MADHUMUNI YA CHAVITA MTWARA NI PAMOJA NA:-
1. Kufanya shughuli zote zinazohusu Viziwi,Kutoa huduma na kuandaa mikakati mbalimbali kwa manufaa ya Viziwi.
2.Kuwaunganisha na kuelimisha Viziwi ili wapate hali bora ya maisha,huduma muhimu kama vile Raia wengine wa Nchi
3. Kupigania haki na usawa,ushirikiano na jumuia zingine,vyombo vya Serikali na mashirika mbalimbali yenye lengo sawasawa na Chama chetu
4. Kushirikiana na Matawi mengine moja kwa moja au kupitia Chama cha Viziwi Tanzania
5. Kufanikisha malengo ya CHAVITA
6. Kulinda na kuheshimu Katiba ya CHAVITA
7. Kuhakikisha matumizi sahihi ya Lugha ya Alama yanapewa kipaumbele na kutumiwa ipasavyo kwa Viziwi wote na Wakalimani katika Matawi. Hivyo Matawi yatabuni mbinu mbalimbali za kuboresha na kukuza matumizi ya Lugha ya Alama. pia kushirikiana na CHAVITA Makao Makuu ili kuweka mikakati ya kupata Wakalimani bora wenye uwezo wa kuwaunganisha Viziwi na Watu wengine wanaosikia
8. Kukusanya takwimu sahihi za Viziwi waliopo kwenye Matawi(Mikoa/Wilaya) zao kwa kushirikiana na Ofisi za Vingozi wa Serikali za Mitaa.

See nearby organizations
-Ada za Wanachama
-Misaada
-Michango
-Ruzuku
-Idadi ya Wanachama wa Tawi la CHAVITA Mtwara ni 6 ambao ni Vikundi vya Viziwi vya Wilaya
na Manispaa ambavyo ni:
1 Kikundi cha viziwi Wilaya ya Masasi - ME 15 KE 10 JUMLA 25
2. Kikundi cha viziwi Wilaya ya Mtwara Vijijini - ME 13 KE 3 JUMLA 19
3. Kikundi cha Viziwi Manispaa ya Mtwara/Mikindani - ME 19 KE 16 JUMLA 35
4. Kikundi cha Viziwi Wilaya ya Nanyumbu - ME 6 KE 6 JUMLA 12
5. Kikundi cha Viziwi Wilaya ya Newala - ME 6 KE 7 JUMLA 13
6. Kikundi cha Viziwi Wilaya ya Tandahimba - ME 16 KE 8 JUMLA 24
Jumla ya Wanachama katika vikundi vya Viziwi vya Wilaya kwa Mkoa wa Mtwara ni 128.