Envaya
Parts of this page are in Swahili. Edit translations

large.jpg

Mimi naitwa Zephania Kyungai mwenyekiti wa kikundi cha sanaa WALIPO kilichoko Tengeru. Naishi na maambukizi ya virusi vya UKIMWA kwa muda wa miaka kumi. Baada ya kufuata ushauri wa daktari niliweza kuondoa usongo wa mawazo na sasa hivi naishi bila matatizo yoyote. Nafanya kazi zangu zote nahudumia familia yangu bila matatizo.
June 10, 2010

Comments (1)

Wapoli Living Positive (Tengeru) said:
Sasa hivi kikundi cha WALIPO kimechaguliwa na wilaya ya Meru kuelimisha jamii kuhusu ugonjwa wa kifua kikuu kwa kutumia sanaa mnato.Mpaka sasa tumekwenda sehemu mbali mbali za wilaya ya meru kutoa elimu hiyo.Tumefanikiwa sana kwani sanaa mnato tunayoionyesha jamii imekuwa ikiwavutia sana na tunawakusanya watu kirahisi na kuanza kuwapa somo.Maana ya sanaa mnato ni sanaa ambayo haitoi jibu.Tunaanza na kisa mkasa ambacho watu wanakuja kwa wingi kuangalia kulikoni na hapo hapo tunaaza kuvunja ukimya kwa nyimbo na baada ya hapo tunatoa igizo fupi linalohusu kifua kikuu na baada ya igizo tunatoa mada kuhusu kifua kikuu.Wafadhili wetu katika mpango huo ni shirika la PATH.
April 4, 2012 (edited April 4, 2012)

Add a comment

Your name:
Your location:
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.