Base (Icyongereza) | Kiswahili |
---|---|
When you first register for Envaya, you are automatically logged in to your new account on Envaya. However, the next time you return to envaya.org, you will probably be "logged out", and will have to log in first before editing your website. In order to edit your website, go to http://envaya.org in your web browser and click Log in, as shown below: Then, type your organization's username and password, which you selected when registering your organization for Envaya, and click the blue button to log in. If your username or password was entered incorrectly, Envaya will display a red error message. Try typing your username and password again, making sure that your password is entered using the same uppercase or lowercase letters as when you registered, then click the button again. Resetting Your PasswordIf you are unable to log in to Envaya, you can reset your organization's password.
If your organization does not have an email address, or if you cannot reset your password using the steps above, go to http://envaya.org/envaya/contact and send us your contact information so we can verify that you should have access to the account. |
Ukijiandikisha Envaya unaingia moja kwa moja kwenye akaunti yako mpya. Lakini wakati mwingine unaweza kurudi envaya.org, huenda ukawa umefungiwa nje na unahitaji kuingia tena kuhariri tovuti yako. Ili kuhariri tovuti yako, nenda http://envaya.org katika web browser yako na bonyeza Ingia, kama ilivyoonyeshwa hapa chini: Kisha andika jina la mtumiaji la shirika lako na neno la siri yaani password, ambazo ulizichaguwa wakati wa kusajili asasi yako, na bonyeza batani ya bluu kuingia ndani Kama umekosea kwenye kuandika jina la mtumiaji au neno la siri, ujumbe mwekundu utajitokeza. Jaribu kuandika jina na neno la siri lako tena, na kuhakikisha kuwa unaliingiza neno la siri kwa kutumia herufi zilezile ulizotumia ulipofungua akunti yako, kama ni herufi kubwa au ndogo, kisha bonyeza batani ya bluu tena. Kubadilisha Neno la SiriKama huwezi kuingia kwenye akaunti yako ya Envaya, unaweza kubadilisha neno la siri ya akaunti yako.
Kama asasi yako haina anwani ya barua pepe, au kama huwezi kubadilisha neno la siri kutumia hatua ya juu, nenda http://envaya.org/envaya/contact na tutumie mawasiliano yako ili tuweze kuthibitisha kama wanapaswa kuingia kwenye akaunti hiyo. |
Ibyasobanuwe
|