Asili (Kiswahili) | Kiswahili |
---|---|
Involvement of CSOs in abandoning harmful cultural practices in TanzaniaTanzania is a country that is extremely rich in traditions and culture, well known to treasure its heritage and pride in cultural practices. Tanzania is a harmonious culture that’s mostly based on a subtle but strong social code of respect and courtesy. The official language in Tanzania is Swahili, although many people speak English. Tanzanian people are known to be extremely friendly and polite. However, there is a growing awareness in Tanzania of the harm which certain cultural practices have on children, adolescents and women. This awareness is reflected in the emergence of NGOs and CSOs formed to campaign for the abolition of cultural practices that harm women and children. Organizations that easily come to mind in spearheading these initiatives are TAMWA, WAMA, AFRICAN UPENDO GROUP, TAWA and TUNAWEZA WOMEN GROUP which address violence against women. TGNT and SWAAT combat gender discrimination and women's cultural vulnerability to HIV/AIDS respectively. KULEANA which is tackling corporal punishment for children and TANZANIA ALBINO SOCIETY which advocates against Albino killings -- the list goes on! Many tribes in Tanzania practice widow inheritance where by widowers may “marry” a sister of their deceased wife-ostensibly to take care of her sister’s children who are also regarded as her own children as well. While there may be no negotiations or free choice on the part of the sister who is to wed her brother in law, quite often the alternative to being inherited is destitution, which, as you can imagine can be hazardous for the woman. There are also many health risks, as her husband may have been infected with HIV, or other STDs in which case she may also be infected. Another known harmful cultural practice in Tanzania is Female Genital Mutilation. A few regions in Tanzania conduct FGM for the express reason that it controls female sexuality and therefore reduces chances of promiscuity. FGM is a big reproductive health risk for women, it interferes with a woman's ability to enjoy sex, and worse, the woman may end up with fistula during childbirth as FGM scars may tear away, resulting in a massive hemorrhage which may also be fatal. In Tanzania, FGM is practiced by ten or more ethnic groups out of the country, with more than 130 ethnic groups, hence even campaigns to stop such practices are often seen by those who practice them as ethnocentric and insensitive to their cherished values and norms by outsiders. In the past 5 years there has been an increase of Albino Killings in Tanzania. The killings are associated with illogical thinking, like witchcraft, seeking wealth quickly, politics, racism etc. The eradication of such killings has been a very difficult and complicated process. The absence of witchcraft law does not help the situation at all, and lack of government readiness in increasing awareness on racism in our culture also contributes greatly in these killings. However, in recent years, efforts have been seen on implement such laws, and Tanzanians have shown a need to move quickly on this law to protect all albinos and give them their basic right to live freely amongst society. Early marriage. Girls are still traditionally discriminated against, and some as young as 11 years are withdrawn from school to be married off. There is an increase of girls who drop out of primary school because some are raised in the belief that they should be married at a very young age to elevate their families from poverty and have a good life for themselves. This leads to early pregnancies causing a list of health issues for young girls. This is also not good for the development of our country because instead of educating women so they can educate their families and be leaders in the development of the country we subject them to bear children too early depriving our country of well educated powerful women in key decision making roles in our society. Sexual harassment can also be a problem caused by harmful cultural practices in communities. In some communities in Tanzania women are viewed as objects, and its not uncommon for them to be subjected to different kinds of sexual harassment whether it be verbal or physical abuse. NGOs like the one we mentioned above, now work on letting women know about their rights and create awareness within the community about the affects of sexual harassment, and also educating society on what sexual harassment is. Harmful cultural practices also contribute in Attendance of Men to Clinic. Most cultures in Tanzania don’t encourage men to visit a clinic for sexual health, as it is seen as a big taboo. The fact that clinics are dominated by female staff and patients doesn't help men feel secure enough to attend a clinic. Our culture also does not encourage men to attend clinics with their spouse for the same reason, fear of appearing weak and the general cultural understanding. Surprisingly, hundreds of elderly women are killed every year, not because they have been legally convicted of performing witchcraft acts, but