Asili (Kiingereza) | Kiswahili |
---|---|
POLICE GENDER DESK TAARIFA FUPI YA DAWATI LA JINSIA NA WATOTO POLISI WILAYA YA MOSHI:
Jukumu la Askari polisi ni kutekeleza sheria na kuhudumia watu, Kulinda watu na mali zao, kuwalinda wasio na hatia dhidi ya udanganyifu au vitisho. Wewe Askari polisi, Magereza, JWTZ na Wananchi wote, Pinga ukatili dhidi ya Watoto wa Tanzania na Afrika kwa ujumla. MAFANIKIO YA DAWATI LA JINSIA NA WATOTO POLISI (W) MOSHI:
Dawati la Jinsia na watoto limetambulika na limezidi kukua ndani na nje ya nchi. Kujulikana huko kumepelekea kuamsha hisia za jamii na kuwafanya wawe na mwamko wa kutafuta huduma za Dawati la Jinsia na Watoto. Aidha kumekuwa na wateja wengine wanaoelekezwa kuja polisi kitengo cha dawati la Jinsia na Watoto kupata huduma hii muhimu, pia wawezeshaji wa kwenda kufundisha masuala ya Haki za binadamu na mambo mengine kama vile;
Dawati la Jinsia na watoto Moshi polisi linatoa mafunzo mbalimbali kwa wananchi vijijini mfano, 2/10/2012 tulikuwa Makami Juu na mada iliyofundishwa ni Polisi Jamii, Dawati la Jinsia na Watoto na Utii wa sheria bila shuruti.
Eneo la Makami Juu lipo Marangu- Kilema. Eneo hilo wanawake na watoto wanakosa haki zao.Hivyo ni ombi letu mfike huko mtoe hata siku mbili itasaidia sana, watoto hawaendi shule, wanawake wanapigwa na waume Zao. MAJUKUMU YA BABA NA MAMA KATIKA FAMILIA:
Asilimia hamsini ya watanzania ni watoto na watoto ni hazina. Kila mmoja ana thamani kwa familia yake, kwa jamii yake na kwa taifa lake kwa ujumla. Sisi sote tunalo jukumu la kutekeleza haki ya mtoto chini ya kifungu cha sheria No. 21 ya mwaka 2009, sheria ya kuwalinda watoto dhidi ya mazingira hatarishi na unyanyasaji inatueleza tunachopaswa kufanya tunapomkuta mtoto katika mazingira hatarishi. HAKI ZA MTOTO.
MIPANGO YA BAADAYE YA JESHI LA POLISI JUU YA DAWATI LA JINSIA NA WATOTO:
Kwa pamoja tuwalinde watoto na vijana wetu, 50% ya watanzania ni watoto wewe una wajibu wa kumlinda Kesho ni Leo. Tafadhali nawasilisha. Mtoa mada:F.1286 CPL BUTONO.P.M. KASUSURA
POLISI JAMII (W) MOSHI, DAWATI LA JINSIA NA WATOTO (W) MOSHI 0764-015858 0658-015858 0786-948693.
|
(Bila tafsiri) |
Ili kuhariri tafsiri, lazima ufungue. Fungua · Jiandikishe