Fungua
TAWI LA CHAVITA MTWARA

TAWI LA CHAVITA MTWARA

Masasi, Tanzania

Tawi la CHAVITA Mtwara kwa kifupi CHAVITA MTWARA lilianzishwa mwaka 2001 chini ya Katiba na kanuni za Matawi ya chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) kwa juhudi za Viziwi wenyewe. Pia sawa na Matawi yote ya CHAVITA Tawi linatumia nembo na Kauli mbiu ya CHAVITA ambayo ni USAWA NA HAKI. Aidha Tawi lina Dira na Utume wake katika kutekeleza malengo yake.

DIRA. Kuwa na Jamii ya Viziwi inayoishi maisha bora na yenye staha

UTUME. CHAVITA Mtwara itahakikisha kuwa Jamii ya Viziwi ina Maisha bora kwa kujijengea uwezo wa kujiamini,kujithamini,kujiendeleza,kukuza matumizi ya lugha ya Alama Tanzania na kushiriki kikamilifu katika shughuli zote za kimaendeleo,kiuchumi na kijamii kwa kushirikiana na Serikali pamoja na wadau wengine.

MAADILI

  • Uaminifu. Katika kutekeleza shughuli zake CHAVITA Mtwara inapenda kuona wanachama wake wanatekeleza majukunmu yao kwa uaminifu wa hali ya juu hasa katika kutunza mali za CHAVITA
  • Kujitolea. Pale inapobidi wanachama wanapaswa kujitolea katika kutimiza majukumu yao
  • Kuheshimu haki za binadamu. Kila mwanachama wa CHAVITA anapaswa kujua kuwa ni muhimu kuheshimu na kuzilinda haki za binadamu hasa za walio wanyonge katika jamii wakiwemo watu wenye ulemavu mbalimbali kama vile Viziwi.
  • Kushirikiana. Kila mwanachama wa CHAVITA ana wajibu wa kushirikiana na wadau mbalimbali katika kufanikikisha utendaji wa kazi wa CHAVITA Mtwara na taifa kwa ujumla
  • Kuwajibika. Kila mwanachama wa CHAVITA anapaswa kuwajibika kwa matokeo ya matendo yake mwenyewe
  • Utendaji wa kazi unaozingatia uweledi(professionalism). Kila mwanachama wa CHAVITA ana wajibu wa kutimiza majukumu yake kwa ufanisi wa hali ya juu
  • Usawa wa kijinsia. Katika utekelezaji wa shughuli zake CHAVITA Tawi la Mtwara litahakikisha kuwa ushiriki wa wanaume na wanawake unazingatiwa bila upendeleo wowote.

MPANGO MKAKATI 2013-2017

Ili kufanikisha Mpango Mkakati wake CHAVITA Mtwara imejiwelea malengo mkakati mnne ambayo ni:-

Lengo mkakati 1:Uwezo wa CHAVITA Mtwara na vikundi vyake vya wilayani umeimarika, ifikapo mwaka 2017

Lengo mkakati 2:Mawasiliano kati ya wanachama wa CHAVITA na jamii yameimarika, ifikapo mwaka 2017

Lengo mkakati 3: Vikwazo vya mawasiliano kati ya viziwi na wahudumu wa afya vimemalizika hadi kufikia mwaka 2017

Lengo mkakati 4:Utawala bora na haki za binadamu (viziwi) umeimarika, ifikapo mwaka 2017.

KANUNI ZA FEDHA

Ili kufanikisha malengo ya kimkakati haya na shughuli zingine za Asasi CHAVITA Mtwara ina Kanuni za fedha ambazo zinazingatiwa na kuheshimiwa wakati wote.