because some traditional healer has instigated the execution by convincing communities that elderly women with red eyes are all witches. Most of the elderly women with red eyes are killed mainly around Lake Zone, people fail to understand that women with red eyes are the victims of indoor pollution; they cook daily on wood stoves and inhales amounts of poisonous gas. Due to scarcity of fuel wood, sometimes cow dung is used as an alternative to firewood. Use of low quality biomass fuels like cow dung causes indoor pollution which is a hazard reflected in eyes turning red. There are many harmful cultural practices in Tanzania that threaten the development of our society. With the help of various NGOs, society is now being educated on the affect of some cultural practices on the growth of our country and many of these practices have seized to exist in some communities due to these efforts. We congratulate all NGOs that have spearheaded these initiatives and encourage others to follow their example. To participate in this discussion, add your comment below! |
Ushiriki wa asasi za kiraia katika kuachana na mila hatarishi katika TanzaniTanzania ni nchi yenye utajiri wa mila na utamaduni na hujivunia hazina za urithi wao.Utamaduni wa kitanzania ni mzuri sana wenye heshima na adabu katika jamii. lugha rasmi nchiniTanzania ni Kiswahili lakini pia watu wengi huzungumza Kiingereza. Watu wa Tanzania wanajulikana sana kwa ukarimu na upole. Kuna uelewa ambao unaendelea kukua nchini Tanzania wa madhara yanayosababishwa na tamaduni si tu kwa ajili ya watoto na vijana bali pia kwa wanawake. Uelewa huu umesababishwa kwa kuibuka asasi mbalimbali za kiraia ambazo zimekuwa zikifanya kampeni kwa ajili ya kukomesha tamaduni mbaya katika jamii.Asasi hizi ni pamoja na TAMWA, WAMA, AFRICAN Upendo GROUP, TAWA na TUNAWEZA WOMEN GROUP ambazo zinapinga unyanyasaji dhidi ya wanawake. TGNT na SWAAT hupambana na ubaguzi wa kijinsia na wanawake walio katika hatari ya kuambukizwa VVU / UKIMWI. KULEANA ambayo inakabiliana na kukomesha adhabu ya viboko kwa watoto na TANZANIA ALBINO SOCIETY ambayo inatetea mauaji dhidi ya binadamu wenye ulemevu wa ngozi (albino). Sehemu kubwa ya jamii za kitanzania wana utaratibu wa kurithi wajane, mwanaume aliyefiwa na mke wake anaweza "kuoa" ndugu wa marehemu mke wake kwa lengo la kutunza watoto wa dada yake ambao pia huonekana kama watoto wake. Familia ya mwanamke aliyefariki huwa ni jukumu lao kumpatia mkwe wao mbadala wa kumrithi mke wake aliyefariki, na familia inaweza kumchagua binti yeyote kutoka kwenye familia bila hata makubaliano kati ya mume na binti anayemrithi dada yake. Utamaduni huu ni wa hatari sana maana unaweza kuleta maambukizi ya ukimwi kwa mwanamke anayerithiwa na mume aliyefiwa na mke, inawezekana dada yake alikufa na VVU naye pia atapata maambukizo hayo.
Ndoa za mapema. Wasichana bado wanabaguliwa katika jamii nyingi za kitanzania, kwasababu wasichana wadogo wenye umri kuanzia miaka 11 wanaachishwa shule na wazazi wao ili waolewe. Kwa upande wa afya jambo hili ni ni hatari, kwa sababu viungo vya msichana huyu havijakomaa kwa hivyo wengi viungo vyao hupasuka wakati wa kujamiiana, na hivyo kusababisha maambukizi ya VVU au mimba za mapema. Utafiti unaonyesha wasichana wengi wameachishwa shule ili kuolewa au kujiingiza mapema katika vitendo vya ngono ili kujitegemea kifedha hasa ukosefu wa ajira na umaskini miongoni mwa wasichana, ukosefu wa taarifa kuhusu masuala ya ngono na ujinga na ukosefu wa elimu miongoni mwa wasichana. Unyanyasaji wa kijinsia. Unyanyasaji wa kijinsia ni pamoja na kumtolea matusi mwanamke, kumshika na kumgusa mwili wake bila ridhaa mfano kwenye nywele, makalio, au matiti. Kuonyesha picha za utupu za wanawake, kumwonyesha mwanamke picha za ngono bila ridhaa yake na kumwongelesha maneno ya kashifa mwanamke wakati anapopita mbele ya wanaume, kumbaka na kumpiga mke wako kama ishara ya upendo katika baadhi ya makabila. Mahudhurio ya Mwanaume kliniki. Katika jamii nyingi za kitanzania kina mama tu ndio huwa wenye jukumu la kuhudhuria kliniki. Wakati pia ni jambo la muhimu sana kwa kina baba kuwasindikiza wake zao kliniki ili kupata ushauri na nasaha mbalimbali, pia kupata elimu juu ya masuala muhimu sana yahusuyo uzazi wa mpango na VVU. Pamoja na hayo yote serikali inapaswa kujaribu kuzifanya kliniki ziwe rafiki kwa wanaume kwa kutoa kipaumbele kwa wanawake ambao wanahudhuria kliniki na waume/wapenzi zao na pia wanaume ambao huleta watoto wao. Mauaji ya wanawake wenye macho mekundu. Cha kushangaza mamia ya wanawake wazee wanauawa kila mwaka kwa tuhuma za uchawi baada ya kupata wao wanachokiita ukweli kutoka kwa baadhi ya waganga wa jadi.Wengi wa wanawake wazee wenye macho mekundu wanauawa hasa katika ukanda wa ziwa victoria, watu hushindwa kuelewa kwamba wanawake wenye macho mekundu wameathiriwa na moshi wakati wa kupika. Wanapopika kila siku kwa kutumia majiko ya kuni wanavuta hewa yenye kiasi cha gesi ya sumu. Kutokana na uhaba wa kuni, wakati mwingine mavi ya ng'ombe hutumika kama mbadala kwa kuni. Hivyo kwa kutumia nishati za kupikia ambazo hazina ubora husababisha macho kuwa mekundu.
a
|
Historia ya tafsiri
|