Base (Swahili) | English |
---|---|
KIKAO cha Kikundi cha Waishio na Vrusi vya UKIMWI na Mkurugenzi wa Taasisi ya kupambana na UKIMWI Kitangari chaleta changamoto. Kikao hicho kilichofanyika tarehe 20 Agosti,2010 katika ukumbi wa kituo cha Afya Kitangari chini ya mlezi wake Ndg.Florence Mnipa, kimeeleza changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo wana mtandao hao. Kubwa kabisa ni pale walipomwelekeza Mkurugenzi wa Taasisi ya kupambana na Ukimwi Kitangari kwamba jamii inayowazunguka inawanyanyapaa. Mkurugenzi alihitaji kujua ni kwa kiasi gani unyanyapaa upo kwenye makazi yao. Maelezo waliyoyatoa walisema,kwa wale wanaotoka Kata ya Malatu idadi yao wapo wengi lakini wanaojitokeza ni 11 tu wengine hawajitokezi kuchukua dawa za ARV sababu kila wanaporudi Hospitalini mitaa wanayopita huwapachika majina ya dhihaka kama; wasanii,wafiwa watarajiwa.
Ombi lililotolewa na Mtunza hazina wa mtandao wa waishio na VVU Ndg.Saidi Shamba mwenye picha hiyo hapo kulia,alisema itolewe elimu kwa jamii ili waelewe na kuelimika kuhusu umuhimu wa kuwajali waishio na VVU kusudi walioanza Dozi wasikatishwe tamaa ili kuokoa vifo vinavyotokea kabla ya wakati wake kutimia.
Pia wajumbe, picha hapa chini walionesha kukerwa na tabia wanayowafanyia wenzao kwenye makazi wanakoishi ya kuwanyanyapaa.
Katibu wa kikundi hicho Ndg.Asia Mtavala Mwisho alimalizia kwa kusema kijiji anachotoka yeye anaitwa ukubwa wa mbuyu unyanyapaa upo kiasi kikubwa tena kinaudhi sana. Mkurugenzi wa Taasisi ya kupambana na UKIMWI Kitangari amewaambia wana mtandao waishio na VVU kwamba atashirikiana nao ili kwa kuanzia kupunguza kasi ya unyanyapaa hata kama si kuziba maneno machafu hayo, lakini yapungue. Mkurugenzi alisikitishwa na tabia ya unyanyapaa kuendelea kubaki katika Tarafa ya Kitangari.
|
Group Session Vrusi living with HIV and Director of the Institute for AIDS Kitangari brings challenges. The meeting was held on August 20, 2010 in Hall Health Centre under the guardian Kitangari Ndg.Florence me, kimeeleza challenges they experience and they have the internet. Is quite large when they pomwelekeza Director of the Institute of fighting AIDS Kitangari inawanyanyapaa society around them. Director wanted to know how much stigma there is in their homes. Details were yoyatoa they say, for those from Cut Malatu their numbers are many, but they appear are only 11 others did not venture to take medicine for ARV because all they try to hospital streets they passed it to fit the names of derision as: artists, lost potential.
The request made by the Treasurer of the network living with HIV Ndg.Saidi field with the picture then right, he said should be educated to the community to understand and learn about the importance of caring for people living with HIV that were started Dose not katishwe desire to save deaths vinavyotokea before its time fulfillments.
Also, members, photographs below were expressed offended by the behavior they did their counterparts in homes where the kuwanyanyapaa.
Secretary of the group Ndg.Asia Mtavala Finally he concluded by saying he wants the village is called the size of baobab stigma is very much longer kinaudhi. Director of the Institute for AIDS Kitangari has told the children living with HIV network that will share with them in order to begin to slow down the stigma, even if you do not plug these dirty words, but yapungue. Director was disappointed with the attitude of stigma continue to remain in Division Kitangari.
|
Translation History
|