Asili (Kiswahili) | Kiswahili |
---|---|
SHUGHULI ZIFANYWAZO NA LINGONET ZINAZO WIANA NA MPANGO KAZI WA TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA –TANZANIA
UTANGULIZI Mtandao wa AZAKi wilaya ya LINDI LINGONET ni asasi iliyoanzishwa mwaka 2002 na kusajiliwa rasmi mwaka 2003,ikiwa na wanachama waanzilishi 13,LINGONET mpaka kufikai mwaka 2014 inawachama 25 ingawa inahudumia asasi zipatazo 60 zilizopo katika wilaya ya LINDI baadhi yao si wanachama wa Mtandao kwa vile kujiunga na mtandao ni khiyari.
Malengo ya kuanzishwa kwa LINGONET ni kujenga uwezo wa asasi wanachama,kuwa kitovu cha kupata taarifa mbalimbali za kitafiti,kisera na kiutendaji,kuwa kiungo kati ya AZAKi,serikali na wadau wa maendeleo na kuratibu shughuli za wanachama katika kuifikia jamii. Katika utekelezaji wa shughuli zake LINGONET imegawanyika katika vitengo saba (7)
Ingawa kitengo cha ushawishi na utetezi ni mtambuka kutegemea na agenda husika LINGONET hujikita zaidi katika kushawishi mabadiliko katika sera,sheria,miundo,mtazamo na mazoea ya jamii katika kushughulikia michakato mbalimbali ya kimaendeleo
MRADI WA WAPE HAKI WENGI WASIO NA SAUTI Mradi huu unatekelezwa na LINGONET kwa ushirikiano na SAVE THE CHILDREN kwa ufadhili wa SIDA/Sweden toka mwaka 2009 na unatarajiwa kuisha mwezi Desemba mwaka 2014
ENEO LA MRADI Mradi wa wape haki wengi wasio na sauti unatekelezwa katika wilaya 7 Tanzania LINGONET ikihusika katika wilaya za Lindi,Kilwa na Rungwa,wilaya nyingine zinazotekelezwa mradi huu ni Temeke,Handeni,Same na Arusha
MALENGO YA MRADI Mradi una malengo makuu matatu ambayo ni
UTEKELEZAJI WA MRADI Mabaraza ya watoto Mradi ulianza kwa kufanya uchaguzi wa mabaraza ya watoto katika ngazi za vijiji,kata na wilaya kwa kufuata mwongozo wa taifa ulioandaliwa na wizara ya jamii,jinsia na watoto,uchaguzi hufanyika kila baada ya miaka miwili kama sheria ya uundwaji mabara ya watoto unavyotaka
Shughuli za LINGONET katika mradi huu ni kuratibu utekelezaji wake ambao kimsingi unatekelezwa na asasi washirika katika wilaya za Lindi,Kilwa na Ruangwa. Ilikuhakikisha shughuli za mradi zinatekelezwa kama zilizovyopangwa mratibu ameajiriwa kusimamia,kufuatilia na kutoa msaada wa kiufundi kwa maafisa maendeleo wasaidizi wanaofanya kazi sambamba na watoto katika ngazi zote.
Mabaraza watoto 90 katika wilaya za Kilwa,Ruangwa na Lindi yameundwa na mabaraza matatu ya wilaya sambamba na baraza moja linalojumuisha wilaya zote tatu,kazi ya mabaraza haya ni kujenga uwezo wa watoto katika kufahamu haki zao,namna ya kuibua vitendo vya ukiukwaji haki za watoto,ufanyaji wa rufaa kwa waathirika,namna ya kuwasilisha maoni yao katika vikao vya wafanya maamuzi na kuhamasisha wajibu wa mtoto sambamba na kudai haki zao.
