haki hizo zimeainishwa katika sheria ya haki za mtoto No. 21 ya mwaka 2009.
  2. Haki ya kuishi na kuheshimiwa.
  3. Haki za watoto wenye ulemavu.
  4. Haki ya kupata jina, utaifa na kufahamu wazazi wake (RITA).
  5. Haki ya ulinzi na usalama.
  6. Haki ya kutoa maoni/ mawazo.
  7. Haki ya kulindwa kutokana na hatari ya watu.
  8. Kuwalinda watoto kutokana na hatari ya kuonyeshwa au kutangazwa.
  9. Kuwalinda watoto kutokana hatari ya kutumikishwa. Sheria inasema mtu yeyote hatamnyima mtoto kufurahia kutumia mali ya wazazi wake.

 

MIPANGO YA BAADAYE YA JESHI LA POLISI JUU

YA DAWATI LA JINSIA NA WATOTO:

  1. Kujenga jengo maalum na kubwa (One stop Center) (Mkono kwa mkono). Jengo hilo linakuwa na ofisi mbalimbali mfano;Doctor, Nurse, Polisi, Ustawi wa jamii, wanasheria Maabara na NGOs mbalimbali. Lengo ni kutoa huduma bora kwa wakati.
  2. Kuongeza vituo vya Dawati nchi nzima.
  3. Kupatiwa vitendea kazi kila Dawati ili kufika kwenye tukio lolote dhidi ya watoto/ Vijana
  4. Kutoa elimu dhidi ya ukatili kupitia Radio, Magazeti na mikutano kwa wananchi.

                   Kwa pamoja tuwalinde watoto na vijana wetu, 50% ya watanzania ni watoto wewe una wajibu wa kumlinda Kesho ni Leo.

   Tafadhali nawasilisha.

Mtoa mada:F.1286 CPL BUTONO.P.M. KASUSURA

        

POLISI JAMII (W) MOSHI,

               DAWATI LA JINSIA NA WATOTO (W) MOSHI

             0764-015858

             0658-015858

           0786-948693.

 

11 Oktoba, 2012
« Iliyotangulia Ifuatayo »

Ongeza maoni

Jina lako:
Mahali ulipo:
Email yako:
(sio lazima)
Anwani yako ya email haitachapishwa.