Mabaraza ya watoto ya wilaya hukutana kila baada ya miezi mitatu kupitia mipango kazi yao na kutathimini utekelezaji wake na kupokea taarifa ya mabaraza ya kata yanayokutana kila mwezi kujadili taarifa ya mabaraza ya vijiji/mitaa yanayotakiwa kukutana kila wiki,LINGONET tunafuatilia ili kuona kama muundo wa mabaraza umefuatwa kwa kuzingatia jinsia,makundi maalumu na idadi ya watoto wanaotakiwa kuunda mabaraza na ukusanyaji wa matukio ya uvunjwaji wa haki za watoto namna zinavyoshughulikiwa
SHERIA YA MTOTO 2009 Mradi pia unajukumu la kufundisha na kueneza sheria ya mtoto 2009 mikataba ya kikanda na kimataifa juu ya haki ya mtoto kwa wadau mbali mbali wa maendeleo na wafanya maamuzi ili kuhakikisha jamii ina ifahamu na kuifuata sheria hii. Hivyo LINGONET imeratibu utoaji mafunzo kwa watendaji wote wa vijiji,mitaa na kata,maafisa wa polisi wanasimamia dawati la jinsia,waheshimiwa madiwani.mahakimu,waratibu wa elimu kata,na asasi zinazofanya kazi za watoto katika wilaya za mradi zinazoratibiwa na LINGONET. Aidha machapisho mbalimbali kuhusu haki ya mtoto yamesambazwa kwa jamii ili kujenga uwelewa na kubadili mtazamo wa jamii kuhusu haja ya kulinda na kuheshimu haki ya mtoto ambayo ni haki ya binadamu. watoto 180 wa mabaraza 3 ya wilaya na 2520 wa mabaraza 90 ya kata nao wamepata mafunzo ya sheria ya mtoto 2009 kupitia mabaraza yao.
UTAMBUZI WA VITENDO VYA UKIUKWAJI HAKI YA MTOTO Kitabu cha usajili wa vitendo vya ukiukwaji haki ya mtoto vimesambazwa kwa watendaji wote wa vijiji na mitaa ili kuorodhesha vitendo vya ukiukwaji wa haki ya mtoto ,aina vitendo hivyo na hatua zinazochukuliwa,watendaji wamepata mafunzo namna ya kujaza vitabu hivi,utunzaji wa kumbukumbu na ufanyaji rufaa wa matukio yanayobainika, mradi unashirikiana na maafisa maendeleo ya jamii katika wilaya husika ilikuhakikisha uendelevu baada ya mradi kumalizika lakini pia waweze kuyasimamia vema mabaraza ya watoto ambayo kwa sasa yanasimamiwa kwa karibu na asasi washirika wa mradi chini ya ulezi wa watendaji wa mitaa/vijiji na kata
MAFUNZO YA VYOMBO VYA HABARI JUU YA HAKI YA MTOTO Mabaraza ya watoto katika ngazi zote wamepata mafunzo juu ya matumizi ya vyombo vya habari,umuhimu wake na namna ya kujenga mahusiano bora na wanahabari,mashindano ya insha na makala zinazoelezea shughuli za watoto na mazingira yao yamekuwa yakifanyika kila mwaka ili kujenga uwezo wa watoto kutangaza shughuli zao na kueneza ujumbe mbalimbali katika jamii. Watoto wa mabaraza wamekuwa wanashirikishwa katika maadhimisho ya mtoto wa afrika kila mwaka na kuwasilisha ujumbe wao kwa jamii kupitia ngoma ,nyimbo,ngonjera na risala. Pia waandishi wa habari wamepewa mafunzo juu ya namna ya kufanya kazi na watoto,kujenga tabia ya kuwasikiliza na kuheshimu mawazo yao.na mradi umeunda Mtandao wa wanahabari za watoto TAJOC kitaifa na una wanachama katika wilaya za mradi
MAFANIKIO
CHANGAMOTO
|
(Bila tafsiri) |
Ili kuhariri tafsiri, lazima ufungue. Fungua · Jiandikishe